KUWA MAKINI KUFANYA MAAMUZI YAKO WAKATI WA NJAA!
- Mch. Gasper Madumla
- Jun 13, 2018
- 3 min read
Updated: Sep 2, 2022

Jamaa anaweza akavunja sahani, maana ana njaa alafu karudi home msosi hakuna, wamemtangulia! Hahahaha,
Waswahili wanasema “adui yako mwombee njaa! ” yaani adui yako usimpige bali apigwe na njaa tu yatosha. Njaa ni zaidi ya bakola za mwalimu wa hesabati, tena mwalimu wa hesabati wa darasa la sita B, maana mimi ndio nawajuaga walimu wa hesabati bhana! (Maana bakola ndio zao, utafikiri hawana watoto, hahahaha). Jamani njaa ni mbaya kuliko maelezo! Usiombee ukamatwe na njaa!
Nimegundua kwamba watu wengi walikosea kufanya maamuzi kwa sababu ya kupelekeshwa ni kitu kinachoitwa “njaa”. Badala ya kufanya maamuzi sahihi, watu wengi hujikuta wakifanya mambo ambayo baadae ukiyaangalia, wakati mwingine unaishia kucheka na kuwaonea huruma. Njaa ikizidi inaweza ikakutoa kwenye lengo sahihi na kujikuta upo pabaya ikiwa utashindwa kuhimili,.
Kwani wewe hujaona mtumishi wa Bwana aliyeshindwa kustahimili njaa, akilazimisha pesa kwenye mahubiri kwa sababu tu ya njaa ( acha wale manabii wa uongo ambao wenye lengo la kutafuta pesa). Au wewe hujaona mtu hajatulia kwa Bwana kwa sababu ya njaa?
Njaa ndio ilimponza Esau hata kujikuta akifanya maamuzi mabaya ya kuuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza. Na ndio maana leo nakutahadharisha kwamba “uwe makini na maamuzi yako wakati wa kipindi cha njaa” kwa sababu ukifanya mchezo kidogo tu, unaweza ukapiga “mweleka mpaka chini” ; njaa haina adabu, inaweza ikakumwaga vibaya! Soma Mwanzo 25:29-34.
Maamuzi aliyoyafanya Esau yalisukumwa na njaa ya kitambo tu. Njaa ilipomshika hakuona thamani ya haki yake, akajikuta akiendeshwa na tamaa ya kitambo tu. Hivi unajua ukiiendekeza njaa, ni lazima uwe mtumwa wa watu. Ebu chukulia wewe ni mtumishi labda ni mwimbaji, au mhubiri aliyeendekeza njaa. Sasa, kama ukiwa katika hali kama hii, utajikuta ukidai malipo kabla ya huduma. Ndio kama vile nakuona ukienda kufanya huduma sehemu fulani, alafu unamwambia mwenyeji wako “sasa,.. Ebu nifanyie maarifa kidogo, niwaachie watoto ela ya kula dagaa kwanza alafu ndio nije mara moja huko… ” Sasa angalia njaa na maamuzi yako yatakavyokuwa.
Yule mwenyeji kweli atakutumia pesa kabla ya kufika kwake. Lakini uwe na uhakika ni lazima atakupangia masharti ya kuhudumu, yaani lazima uhudumu kama atakavyo huyo aliyekupa pesa kwa maamuzi yako ya kinjaa – njaa. Sasa utajikuta umewekewa mipaka ya kihuduma, kwa sababu si umekula ela ya watu kwa njaa yako tu! Ni hatari sana hii, kwani wewe hujawahi kuona haya? Mimi nimeona
Siku moja tulipokuwa mkoa fulani tukichapa injili huko. Sasa, mtu mmojaesha mwenyeji akaomba twende kwake tukale baada ya mkutano. Wenzangu wakaenda kwa huyo ndugu, na huyo ndugu alihakikisha anawachanganya kwa msosi. Akawaandalia bonge la supu la kuku wa kienyeji kama kifungua kinywa kwanza; sisi tunaita “kusukutua”.
Kisha akawamaliza na chakula. Sasa kula sio dhambi, wala sio vibaya bali kibaya ni kuonesha njaa kwa wageni. Sasa mgeni akikulisha vizuri, kama hautakuwa makini unaweza ukajikuta unatoka kwenye lengo husika. Unajua tunashauri ukiwa ugenini na njaa yako uwe makini sana na maamuzi yako. Mimi nakuambia kuna watu wamejikuta wakijifunga kwa maneno yao wenyewe kwa sababu njaa imewapiga. Ngoja nikuulize; Hivi umeshawahi kuwa na njaa iwe ni njaa ya chakula kwa siku au njaa ya kukaukiwa nyumbani kwamba wote hamjui siku itaishije?
Alafu ebu cheki, maamuzi yako! Hapo ndipo uwe makini sana. Lakini ifike wakati wa kuficha njaa yako bhana, sio kila mtu ajue kwamba una njaa kipindi hiki, Bwana akijua Yeye yatosha! Maana kuna watu wakiwa na njaa basi mtaa mzima utajua! Bali wewe ukiwa na njaa, paka midomo yako mafuta, jitahidi japo kuoga basi eeh, kisha sugua goti kwa Bwana huku ukichunga kinywa chako, hivyo ndio sawa. Ukiona unahitaji msaada zaidi wa kimaombi, au umeguswa na ujumbe wa leo basi usisite kuwasiliana nami kwa namba hizi;
kwa
+255 683 877 900
Namba ya What’sapp ni .+255 746 446 446
Mch. Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comentarios