MAMLAKA YA MWAMINI~04
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 14, 2018
- 2 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
03.Mamlaka juu ya miji ( Luka 19:17)
“ Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi. ” Luka 19:17
Kuna wenye mamlaka katika miji,hata katika ulimwengu wa roho kuna wanaotawala miji. Kuna miji mingine ipo chini ya tawala za nguvu za giza,yaani mwenye kutawala miji hiyo ni ibilisi na wakala zake. Katika miji kama hiyo,ujue hakuna wema utakaotendeka,bali miji hiyo itatawaliwa na matukio ya ajabu ajabu siku zote kama vile vifo vya kichawi chawi,magonjwa n.k. Neno la hapo juu tunaona Yesu akimpa mamlaka yule mwaminifu,kwamba awe na mamlaka juu ya miji kumi,hii ina maana mtu anaweza akatawala mji kiroho ( hata kimwili). Adui ibilisi,naye aweza kushika mji fulani kwa lengo la kuthibiti maendeleo ya mji.
Chanzo kikuu cha ibilisi kutawala mji inatokana na hali mbaya ya kiroho ya waasisi wa mji huo pale walipoukabidhi mji katika nguvu za giza. Pia uovu uliofanywa katika mji ni lango la ibilisi kutawala mji huo. Lakini nataka ujue kwamba mwamini anayo mamlaka ya kushughulikia miji iliyotekwa na adui. Mwenye mamlaka ya Kristo kama wewe unayo nguvu ya kukomboa mji wako. Hivi unajua hata nyumba yako ni mji? Ndio huo ni mji mdogo,na unapaswa kukombolewa!!!
Kumbuka; watawala wa mji huitwa “wakuu wa mji”,hao wakuu ndio ufanya maamuzi ya namna gani mji uende. Wakuu hawa wanaweza wakawa ni binadamu kama wewe ila nyuma yao kuna nguvu inayowaendesha katika utawala wao. Na mara nyingi wakuu wa mji huendeshwa na ngvu za giza,ndivyo inavyokuwaga! sasa ikiwa mkuu wa mji wako ni mtu anayetegemea nguvu za giza kuongoza mji basi ujue ataufunga mji juu ya madhabahu za giza na matokeo yake ni uovu utakithili,haki haitakuwepo,na mabaya ya kila aina yatakithili!!!
Na ndio maana kuna umuhimu sana ya mkuu wa mji awe ni mtu aliyeokoka,ili mamlaka yake ya Kristo yenye haki,upendo na huruma kwa wote ionekane. Tambua hili,wewe ni mwenye mamlaka katika mji wako! Kwa kuwa mamlaka juji huo unayo,unapaswa sasa kuitumia mamlaka hiyo,kumpokonya adui mji wako,apende asipende!
Ebu chukulia mji wa nyumbani mwako umetekwa na mtu labda mwanamke mwenzako kauteke kiasi kwamba hata mumeo kawekwa chini,na huyo adui ndiye anayetamba katika mji huo. Pesa ya mumeo,uchumi wako na maendeleo kwa ujumla yako yapo chini ya mwanamke wa nje. Hapo usikubali hata kidogo mtu mwingine ateke mji wako,maana wewe ndio mwenye mji huo,na mamlaka Bwana amekupa. Kitu kikubwa cha kufanya ni kupambana naye kiroho kwa maombi mpaka kieleweke!!!
Kwa maombezi na msaada zaidi piga sasa kwa +255 683 877 900
Namba ya what’s app ni+255 746 446 446 .
Mchungaji Gasper Madumla.
UBARIKIWE
Comments