top of page

MAOMBI / PRAYERS ~05

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi…

II) MAOMBI YA KUSIFU NA KUABUDU

Kama vile ilivyo nyimbo za kusifu na kuabudu ndivyo ilivyo maombi ya kusifu na kuabudu. Maombi ya namna hii yanaeleza ukuu na uweza wa Mungu pamoja na kuonesha hali yote ya kumtegemea Bwana. Mwombaji aweza akawa mtu yeyote si lazima awe mwimbji. Ni vyema kila mwombaji ajifunze kumuelewa Mungu alivyo ili moyo wake ujawe na maneno ya kumsifu na kumwabudu Mungu.

Kwa bahati mbaya maombi ya kusifu na kuabudu hayafanyiki sana kwa maana watu wengi wanataka kuomba ili kupewa kitu,na kusahau kumimina sifa mbele za Mungu kwa kazi kubwa Bwana aliyowafanyia. Tunaposema “kusifu” tuna maana ya kumwelezea Bwana alivyo,mfano Yeye Bwana ni mkuu sana,umetukuka na kumwabudu Bwana ni kitendo cha kumtegemea yeye mfano wewe Bwana ndio kimbilio langu,kwako nakimbilia n.k

Tena MUNGU hupendezwa sana na maombi ya kusifu na kuabudu,kwa maana ni ibada yenye nguvu sana. Kwa kuwa Yeye huketi kwenye sifa za watu wake“Na Wewe U Mtakatifu,Uketiye juu ya sifa za Israeli.” Zab.22:3.

Kumbuka; Bwana hutushindia vita na watesi wetu pale tunapokaza kumsifu Yeye katika Roho na kweli. Fikiria ; upo katika vita kali,labda adui yako amekuinukia kiasi kwamba umekosa msaada kwa ndugu zako hata rafiki zako wamekutenga, lakini ukaanza kumgeukia Mungu huku ukimuinua na kumtukuza ukisema;

Wewe ni Mungu,Bwana wa vita,Mungu mzuri,mwenye nguvu ninakuabudu…. hata kwa hili ninalopitia sasa,bado wanipenda ninakuabudu Eeh Bwana Yesu,pokea sifa na utukufu maana wastahili….N.K” Ukiwa na tabia ya kufanya hivyo hata katika mapito yako,ujue Bwana ni mwaminifu mno. Atakushindia isivyo kawaida! Ebu angalia mfano huu; Namna ile Bwana alivyowapigania Wayahudi katika kipindi cha Yehoshafati mfalme wa Yuda.

Biblia inasema katika (2 Nyakati 20:1-2) Akina Yehoshafati waliinukiwa na mataifa makubwa na ukiendelea kusoma utagundua kwamba Wayahudi hawakuwa na msaada wowote wa kupigana na watesi wao isipokuwa kumgeukia Mungu tu. Walipomgeukia,wakaanza kumsifu Bwana na kumwabudu kwa uzuri na utaratibu wote,na angalia kile kilichofuata. Biblia inasema Bwana akawapigania hata wakateka nyara za adui zao.

Kumbe! Kusifu na kuabudu ni dawa!!!Tena ni ushindi kwa adui zako. Si jambo jepesi hili,lakini inawezekana. Kumbe,vita si yetu bali ni ya Bwana,kwa maana Yeye Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki ( 1 Samweli 17:47 ) Lakini ni pale ambapo tunapokuwa tumejitoa kidhati kwa Bwana,naye Bwana hupigana mwenyewe. Kumbuka; ili uweze kusifu na  kuabudu,unapaswa kujifunza sifa na tabia za Mungu. ( Tafuta somo hili la sifa na tabia za Bwana,hapa kwenye blogu hii)

ITAENDELEA…

Kwa msaada zaidi wa maombi,naomba usisite kunipigia kwa simu yangu hii~mimi nipo karibu nawe kwa maombi piga;+255 655 11 11 49/683 866 900

Mchungaji Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page