top of page

MALANGO YA MJI -02 (tamati)


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

Kumbuka si kila mambo mabaya yanayokutokea mara kwa mara kwenye maisha yako yamesababishwa na uovu,dhambi au mambo ya kuridhi. Lakini mengi ya mambo ambayo watu hupitia leo ni kwa sababu ya matokeo mabaya ya hapo awali. Ukweli ni kwamba mtu akiwa ndani ya Kristo ni kiumbe kipya (2 Wakorintho 5:17),Lakini mambo ya kurithi ni lazima yasafishwe kwa damu ya Yesu. Kama jinsi ilivyokuwa kazi ya lango kupitisha na kutoa kitu. Katika kupitisha,kunaweza kukapita kitu kibaya kwenye ukoo wako na wengine mkaangaika kwa kitu hicho,mfano zipo familia zinazotembea kwenye laana. Laana imesimama kwenye lango la mji/ukoo hata kupelekea laana hiyo kurudisha nyuma maendeleo yoyote ile.

Ebu fikiri ikiwa laana imesimama kwenye lango la mji,hapo utagundua hakuna kitakachoinuka chochote kile iwe na kufanikiwa au iwe ni maisha,kwa ujumla hakutakuwa na cha maana kwenye familia ya namna hiyo. Wakati mwingine lango huzuia kitu. Katika lango la kiroho la mji wako,linaweza kuzuia jambo la kiungu ingawa litafanikiwa lakini kwa shida sana. Hujawahi kuona mtu anatakiwa awe mtumishi wa Bwana lakini anaweza kuzuiliwa asiende mbele kwenye kusudi lake ingawa anaweza kufanikiwa hapo baadaye kwa maana hakuna awezaye kuzuia kusudi la Mungu (Ayubu 42:2).

Nilishawahi kumsikia binti mmoja ambaye alikuwa mbioni kuachwa na kijana aliyekuwa amempatia mimba na walikuwa hawajafunga ndoa bado. Walitofautiana huku mwishoni kwa maana kijana hakutaka hiyo mimba na alimwambia binti aitoe,lakini pia kijana alikuwa akiwa na mahusiano ya mabinti wengine. Binti anasema kwao,mama zake wakubwa na wadogo walizalia nyumbani. Hapakuwepo na mwanamke aliyeolewa bali walikuwa wakizaa na kuleta watoto kwa bibi walelewe.

Sasa na yeye yupo na mimba na mahusiano yake na huyo kijana yalikuwa yanakatika,alikuwa anakaribia kuachwa kabla ya kuolewa. Yaani kile kile kilichokuwa kinaendelea kwa mama zake ndicho kinakuja kumpata na yeye. Hivi unaona hapo? Hivyo bila shaka kulikuwa na tatizo kwenye mji wake,kulikuwa na shida hasa kwenye lango,ndio maana kitu kile kile kinatambaa kwa wengine. Bila shaka hata wewe inawezekana kuna kitu kinachofanana na hiki,labda sio ishu ya kuoa na kuolewa lakini ikawa ishu ya kuzaa,magonjwa,faraka n.k

  1. Lakini sasa ikiwa ndivyo,nini kifanyike kuwa mbali na majanga haya ?

Kukombolewa – Ni muhimu sana kuombewa na mchungaji kwa kumshirikisha yote unayopitia kwenye mji wenu ili akueleze kiundani. Kukombolewa kuna maana ya kufunguliwa kwenye hivyo vifungo kwa njia ya maombi  na neno la Bwana. Hii ndio dawa kubwa la kuepukana na majanga haya. Katika eneo hili kuna matumizi ya damu ya Yesu,kuna kuokoka kwanza.

Ikiwa kama umebarikiwa nifahamishe, pia Kwa maombi na msaada zaidi , piga +255 683 877 900.

What’sapp namba +255 746 446 446

Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page