top of page

LISHA NDUGU ZAKO.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Watu wengi hawana tabia ya kuwatunza,kulisha,kuwajali watu wa nyumbani mwao wenyewe. Mara nyingi tumeshuhudia watu wakiwalisha marafiki zaidi ya ndugu zao.

Mapenzi ya Mungu wewe ujue namba nzuri ya kuwalisha ndugu zako zaidi watu wa nje. Maana mtu yeyote anayewalisha,anayewatunza watu wa nyumbani ni Bora zaidi,Tena afaa katika utumishi uliotukuka. Kiroho hali ipo hivyo hivyo, ndugu zako ni wale waliookoka,( mlio ktk Imani moja).

Kuwalisha ndugu zako ni zaidi ya kuwapa ugali, chakula- hasa hasa unachohitaji kuwapa ndugu zako ni Neno kuhakikisha nao pia wanapata neema ya kuokoka na kumjua Mungu wa kweli.

“Naye Yusufu akawalisha babaye na nduguze na nyumba yote ya babaye, kwa kadiri ya hesabu ya watoto wao.“ Mwanzo 47:12

Unakumbuka habari ya Yusufu aliyekuwa waziri mkuu huko Misri baada ya mapito mengi. Sasa ndugu zake Yusufu wamemfikilia kutoka mbali kwenye nchi ya Kanaani,naye Yusufu hakuwalipa mabaya nduguze ( kama waliomfanyia) bali aliwalipa mema ( Warumi 12:21). Ndipo tunaposoma hilo andiko la juu ya kwamba akawalisha ndugu zake. Tendo la Yusufu la kuwaketisha nduguze na “kuwalisha” ni tendo linaloeleza “pendo” alilonalo Yusufu.

Kumbuka ; Chakula alichotoa Yusufu kwa nduguze kilikuwa ni chakula cha kawaida kabisa kama tunachokula siku zote,hakikuwa chakula cha kiroho. Yaani Yusufu alitoa chakula cha kawaida,nami Leo nataka kuzungumzia “kulisha ndugu zako kwa chakula cha kawaida kabisa ” kama fundisho la leo kwako.

Bila shaka unao ndugu wa damu yaani ndugu wa kuzaliwa. Tena bila shaka ndugu zako ni maskini,hawana kitu. Wengine wapo mbali na wewe,labda wapo kijijini kwenu au nyumbani kwenu. Bila shaka unao ndugu ambao wanakuangalia wewe,wanakutegemea wewe. Ndio,unao bhana ndugu wa namna hiyo. Swali ,Je unawalisha ? Nakuuliza tena,Je unawalisha ndugu zako? Au umewasukumia mbali ? Jifunze leo.

Mtu mmoja ninamjua,sasa yapata miaka 30+ (30 na),tangu aende ulaya,hajarudi na wala hajui wazazi wake wanakula nini ! Wanavaa nini! Hajui wadogo zake wanaishije ishije!! Kwanza wazazi wake wenyewe ni wazee sana,na wametelekezwa. Yaani mpaka mzazi wake mmoja alikuja kufariki,lakiji jamaa hakurudi sana sana kawatumia vijisenti vya kununua jeneza na kupika wali katika msiba,hakurudi dah!!!! Inauma kuwa na mitoto namna hii isiyojua namna ya kuwatunza watu wa nyumbani kwao

Wewe Je? Ni lini mara ya mwisho kutuma ela ya matumizi kwa baba na mama yako? Ni lini mara ya mwisho kutuma ela ya kula nyumbani kwa wadogo zako? Mbona ndugu zako wanahaha kana kwamba hawana ndugu aliyefanikiwa??? Wewe unanielewa lakini? Jifunze kwa Yusufu,aliwalisha watu wa nyumbani kwake.Hivi kweli unashindwa kukumbuka ni wapi ulipotoka? Anyway….

Ebu tujifunze neno hili “ kwa kadiri ya ndugu zako,jitoe kwao” Mungu amekuokoa wewe kisha amekupandisha kwa makusudi ya kuwasaidia ndugu zako. Ndugu zako sio wanawake / wanaume unaotumia nao,kwa maana hao ni wapitaji tu,na siku ukichalala ( ukifulia),hutawaona hao. Yusufu mtu aliyeinuliwa na Bwana,tena na kutendewa mabaya sana lakini bado aliwapa kipaumbele ndugu zake katikati ya wageni.

Hata kwako,inawezekana ndugu zako wamekutenda vibaya,tena vibaya. Lakini Bwana amekupigania katika mabaya yao,na hapo moyo wako usije ukainuka dhidi yao kwa kulipa kisasi. Bali jifunze huo ndio muda mzuri wa kuwatendea mema,na moja ya jema ni kuwatunza. Wakati mwingine ukifikiri walivyojitahidi wakuangushe,unaumia. Lakini kumbuka,usilipe baya. Wewe watunze ndugu zako mpendwa kwa kuwalipa mema.

Mimi huwa ninashangaa kuwaona watu ambao Mungu amewainua lakini wao bado hungangania kulipa mabaya kwa ndugu zako! Wewe umeinuliwa,inua na wekine basi. Kwani kuna shida gani kuwatengea bajeti familia yako? Inawezekana wewe ni Yusufu kwa ndugu zako,hivyo jifunze neno hili mahali hapa.

Ukirudi nyumbani,kumbuka;

Jitahidi kuwa mtu wa kawaida fulani hivi. Unapokuwa nyumbani kwa ndugu zako,usiwadharau wala kuwaona hawana elimu. Wala usiongee “kizungu chako” kwa sababu tu ulisafiri na kukaa nje kidogo. Jiweke sawa kwa kila ndugu yako mmoja mmoja. Sasa,unaporudi nyumbani rudi kuwalisha,kuwatunza hao ndugu zako,ukumbuke Yeye Mungu aliyekuinua ndio huyo huyo anaweza akakushusha endapo kama utakataa kunyenyekea.

Hivi unajua kuna watu ambao hawataki kabisa kuonekana kama wao ni watanzania,au ni wa jamii fulani hivyo wakirejea makwao hujifanya kama ni wageni fulani na hubadili lugha,mtindo wa maisha,namna ya kutembea n.k. Wamesahau kwamba wao ni watoto waliokuwa wa kimaskini kwa sababu hata bado ndugu zao ni maskini. Sasa kuna haja gani ya kuishi maisha ya kuigiza? Ni vyema ujifunze kuwalisha ndugu zako kwa kula nao pamoja kile watakachokula tena kwa moyo mmoja.

Jifunze kwa Yusufu bhana,uone namna ya alivyowatanguliza ndugu zake. Leo ndugu zako umewaacha mbali,wala huwasaidii!!! Mbaya! Walishe bhana,hao ni ndugu zako tu. Hata kama hawajasoma kama wewe,lakini bado ni ndugu zako, hata kama hawajaokoka kama wewe bado ni ndugu zako,hata kama ni maskini bado ni ndugu zako tu. Chukua hatua sasa!

Ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezi pia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 683 877 900 

WhatsApp ni .+255 746 446 446

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page