MAMLAKA YA MWAMINI~03
- Mch. Gasper Madumla
- Dec 29, 2017
- 2 min read

Na Mch. Gasper Madumla.
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
02. Mamlaka juu ya pepo na magonjwa ( Luka 9:1)
Kila mwamini katika Kristo amepewa mamlaka hii ya kutoa mapepo pamoja na kuponya magonjwa. Na mamlaka hii inafanya kazi hata sasa. Neno linasema “ kawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.” Neno “ akawaita’‘ lina maana aliwajua kwanza,akawapenda na kuwaleta kutoka upande mmoja hata upande wake Yesu. Leo hii wewe,ukiwa kama umeokoka,ujue nawe “umeitwa”. Kumbuka ;wale wote aliowaita aliwapa kitendea kazi kinaitwa Roho mtakatifu na ndani yake akaweka “uwezo na mamlaka” juu ya mapepo wote bila kujali aina ya pepo,bali pepo wote wawe chini ya aliyeitwa. Pia mamlaka juu ya kuponya magonjwa yote.
Lakini nataka ufahamu neno hili hawa walioitwa walikuwa ni wanafunzi wa Yesu,kuonesha kwamba alikwisha wachagua mapema kisha ndipo akawaita na kuwapa uwezo na mamlaka. Tafsiri ya kuwaita wanafunzi inaweza ikawa na maana mbili hivi,maana ya kwanza ilikuwa ni watu waliookoka kisha wakaketi kwenye Neno la Kristo hata wakafanyika wanafunzi.Pili,ni watu walioitwa na kupewa uwezo na mamlaka moja kwa moja kisha wakaendelea kubaki katika uanafunzi.
But kitu cha muhimu ni kwamba kuna mamlaka juu ya mapepo yote na magonjwa yote,mamlaka hii imetoka kwa Bwana Yesu,mkuu wa mamlaka zote. Kumbe hakuna cha kuogopa pepo wala maradhi kwa maana yote hayo yapo chini ya mamlaka iliyopo ndani yako. Huitaji kujifunza elimu ya mapepo na majini ili uwajue ndipo uweze kuwatoa,bali unahitaji kujua juu ya mamlaka ambayo Kristo aliyoiweka ndani yako.
Hivi,jiulize; Kwa nini Yesu aliamua kuweka uwezo huu wa kutoa mapepo yote na kuponya maradhi? hilo ni swali muhimu sana,but jibu lake ni kwamba Yesu alitaka watu wafunguliwe kutoka katika utawala wa giza,na kuamishwa kwake. Yesu ni mwenye huruma ya kuwajua watu wake waliofungwa . Ukijitambua wewe,kwamba unayo mamlaka juu ya mapepo na maradhi,hautabaki kama hivyo ulivyo. Ebu anza sasa kutambua hilo,kisha chukua hatua ya kuutangazia ufalme wa giza kwamba wewe si wa kawaida,una mamlaka na una utiisho dhidi yao. Kwa sababu ili mamlaka ifanye kazi inahitajika uanze haya mazoezi ya kuutangazia ulimwengu wa roho!
Sasa ebu tazama picha ya hapo juu – Unajifunza nini kupitia picha hiyo? Je unamwona huyo kiongozi mkubwa aliye mwekundu? kisha si unaona wote wameshikana wakielekea kule kiongozi wao anakowaambia waende. Moja ya jambo muhimu la kujifunza hapo,ni kwamba Mamlaka juu ya mapepo na maradhi inatolewa na kuongozwa na kiongozi mmoja aitwaye Yesu Kristo.
Then,ili mamlaka hiyo ifanye kazi ipasavyo unapaswa kufuata maelekezo ya mtoa mamlaka kama unavyowaona hao katuni wengine wanavyofuata maelekezo kwa kutembea sawa sawa na mtoa maelekezo. Ukiwa mtii wa kumsikia mtoa mamlaka hiyo,basi ujue hakuna pepo lolote litakaloweza kusalia,bali ni lazima litatolewa tu. Angalia tena pia hiyo ya katuni hapo juu,kisha utajifunza mambo mengi zaidi ambayo hata sijayasema hapa…
ITAENDELEA….
Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900
Namba ya what’s app ni .+255 746 446 446
Mchungaji Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comments