top of page

MAMLAKA YA MWAMINI~05

Na Mch Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Ukamilifu wa mamlaka yoyote ni uwepo wa “nguvu” Kwa maana mamlaka pasipo na nguvu bado hajawa mamlaka. Mamlaka ya mwamini nayo hutegemea nguvu,ili kuwa mamlaka kamili. Nguvu iliyopo katika mamlaka ya mwamini ni nguvu ya Kristo Yesu. Nguvu zake ni tofauti kabisa na nguvu zozote zile kwa maana nguvu zake Kristo ni “uweza wa Kifalme” Isaya 9:6

Uweza wa kifalme ni nguvu ya kuamuru visivyoonekana kuonekana. Kama uonavyo mfalme wa kawaida hutumia uwezo wake wa kumwambia huyu njoo naye huja,na yule nenda kule naye huenda. Yesu Kristo ndiye Mfalme wa wafalme,kwa maana Neno lake ni sheria,akitamka,imekuwa hakuna ajument yoyote. Hivyo uweza huu ameumilikisha kwa mtu aliyeokoka,ili kusudi kumtambulisha aliyeokoka kwamba anayo mamlaka dhidi ya falme nyingine zote. Lakini ndani ya mamlaka ya mwamini kuna mambo mawili yanayoleta nguvu,kuna “jina la Yesu na damu yake

  1. Jina la Yesu

Huwezi kutenganisha mamlaka iliyopo ndani ya Yesu na jina lake. Ndani ya jina la Yesu ipo mamlaka ya kipekee na ndio maana tumepewa jina YESU lililo juu ya majina yote ( Yohana 14:13-14).Tunapolitumia jina YESU tunatumia mamlaka iliyopo ndani yake. Katika hali ya kawaida jina limebeba nafasi au uwezo wa mwenye jina. Kwa mfano unapolitaja jina la Mh. John Pombe Magufuli,jina hilo limebeba kazi,nafasi aliyonayo Mh. Magufuli kama rais wa Tanzania wa awamu ya tano. Na unapolitaja jina YESU unataja ukuu wa aliouweka ndani ya jina YESU.

Ndani ya Jina Yesu,kuna nguvu ya kipekee. Na ndio chanzo kikuu cha mamlaka ya mwamini,kwa maana hakuna mamlaka ya mwamini pasipo jina Yesu. Angalia mfano wa katuni hapo juu,utaona huyo mmoja akiwatangulia wenzake. Na wenzake wote wamekua wafuanzi wake,wanaitwa kwa jina lake,hii ni kuonesha watu wote hutumia kibali cha jina la kiongozi wao,na kwa sababu hiyo wana nguvu kwa maana kiongozi wao yupo mbele yao.

Katuni hiyo inatufundishwa kitu kwamba Yesu ndio kiongozi wetu yupo mbele yetu,nasi tunatembea katika nyayo zake yeye,tunaitwa kwa Jina lake Yeye kwa maana fahari za nguvu zetu hutegemea Jina lake. Ukitaja tu jina Yesu,basi hata kuzimu inataharuki,maana wanajua jina hilo. Popote Jina Yesu,lina nguvu ya kimamlaka.

Ngoja nikupe mfano;

Chukulia katika hali ya kawaida,wewe unatumia jina la mmoja wa mtu mashuhuri duniani,tena ni mtu tu! labda tuseme ni Obama ( aliyekuwa rais wa Marekani),Sasa ukiingia mahali na wakatambua wewe ni wa akina Obama. Basi ujue waliokuzunguka mahali hapo watakuona  tofauti,wengine wataogopa,wengine watajipendekeza,yaani basi tu !!!! Kwa sababu ya jina tu!!! Na ndivyo hali ilivyo unapotumia jina YESU,ulimwengu wa roho hautulii,lazima upate shida!!!! Lakini Jina Yesu litakuwa na nguvu sana kwako ikiwa wewe utakuwa ni wa Yesu/mali yake yaani umeokoka na umekubali kutembea katika nyayo zake mfano wa katuini hapo juu,(Angalia katuni hiyo hapo juu,utajifunza kitu)

ITAENDELEA….

Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900

Namba ya what’s app ni .+255 746 446 446

Mchungaji Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comentarios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page