top of page

KUTEMBEA NA MUNGU KATIKA UTII~mwisho

Na Mch. Gasper Madumla.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi…

03. Kukamatwa na roho ya mazoea.

Mungu anasema nasi kwa njia mbalimbali.mojawapo ya njia ambayo Mungu huitumia kusema nasi ni njia ya watumishi wake wanaotuchunga na kutuongoza kiroho. Sauti za wachungaji wa Mungu ni sauti ya Mungu. Lakini leo kunashida ambayo inasumbua wengi hata wameshindwa kuvuka. Wengi wameshindwa kutembea na Mungu ipasavyo kwa sababu ya shida hii. Nayo “ kuwa na roho ya mazoea”

roho ya mazoea inaweza ikawa katika neno au katika kuwazoelea watumishi wa Mungu. Ebu jikague wewe katika eneo hili. Je una roho ya namna hii ya kulizoelea neno la Mungu? Au Je una roho ya kumzoelea mtumishi wa Mungu? Inawezekana kabisa ukawa umeshikiliwa na roho ya namna hii. Ukiwa na roho ya mazoea,basi kamwe huwezi kutembea na Mungu ipasavyo katika utii wa sauti ya Mungu.

roho ya mazoea imekuwa kikwazo kwako na kwa wengi kiasi cha kuwa kinyume na sauti ya Mungu. Maana ikiwa utamzoelea mtumishi wa Mungu,hata akisema nawe ujumbe wa Mungu, wewe utaona ni kawaida sana na kupuuza.hivi unajua hata watu wa karibu na Yesu hawakupokea miujiza mingi kwa sababu walimzoelea mno na kumuona mtu wa kawaida sana,na hawakujua Yesu amebeba nini kwa ajili yao na ulimwengu mzima. Lakini kwa sababu ya roho ya kumzoelea,hawakuweza kuisikia sauti ya Mungu. ( Mathayo 13:57-58)

Ukuta mkubwa uliopo kwako ni hali ya kuwa na mazoea juu ya neno la Mungu. Ebu miili za,pale neno linapohubiriwa na kisha ukalisukumia mbali na kuona kwamba si la kwako na kuliona la kawaida tena na ukasema“ neno hili nalijua vizuri,sihitaji kulisikia tena…”  . Umesahau ya kwamba,Neno ni jipya kila siku iitwapo leo.

Huwezi kutembea na Mungu ipasavyo katika utii ikiwa una roho ya mazoea. Maana kila jambo la Mungu utaliona unalijua na huhitaji kujifunza. Hiyo ni moja wapo ya roho mbaya sana. Ebu tuliangalie jambo hili tena ndani ya biblia.

“ Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.Wakasema, Je! Ni kweli BWANA amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? BWANA akasikia maneno yao.Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.Hasira za BWANA zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.” Hesabu 12:1-3,9-10

Akina Miriamu na Haruni walimzoelea mno Musa mtumishi wa Mungu. Hata kuona kwamba Mungu hawezi kusema nao pia,kwamba Mungu atasema na Musa tu! Wakimuangalia mkewe ambaye ni mkushi,wakamdharau !’ Ni kwa sababu walimzoelea mno Musa. Kilichompata Miriamu kilikuwa ni matokeo ya kumzoelea mtumishi wa Mungu Musa; Miriamu akapata ukoma.

Leo wengi wana ukoma wa kiroho kwa sababu wamekuwa na roho ya mazoea kwa watumishi wa Mungu na kwa neno la Mungu. Ukoma wa kiroho unaweza ukawa ni kukosa kukubalika katika mambo yako,kila uingiapo huna kibali watu wakijitenga nawe kama vile uonavyo watu wakiwatenga mbali wenye ukoma.

Mtumishi wa Mungu anaweza akawa na makosa yake maana ni mwanadamu na yeye. Lakini kukosea kwake kujizuilia kupokea neno la Mungu kwa kinywa chake. Habari ya makosa yake atamalizana yeye na Mungu wake,wewe hayo hayakuhusu,fuata ya Bwana tu ili upokee.

Kitendo cha Musa kumuoa mwanamke mkushi kilikuwa ni cha Musa mwenyewe,lakini kwa sababu ya roho ya mazoea akina Miriamu wakajikuta wakiangukia adhabu mbaya sana na adhabu ile ya kupata ukoma ilisababisha watu wote wachelewe safari maana hawakuweza kuendelea mbele,nao wakakaa siku saba kwa sababu ya kosa la mtu mmoja tu.

Usiwe na roho ya mazoea katika eneo lolote lile, maana hutaweza kutembea na Mungu ipasavyo. 

Sasa,Mungu akitaka kusema na kanisa,atasema kwanza na malaika wa kanisa hilo. “ malaika wa kanisa” ni yule aliyepewa dhamana ya kusimamia na kuliongoza kanisa. Wengine husema ni “ mbeba maono” ikiwa Mungu atasema naye,nawe ukaikataa sauti ya kiongozi wako,mchungaji kiongozi wako. Basi ujue utakuwa umeikataa sauti ya Mungu.

Kila kanisa kuna kiongozi wa juu asimamaye kuliongoza hilo kanisa pamoja na wasaidizi wake. Ukishindwa kuisikia sauti ya kiongozi, ujue umeshindwa kuisikia sauti ya Mungu pia. Utii wa sauti ya Mungu unaanzia kuitii sauti ya kiongozi( baba/mama yako wa kiroho). Usitegemee kutembea na Mungu ipasavyo ikiwa huisikii sauti ya kiongozi wako,sababu sauti hiyo ni sauti ya Mungu kwako.

Sasa,jiulize ni mara ngapi umeenda kinyume na sauti ya baba au mama yako wa kiroho?  Ni mara ngapi unaambiwa uwahi ibada na unachelewa? Ni mara ngapi unaambiwa ulipe zaka na haulipii kabisa? Ni mara ngapi unaambiwa uombe ukiwa nyumbani kwako lakini wala hauombi? Ni mara ngapi unaambiwa ufanye hivi na hivi,nawe haufanyi hata moja? Je hujui kwamba umeshindwa tena umekataa sauti ya Mungu? Au unategemea Mungu ashuke mzima mzima aje kwako na kukuambia hayo? 

Sasa,ikiwa hayo huyafanyi utafanikiwaje? Maana neno linakutaka uisikie kwa bidii kutunza kuyafanya yote ndipo ukafanikiwe ( Kumbukumbu 28:1)

Mambo ya kufanya ili uweze kuitii sauti ya Mungu,kwa maana umeshindwa kutembea na Mungu ipasavyo katika utii.

  1. Toba ~ hakikisha unaingia kwenye toba akimsihi Mungu akusamehe kwa dhambi ya kutokuitii sauti yake. Na ikiwa hujaokoka unahitaji kuokoka kwanza,na uongozwe sala ya toba.

  2. Omba kwa Mungu akupe wepesi wakulishika neno lake kwa kinywa cha watumishi wake.

  3. Anza mazoezi ya kusikiliza kwa umakini na kutii yote unayoagizwa na kiongozi wa kiroho.

Inawezekana ukawa inajitahidi sana kutembea na Mungu katika utii wa sauti yake,lakini unashindwa. Ebu unipigie ili tuweze kuomba pamoja,piga kwa; 

; +255 683 877 900

Namba ya Whatsaapp ni .+255 746 446 446

Mch.Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page