top of page

MAMLAKA YA MWAMINI~ 02

Na Mch.Gasper Madumla.


02. AINA ZA MAMLAKA.

Kwa ufupi,

Zipo aina mbali mbali za mamlaka kama vile mamlaka mbali mbali za kawaida na mamlaka mbali mbali za kiroho. Tunazozingazia hapa ni baadhi tu mamlaka za kiroho,katika mazingira ya kawaida kabisa;

  1.  Mamlaka ya kiofisi / kazini ( Mathayo 8:9)

  2. Mamlaka ya mbinguni na duniani / Mamlaka ya Yesu – ( Mathayo 28:18 )

  3. Mamlaka ya juu ya pepo wote na kuponya maradhi/magonjwa ( Luka 9:1)

  4. Mamlaka juu ya miji ( Luka 19:17)

  5. Mamlaka ya kifamilia / ukoo

01. Mamlaka ya kiofisi/katika eneo lako la kazi.

Ikumbukwe ya kwamba; katika kila eneo kuna mamlaka kuu ifanyao kazi. Hata eneo la ofisi yako ipo mamlaka ya kiroho inayotawala hapo,na wapo wenye hiyo mamlaka rohoni. Inawezekana wewe ukawa huwajui but wapo tu. Inategemea kazi / ofisihiyo imekabidhiwa / ipo nyuma ya msingi wa nguvu gani. Mamlaka za giza zinaweza kutawala ofisi yako,lakini utambue kwamba sivyo Mungu atakavyo,kwa maana ni mpango wa Mungu wewe mwenyewe ndio utawale hapo kwa kuwa unayo mamlaka ya Kristo ndani yako ya kutawala hiyo ofisi / kazi.

Katika Mathayo 8:9 Neno linasema; ” Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.” Swali la kujiuuliza huyu akida/kiongozi amewekwa na nani? atawale nini? Pamoja na hayo, tunaweza kujifunza kitu kwa huyu akida kwamba alikuwa na mamlaka juu ya kazi yake,kiasi kwamba akiamuru mambo yanakuwa bila mjadala wowote ule.

Kumbuka; ni lazima “uwekwe” na mwenye mamlaka,kwa maana hakuna mamlaka ya kujipa mwenyewe. Lakini pia lazima wengine wawe chini yako wewe mwenye mamlaka. Ndivyo ilivyo hata kwa sasa,ndani ya Kristo,sisi tumewekwa na kwa sababu hiyo ofisi / kazi ipo chini yetu,tunapaswa kuamuru katika ulimwengu wa roho na mambo yawe. Kwa hiyo,mamlaka ya kiofisi / kazini ina mambo matatu “ Kuwekwa na mwenye mamlaka kuu zaidi yako,nguvu ya sauti/kutiisha,watu / vitu vitakavyofuata sauti yako ” Kikikosekana hata kimoja katika hivi,basi ujue bado huna mamlaka kamili. Kama mwana wa Mungu,ofisi / kazi hiyo uifanyayo umepewa na Bwana ili wewe uwe mtawala kiroho hata kimwili pia. Mamlaka yako huanzia rohoni katika kazi yako. Hivyo lazima uwe umejiungamanisha na Kristo mkuu wa mamlaka zote.

02. Mamlaka mbinguni na duniani / Mamlaka ya Yesu ( Mathayo 28:18)

Yesu ndiye mkuu wa wakuu,mwenye kuweka mamlaka kwetu. Huyu alikuwa kiboko yao!!!! Mamlaka yake ilikuwa mbinuni na duniani kuonesh hakuna mamlaka nyingine iliyokuwa juu yake. Biblia inaeleza kuwa “uweza wa kifalme ulikuwa begani mwake” Hakika huyu alikuwa ni Mungu. Kumbuka pia ;Mamlaka ya Yesu ndiyo ipo ndani yako pia,kwa kuwa tunatawala pamoja naye. Ni vyema kutambua ya kwamba Yesu ana nguvu hapa duniani hata Mbinguni.

Kwa msaada zaidi pamoja na maombi piga kwa ;+255 683 877 900

Wht’sapp +255 746 446 446

ITAENDELEA

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page