KUOLEWA
- Mch. Gasper Madumla
- Oct 28, 2017
- 4 min read

Epuka mtandao wa kimapenzi,tulia kwa Bwana mpaka wakati wa kuolewa.
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Desturi yetu tuliyonayo katika mahusiano kuelekea katika ndoa ni kwamba,mwanamke ndiye anayeolewa na mwanamme mmoja. Na huo ndio utaratibu wa kiungu. Na “ kuolewa” ni tendo la heshima Kwa mwanamke. Huleta furaha si kwa na heshima Kwa mwanamke mwenyewe na hasa katika familia husika.
Kuolewa hakulazimishi Kwa maana huwezi kulazimisha mwanamke awe mke wa mtu Fulani bila yeye mwenyewe kumpenda. Biblia inatupa mfano mzuri wa sana wa mwanamke aliyeolewa katika utaratibu unaofaa, mwanamke huyo ni Rebecca ( Mwanzo sura ya 24 yote)
Kwa hila adui anajitahidi sana kuzuia mabinti wasiolewe,au wasiolewe Kwa wakati. Kuna roho kabisa inayozuia mabinti wasiolewe na watu sahihi,Kwa mfano utakuta Binti amejitunza, lakini Kila kijana anayekuja achukui muda mrefu,huondoka.
Na ukichunguza sana utagundua ni roho inayokuzuia usiolewe! Hivyo ni lazima ushughulikie mapema roho hizo Ili uingie katika ndoa mapema katika muda sahihi. Pamoja na sababu hiyo ya kiroho,zipo pia sababu nyingi zinazozuia binti kuchelewa au kutokuolewa kabisa.
Pia zipo sababu nyingine ambazo mabinti wenyewe husabanisha hata wasiolewe au waolewe na watu wasio sahihi Kwa mfano;
1. Hali ya kuchagua chagua sana.
Kuna mabinti ambazo huchagua sana kiasi kwamba mpaka wanatoka nje ya kusudi la Mungu. Mi nakumbuka nilimwona Binti mmoja ambaye ni mtaalamu wa kuchagua chagua,yaani mpaka Leo hajaolewa,na amezeeka Kwa sasa!!! Kwa maana Kila anayekuja hupima katika vipimo vyake alivyojiwekea na akikuta kipimo hata kimoja kikipungua basi anamkatalia. ( Ni kweli,ni vyema kuchagua kilicho Bora, lakini isiwe too much!!!
2. Hali ya kujiachia sana Kwa wakaka!
Hivi unajua kama binti akijiachia kwa wakaka,anajiwekea uzito wa kutokuolewa. Kwa maana hakuna mwanamme anayetaka kuoa binti ambaye ni mwepesi kuingilika. Ukweli ni kwamba,kuna baadhi ya mabinti ambao wanajiwekea kikwazo wenyewe. Tabia ya kujilahisisha kwa wakaka inaondoa nafasi kubwa ya kuolewa kwa mabinti.
3. Mitazamo mibaya pamoja na mitazamo ya wazazi
Kuna mitazamo mingi isiyofaa inayoendelea kugonga vichwa vya mabinti wengi ambayo inakwamisha mahusiano. Mfano; Wengine wanatazama suala Zima la makabila na walishaambiwa kwamba kabila hiki linapiga au ni wahuni n.k ( inawezekana ikawa ni kweli,but hicho sio kigezo kikubwa Kwa maana hutegemea na hali yake ya kiroho)
Kwa mitazamo kama hiyo,unaweza ukakuta Binti anashindwa kumkubalia mkaka aliye sahihi kabisa ya kuao. Wazazi nao huchangia kukwamisha Binti kuolewa pamoja na kwamba wazazi Wana mchango mkubwa wa kuwasaidia mabinti zao kuolewa. Lakini wapo wazazi ambao hawataki mabinti zao kuolewa na watu waliowachagua wao wenyewe isipokuwa wazazi wanataka kuwachagilia wachumba,na mwisho wa siku mabinti wanachelewa kuolewa!
Ni lazima utambue yafuatayo;
Wewe ni wathamani,hivyo usikubali uchezee ujana wako
Yupo mwanaume mmoja tu atakaye kuwa mume wako,na sio wanaume wengi.
Upo wakati muafaka wa kuanza uchumba hatimaye ndoa takatifu.
Hatuna maswala ya boyfriend na girlfriend katika wokovu,bali tuna uchumba mtakatifu. Kwa maana ile dhana ya u- boyfriend na girlfriend ni dhana ya kuishia kwenye dhambi ya ngono. Katika wokovu ni mwiko mambo hayo.
Usiwe na haraka sana katika mambo yako ya kuolewa. N.K
Sasa,niweze kumjibu huyu dada kwa swali lake lilipo hapo juu kama sehemu ya fundisho hili sawa sawa na neno la Mungu. Awali ya yote ni vyema ukafahamu kwamba ili uweze kutambua mwanaume wa kweli unahitajika kwanza wewe mwenyewe uwe wa ukweli. Kwa maana haiwezekani tena ni vigumu kutambua wa ukweli ikiwa wewe si wa ukweli. Siku zote wale wanaofanana hutembea pamoja ( Amosi 3:3).
Hivyo basi,ukiwa wewe ni binti mwenye hofu na Mungu,uwe na uhakika wanaume watakao kuja kwako ni wa namna hiyo hiyo uliyonayo wewe. Akija mwanaume na kusema anataka kukuo,wewe usishangae sana kwa maana leo hii imekuwa ni mtindo wa wanaume kusema hivyo maana wengine wanakuhitaji wakutumie na kukuacha. Bali usikiapo maneno mazuri ya mwanaume kwamba anataka afunge ndoa na wewe,hapo mambo ya kufanya ndipo ufanye yafuatayo;
01. Mwambie “subiri nitakujibu”
Hapo;wala usioneshe kwamba umemkubalia au umemkatalia. Katika kipindi hicho cha kumuweka benchi huyo mwanaume kwa kuwa umemuambia subiri nitakujibu,hapo ndipo unapofika na kumuuliza Mungu juu ya huyo mwanaume. Na ikiwa utaomba vyema,uwe na uhakika utamjua ndie au la! Sasa usiangalie vitu vya nje kwa maana macho ya mwili hudanganya. Wengi wamekoseshwa na mitazamo ya macho yao,wameacha mambo ya Mungu na kugeukia macho ya kawaida ya mwili.
Ikiwa hakika huyo mwanaume ni wa Bwana,uwe na uhakika atakuoa tu hata bila kulala naye. Kulala na mwanaume sio kigezo cha kuolewa,bali ni kigezo cha kuachwa haraka na ni kitendo cha kufanya dhambi mbele za Mungu. Mwenye kuhitaji kuoa haitaji penzi kwanza bali anahitaji usafi wa moyo na utakatifu wa kweli.
Hivi muonjaji onjaji wa samaki ni mnunuaji? Umewahi kujiuliza hivyo. Mtu anayeonja onja hakika sio mnunuaji bali ni muharibifu na hatari mtu huyo.
Hivyo utulivu wewe na Mungu unahitajika sana ili uweze kujua uhalisia wa huyo mwanaume. Nasema utulivu na Mungu sio utulivu na huyo mwanaume au utulivu na shoga yako ,hapana bali unahitaji ukae ukiomba mbele za Mungu akuoneshe yote yaliyojificha kwa huyo mwanaume.
02. Epuka mitoko naye,kwa namna yoyote ile pamoja na simu za mara kwa mara.
Ikiwa kama utaruhusu kutoka naye japo kwa nia njema basi ujue yatakushinda hayo! Maana katika kila mtoko kuna mazungumzo mengi ambapo si rahisi kujizuia hisia zako hata kama umeokoa kwa kunena kwa lugha mpya!! Tena athari moja wapo ya kutoka mara kwa mara pamoja na mtu akupendaye ni kuleta picha mbaya wa kanisa na kwa watu kwa maana mtahiniwa kwamba ni wazinzi. Hata hivyo tabia hii itakunyima nafasi ya kimaombi na Bwana na hapo hautajua yaliyo mapenzi ya Mungu.
Lazima uwe na mipaka yako mizuri,kwa kuepuka simu za mara kwa mara kwa maana si kweli kwamba mtakuwa na mambo muhimu sana hata kuongea mara kwa mara kwa njia ya simu. Kumbuka kwamba mazungumzo mabaya hujaribu tabia njema. Kwa kuwa umemuambia asubiri majibu yake basi na hapo uepuke kuzungumza naye mara kwa mara katika simu hata mazungumzo ya ana kwa ana.
Ikiwa kama kuna watatu au zaidi wamekutamkia kukuoa na wao wenyewe hawajuani,fanya;
Kumbuka kwamba kila binti ni lazima atafufuatwa na wanaume kutakwa. Hivyo kufutwa sio jambo la kushangaza kwa binti,lakini wakiwepo wenye kutaka kuoa basi dawa ni ile ile. Mmsikilize kisha mwambie tena“ subiri nitakujibu ” usikubali mapema eti kwa sababu ya kuolewa,hapana! Ni vyema kuwa makini na Mungu katika eneo hilo kwa maana ni Yeye Mungu kwa Roho wake wa milele atakaye kujibu kwa usahihi zaidi.
Ni bora ukose mengine sio kuolewa! Unahitaji kutulia sana. Usikubali kufungua mlango wa mapenzi kwa yeyote yule kwa maana endapo utafungua,hautaweza kumsikia Roho mtakatifu katika eneo hilo bali utaendeshwa na mapenzi.
Unajua suala halipo kwa wingi wa wanaume wanaokujia bali suala ni namna gani unavyostahimili ujio wao tena ni namna gani unavyoweza kumsikiliza Roho mtakatifu kwa ajili ya ujio wao.mpango wa shetani ni kukuletea asiye wako ili uwe na kilio katika ndoa yako na ukose Bwana.
Kwa msaada zaidi waweza kunipigia simu sasa +255 683 877 900
Mchungaji Gasper Madumla
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE
Comentarios