top of page

MALANGO YA MJI- 01


Darwaja_(The_Gate)

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

“malango” ni sehemu ya maingilio ya kutoka au kuingia. Moja kati ya sehemu muhimu kwenye jengo ni malangoni kwa maana hapo ndipo watu na vitu huingia na kutoka. Malango yakifungwa basi hapo hakuna kitu kitakachoweza kupita !!! Kuna malango mbali mbali kama vile,wazaliwa wa kwanza huitwa ni malango,malango ya kanisa,na kuna malango ya miji. Malango tuliyoyazoea ni malango ya wazaliwa wa kwanza,lakini leo tunajifunza kitu tofauti kidigo.

Tunapozungumzia leo malango ya mji inawezekana ikawa ni ngumu kidogo kuelewa kwa sababu sisi tu uzao wa kipindi hiki,lakini watu wa kale wa kipindi cha akina Samsoni,Joshua n.k wanaelewa nini hasa malango ya mji kwa sababu katika kila mji ulikuwa na malango yake ya kuingia mjini na kutoka mjini. Hivyo kulikuwa na lango la kuingia na la kutokea.“ Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye.” Luka 7:12 (soma pia 1 Wafalme 17:10,Mwanzo 19:1 n.k)

Maandiko haya yanataja milango ya miji kuonesha kwamba miji ilikuwa na milango. Milango hii haikuwa milango ya kiroho bali milango kama milango. Kwa lugha nyepesi milango ya miji hiyo ilikuwa kama sehemu ya kutofautisha mji na mji kama vile mipaka lakini katika mipaka hiyo kulikuwa na sehemu unayoweze kuingi au kutoka. Yerusalemu kama mji nao una lango lake (Marko11:4).Biblia inatuambia Yesu alipokwenda kwenye mji wa Naini,hapo kwenye mji alipokaribia kwenye “lango la mji” ndipo palikuwa na watu wamebebamaiti… nataka nikuoneshe tu kwamba “ kulikuwa na lango la mji”. Ukitafakari kuhusu malango,utagundua kwamba kila jambo limebeba lango hata kaburi lina lango lake ( Marko 16:3)

Hivyo nataka ufikirie “malango kiroho” hasa katika eneo la mji. Nisemapo malango ya mji,nina maana ya sehemu ya kiroho katika mji (nyumbani kwenu) inayofanya kazi ile ile ya kuzuia au kupitisha kitu. Ikiwa utaenda nyumbani kwenu,utapokelewa na ndugu zako waliopo hapo nyumbani kwa sababu umeingia tayari kwenye mlango wa mji wenu. Kikawaida huwezi kuiona milango ya mji wenu,lakini utaona matokeo ya kile kitakachoweza kupita au kuzuiliwa. Ebu fikiria ikiwa kama kwenu kutakuwa na shida hiyo hiyo kizazi hadi kizazi,hii itakuwa na maana kwamba kutakuwa na shida kwenye mlango wa mji wako. Ngoja nikuoneshe hili,“Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. ” Mwanzo 4:7

Katika andiko hilo,unajifunza nini? Je unafikiria ni mlango gani unaotajwa hapo? ni mlango wa kawaida au wa kiroho? Ukitafakari katika mstari huu,utagundua ni mlango wa kiroho ndio unaozungumziwa hapo,dhambi ilikuwa imesimama kwenye mlango wa Kaini. Na kwa sababu haikushughulikwa,tunaona matokeo ya dhambi hiyo katika kizazi cha tano kiitwacho Lameki aliyeuwa mtu kama babu yao Kaini alivyomuua Habili (Mwanzo 4:23). Uovu ulisimama langoni,na kwa uovu huo ukawala kizazi hata kizazi. Huu ni moja ya mfano ulio hai katika maisha yako,ebu cheki ni nini kilichosimama kwenye lango la mji wako? kinaleta matokeo gani kwako mtu ambaye ni kizazi kingine kabisa!

Alaa kumbe!!! Nimegundua kwamba suala la malango ya mji ni suala muhimu sana kushughulikiwa. Na ndio maana watu wajanja hushughulika na mambo ya malango mapema pale tu wanapokuja kwa Kristo. Wewe pia yakupasa sasa uanze rasmi kushughulikia mambo haya,kwa maana kama utapuuzia ujue yatatesa na kizazi chako pia.

ITAENDELEA…

Ikiwa kama umebarikiwe, nifahamishe. Kwa huduma ya MAOMBI piga kwa namba hizi hizi; +255 683 877 900.

What’s namba +255 746 446 446

Na Mch. G.Madumla

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page