top of page

MACHO YA KIROHO.

Updated: Sep 2, 2022


Laiti kama ungelifunuliwa leo, japo kwa dakika moja tu,ili uone mambo yanayoendelea sasa katika ulimwengu wa roho,ungelishangaa sana tena ugelipigwa na butwaa!!! Kuna mambo mengi usiyoyajua,tena makubwa na ndio maana Neno linakutaka uomwombe Bwana akuoneshe mambo makubwa na magumu usiyoyajua ( Yeremia 33:3). Uwezo wa kuona kiroho ni kazi ya macho ya rohoni.


Kazi hii ni mojawapo ya kazi ya Roho mtakatifu kwa maana awezeshaye mtu kuona kiroho ni Yeye Roho wa Bwana. Katika hali ya kawaida kuna mambo ambayo huwezi kuyaona kwa sababu macho yako ya damu na nyama yanakikomo chake cha kuona.

Hivyo utagundua kwamba kuna mengi katika roho usiyoyajua wewe,nawe ni mtumishi wa Mungu.Kama mtu wa Mungu, macho yako ya kiroho yanapaswa kuona. Kwa maana Roho mtakatifu yupo ndani yako Yeye achunguzaye mambo yote hata mafumbo ya Mungu ( 1 Wakorintho 2:10).


Hivyo utagundua kwamba kazi ya kuona kiroho si kazi ya nabii bali ni kazi ya Roho mtakatifu, ikiwa nabii amepewa kuona,wewe pia unapaswa kuona ingiwa mnaweza mkaona tofauti. Kumbuka;

Macho ya rohoni ni uwezo wa kiroho wa kuona mambo katika ulimwengu wa roho. Lakini hata hivyo,yapo masikio ya kiroho ambapo ni uwezo wa kiroho wa kusikia. Kwenye biblia wapo watu ambao tunawezakujifunza kwao katika hili. Watu kama akina Eliya, Elisha,Paulo,wana wa manabii, Daniel,Ezekieli,Isaya,Yeremia na wengine wengi,pamoja na Yesu mwenyewe.


Katika kipindi cha Elisha,kulikuwa na mfalme wa Shamu alipanga vita dhidi ya Waisraeli mara nyingi lakini hata hivyo hakufanikiwa kuwapata kwa maana kila alipokuwa akipanga,Waisraeli walijua mara moja na kuwawahi maadui zake. Siku moja mfalme wa Shamu alighadhibika na kuwauliza watumishi wake,“ Ni mtu yupi miongoni mwetu aliye upande wa mfalme wa Israeli ? ”


( kwa maana alifikiri labda kuna mtumishi wake mmoja atakayekuwa akivujisha taarifa zake). Wakamwambia sivyo mfalme, bali kuna mtu anaitwa Elisha,yeye ni nabii wa Israeli anayejua hata mambo yako unayoyapanga kwenye chumba chako cha kulalia.

Baada ya hayo,Mfalme wa Shamu akakusanya kikosi amtelemkie Elisha, na mtumishi wa Elisha alipoyaona majeshi ya Shamu, ndipo alipoogopa. lakini Elisha akamjibu;“


Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. BWANA akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote.“ 2 Wafalme 6:16-17


Tatizo la mtumishi wake Elisha lilikuwa katika uwezo wa kuona kiroho bali aliweza tu kuona kimwili. Na kwa sababu ya tatizo hili,aliogopa sana kuyaona majeshi ya washami,hakujua majeshi ya Bwana yaliyo pamoja nao. Tunajifunza jambo,kwamba ikiwa huwezi kuona kiroho ni rahisi kumwogopa adui yako,kwa maana macho ya damu na nyama huleta hofu/ hudanganya.


Lakini ikiwa utafanikiwa kumwona adui yako kiroho, na jinsi nguvu ya Mungu iliyopo upande wako,basi ujue huwezi kumkimbia adui yako au kumwogopa. Unafikiri kwa nini Elisha hakuweza kuteteleka/hakuogopa? Kwa sababu alikuwa akiona kiroho na kuyaona majeshi ya Shamu ni madogo sana yenye kiwango cha chini ukilinganisha na majeshi ya Bwana.Bila shaka, Elisha alipewa uwezo wa kuona kiroho na kusikia kiroho. Alipowatazama hakuona chochote cha kumtisha.


Nguvu ile ile aliyokuwa nayo Elisha ndani yake ndio ipo kwako ndani yako, ni kuamini tu na kusonga mbele. Ukisoma kwa ukaribu andiko hilo hapo juu,utagundua kwamba,


  1. Hutakiwi kuogopa adui zako!

  2. Wapo maadui zako wanaokuzunguka kwa hila.

  3. Ipo nguvu ya Mungu kubwa zaidi ya nguvu ya adui,iliyokuzunguka pia.

  4. Unaweza ukawa mtumishi uliyekosa macho ya rohoni kama mtumishi wake Elisha.

  5. Unaweza pia kuona kiroho kama Elisha alivyponaà

  6. Macho ya rohoni yanaweza kufumbuliwa,na hatimaye ukaona kiroho.


Elisha alipomwomba Mungu kwa habari ya kufunguliwa macho ya mtumishi wake, hakika Bwana alitenda kwa kumfungua macho ya rohoni naye akaona. Na ndivyo ilivyo hata wakati huu,ukiwa huwezi kuona kiroho, mtu wa Mungu mwenye mafuta/upako wa macho ya rohoni!. Jambo la msingi kujua ndilo hili“ Macho na masikio ya rohoni ni kazi ya Roho mtakatifu,kisha unaweza ukaombewa na hatimaye ukapata uwezo huu.


Kumbuka;


Ikiwa Mungu amekuonesha kitu,basi ujue kuna maana ya kitu hicho. Vivyo hivyo atakupa na namna ya kushughulikia kile ulichokiona,kwa maana hakuna haja ya kuona kitu kisha ukawa hujui namna ya kushughulikia.


Hakuna jambo la muhimu kwenye maisha yako kama kuwa na macho ya rohoni na sikio la kiroho


Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp +255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.


UBARIKIWE.

댓글


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page