top of page

MAMLAKA YA MWAMINI~ mwisho (06)

Na Mch. Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Damu ya Yesu;

Hili nalo ndio jambo la pili linaloleta nguvu katika ma ya mwamini kwa maana kuna nguvu ndani ya damu ya Yesu Kristo. Ebu fikiria pale tunapotiisha mapepo,nguvu za giza kwa damu ya Yesu. Damu ya Yesu ni damu iliyotofauti kabisa na damu yoyote ile,haifanani na chochote,kwa maana damu hii ina vinasaba/DNA ya Mungu mwenyewe,haijachanganywa na chochote,ni damu halisi. Hivyo ina uwezo uletayo mamlaka kwa mwamini pale anapoitumia ( Lakini,mwamini ni lazima ajue,ajitambue na kuamini ndipo itakapofanya kazi)

5. Mamlaka ya kifamilia / ukoo

Mwamini katika Kristo amepewa mamlaka juu ya familia yake na ukoo wake kwa ujumla. Kama ujuavyo kwamba kila familia ina kiongozi wa familia,ina msemaji wake pia. Labda kiongozi aweza kuwa ndio msemaji wa familia hiyo. Ukoo nao ni hivyo hivyo,katika ukoo kuna kiongozi/msemaji wa ukoo kutegemea umri/utu uzima wake au kutegemea nafasi ya heshima ya mtu wa kiukoo. Watu waliopewa dhamani ya kusimamia mambo ya kifamilia au kiukoo ni watu wenye mamlaka.

Mwamini yeyote akiwa ndani ya Kristo,bila kujali umri wake wala nafasi yake ya ukoo,mtu huyo ni mwenye dhamana ya kuongoza familia na ukoo pia. Ikiwa wewe ni mwamini katika Kristo/umeokoka,basi uje unayo kazi ya kuongoza vyema famila na ukoo kwa ujumla. Maongozi yako yanaanzia rohoni mahali mamlaka yako ilipo. Nikuulize; Unataka familia / ukoo wako uweje? uendeleaje? Vile utakavyo unapaswa ushughulikie katika ulimwengu wa roho mapema,unatiisha mambo katika familia yako na hatimaye yanakuwa katika Jina la Yesu

Tutafakari picha iliyopo juu;

Picha hiyo ni katuni wawili wanaoonekana wamembeba mwenzao. Na huyo mwenzao kuna mahali hasa/maalumu anakoelekea,(inavyoonekana kule aendako ni sehemu muhimu). Lakini hawezi kuelekea kule anakotaka kwenda yeye mwenyewe isipokuwa “amebebwa” Sasa nataka upate picha hii,wale waliombeba ni wana ukoo fulani,watu waliookoka. Wakitumia mamlaka yao ndani ya Kristo kumwongoza na kumbeba kiongozi wa familia/ukoo mahali ambapo wao wanataka aelekee.

Kumbe ni muhimu sana kwako wewe uliyeokoka,kuitumia mamlaka yako katika familia/ukoo wako ,ili kusudi familia yako iende vizuri. Wengi leo wamekuwa wakilalamika sana pale familia inapoyumba,lakini ni watu hao hao ambao hawakufanya chochote/hawakutumia mamlaka yao ndani ya Kristo. Hata wewe,usisubiri mpaka mambo ya familia yako yamearibika ndipo uchukue hatua,anza sasa!

Mamlaka juu ya dhambi ( Luka 5:24)

“ Lakini, mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (alimwambia yule mwenye kupooza). Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende zako nyumbani kwako.” Luka 5:24

Mamlaka juu dhambi ni aina ya mamlaka muhimu sana kwa mkristo,ni pale unapoweza kuiamuru dhambi fulani baada ya toba,kwamba isichukue nafsi ndani yako. Mamlaka hii pia inafanya kazi kwa kumuombea mtu toba hata pasipo mtu huyo kuomba na wewe. Mfano unaweza ukawa una mgonjwa aliye mahututi labda hawezi kusema,amekata kauli lakini wewe ukamuombea na kumpaka mafuta ya Roho mtakatifu na yule mgonjwa watasamehewa ikiwa utaomba kwa imani. (Yakobo 5:14-15)

Kama kuhani wa Bwana,umepewa mamlaka juu ya dhambi. Tazama Yesu alivyosema kwamba Yeye anayo mamlaka juu ya dhambi,na kwa mamlaka hiyo hiyo ipo ndani yako wewe uliye ndani ya Yesu. Hili ni jambo la ajabu kidogo,kwa maana tunafahamu kwamba ili mtu ajibiwe maombi yake ni lazima aombe lakini katika mamlaka ya namna hii,inamgusa hata yule asiyeomba aweza kusame hewa dhambi zake.

Angalia mfano mwingine kwa yule mgonjwa aliyekuwa amelazwa muda wa miaka thelathini na minane( Yoh.5:5-9,14).  Mtu huyu alikuwa na dhambi zilizomtesa muda mrefu kitandani,lakini Yesu Kristo alipokutana naye alimsamehe dhambi. Biblia haituambii kwamba mtu huyo aliomba toba kwa Bwana,bali tunaambiwa Bwana alimuhurumia akamwambia “ simama,jitwike godoro lako,uende” naye akaenda. Kilichomfanya apokee uzima ni baada ya kusamehewa dhambi zake (Yoh.5:14)Ni muhimu kuitumia mamlaka hii juu ya dhambi zote.

Kwa msaada zaidi,na maombezi nipigie kwa simu+255 683 877 900/

Namba ya what’s app ni+255 746 446 446 .

Mchungaji Gasper Madumla.

UBARIKIWE

Комментарии


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page