top of page

KWELI 6 ZA INJILI

Updated: Sep 2, 2022



“Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mungu inadhihirishwa ndani yake, toka imani hata imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa imani.” Warumi 1:16-17


01.“siionei haya injili” – Kuna mambo chini ya jua ya kuyaonea haya,lakini sio injili. Unaweza ukaona aibu/haya juu ya mambo mengine lakini unapofika katika injili,aibu inakaa pembeni. Mfano,ukikaa na mtu asiyemjua Mungu wa kweli,huna sababu ya kukaa kimya kwa sababu unaona haya atakuonaje ukimwongelesha kuhusu habari njema,hapo ndipo hutakiwi kuona aibu,bali sema naye. Unapoongea na mtu awaye yote,tafuta nafasi ya kushiriki /ku-share injili kwa kile unachokifahamu,bila kuogopa kwa maana ukimwomba Mungu kabla ya neno atakuwezesha.

02.” Injili ni nguvu ya Mungu” ( It is the power of God) – Injili ni habari njema ambayo ni nguvu ya Mungu. Hakuna haja ya kutafuta nguvu ya ziada yoyote,bali nguvu ipo kwenye injili. Kama injili halisi ipo,basi hapo nguvu halisi ya Mungu ipo pia. Nguvu hii ni ajabu kwa maana si nguvu ya mnenaji wala yeyote bali ni ya Mungu. Ni vyema kujua kwamba injili ni nguvu ya Mungu,Neno lake lina nguvu ya kuokoa,kuangusha,kusawazisha n.k .Ikiwa mtu anatafuta nguvu ya Mungu,basi aitafute injili.


03. ” Injili inaleta wokovu kwa watu wote ” (that brings salvation to every one who believes) – Mtu mmoja akauliza “ Injili ni kwa waliopotea tu?” Jibu lake “hapana,injili ni kwa watu wote,” Watu wengi hudhania kwamba injili ni kwa wale walio nje ya Kristo,lakini ukweli ni kwamba wakristo nao wanahitaji kuisikia sana injili ili watengeneze uhusiano wao na Mungu. Ni vyema watu wakajua,Hakuna wokovu nje ya injili. Injili inaachilia wokovu kwa watu wote kwa maana injili ni habari njema.

04.” Kwa aaminiye,kwa Myahudi kwanza,kisha Myunani ” – Ukuta uliopo kati ya Myahudi na Mmataifa/Myunani unavunjwa na imani. Imani imesimama kwenye nafasi kama daraja la kutuunganisha wawili waliokuwa mbali kuwa kitu kimoja. Pale Myahudi kwa asili anapomwamini Kristo,ni sawa na Mmataifa atakaye mwamini Kristo. INjili haiangalii utaifa wa mtu,bali imani ndio kitu cha msingi. Wokovu wala hauitaji matendo mazuri,bali imani tu kwa Kristo kwa Myunani na Myahudi pia.


05.”Haki ya Mungu inadhihirishwa” – Mungu anajifunua ndani ya injili,haki yake inafunuliwa ndani ya injili. Hii ni sawa na kusema haki ya Mungu tunaifahamu kwa njia ya injili.Haki hii ni kwa njia ya imani toka mwanzo hata mwisho/toka imani hata imani. Unawezaje kujua haki ya Mungu kama hujaiangalia injili ? Unawezaje kuona wema wa Mungu nje ya injili? Bali kupitia injili ndipo tunaweza kuona haki ya Mungu.


06. ” Mwenye haki ataishi kwa imani ”- Hili ni somo jingine,Lakini ndivyo ilivyoandikwa. Kwamba mwamini hawezi kumpendeza Mungu kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa imani tu (Waebrania 11:6).Katika maisha ya kawaida lazima ujifunze kuishi kwa imani,kuishi kwa imani ni kuishi ndani ya injili ya Bwana,jinsi Neno lisemavyo ndivyo uishivyo.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI

piga kwa+255 683 877 900

Whatsapp .+255 746 446 446


Na Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page