top of page

MAMBO MATATU MUHIMU KANISANI.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Kanisa linamsingi na taratibu zake katika nyanja mbali mbali. Tunapoliangalia kanisa lililokuwa na lazima tutagundua sababu zilizolifanya kanisa kukua kwa maana ukuaji wa kanisa hauji kwa bahati,dharula.Bali ni kanisa linahitaji mchakato wa kupitia katika ukuaji. Ninaangazia mambo matatu tu,yale mambo muhimu kati ya mambo mengi ya muhimu katika ukuaji wa kanisa.,nayo ni kama ifuatayo;

01. Roho mtakatifu ;

Kanisa la Kristo haliwezi kutenganishwa na Roho mtakatifu. Hivyo kanisa ni lazima lijifunze mengi na kumfahamu kiundani Roho mtakatifu. Kanisa lisipofundishwa habari za Roho mtakatifu kiundani,litakuwa hatarini kupotea na kuanguka kwa maana waamini hawataweza kumtegemea Roho mtakatifu. Bila Roho mtakatifu kanisa haliwezi kusonga mbele katika eneo lolote lile. Hivyo,Kujifunza habari za Roho zinalipelekea kanisa kumfahamu Roho na hatimaye kitakachofuata ni kutegemea Yeye katika maongozi yote,hili ndilo jambo la kwanza na muhimu sana kwa kanisa la Kristo.

02. Kukaa katika Neno (Yoh.8:31-32)

Neno “kukaa” lina maana ya“ kutulia au kubakia”. Mwenye kukaa ni yule hana papala bali kuwa na utulivu na kubakia mahali pamoja. Kanisa la Kristo lililo hai,lazima likae kwenye neno la Mungu ipasavyo. Katika neno ndipo kuna ushindi wa kila kitu. Hata shetani hushindwa katika neno;hivyo ni muhimu sana! Hila za shetani ni kulitoa kanisa katika maarifa ya Mungu (Neno),akifanikiwa hapo tu,basi ujue kanisa litapigwa na kupigika kweli kweli.” Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.’‘ Wakolosai 3:16

03. Maombi.

Moja kati ya msingi wa kanisa la Bwana ni Maombi (Luka 19:45-46),Kama vile Kristo Yesu alivyokuwa mwombaji ndivyo lilivyo kanisa lake. Bila maombi,kanisa haliwezi kusonga mbele kwa sababu mambo hayaendi kwa wingi wa vikao,hoja na umakini bali kwa maombi. Na ndio maana kanisa hata kama halina vikao vingi vya kujadili maendeleo lakini likawekeza muda wake katika maombi na kuwa na vikao vichache,basi ujue kanisa litashinda!. shetani analijua hili,na ndio maana kuna baadhi ya makanisa ya kiroho yametiwa uvivu,na kujikuta hawana maombi kabisa bali kuweka vipaumbele vitu vingine,na kwa sababu hiyo,kanisa linakuwa halina nguvu ile aliyoitamka Yesu,kwamba kanisa litaishindamilango ya kuzimu (Mathayo 16:18)

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Kwa huduma ya MAOMBI  piga kwa namba hizi hizi; +255 683 877 900

What’s app  namba +255 746 446 446

Na  Mch. G.Madumla 

UBARIKIWE. 

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page