top of page

KUOKOKA KATIKA AGANO LA KALE

Updated: Sep 30, 2022


Swali la kujiuliza;


Watu wa agano la kale waliokokaje-Wakati Yesu Kristo alikuwa bado hahaha katika mwili? Je kulikuwa hakuna wokovu? Na kama kulikuwa hakuna wokovu,Ina maana wote walienda motoni?


Unaweza ukawa ukijiuliza juu ya watu waliokua wakiishi kabla ya ujio wa Yesu,kwamba wote waliishia wapi? wote Wamekwisha hukumiwa kwa kuwa walikuwa wakiishi kabla ya wokovu? Na ikiwa ndivyo hivyo,je utasema kwamba hata wakina Ibrahimu,Musa na wengine kama hao wote hawajaokoka? Walipotea? Kama sivyo,Sasa inakuwaje hapo? Anyway!,nataka ulione hilo siku ya leo. Sasa,ili uweze kujua jibu sahihi katika swali hili ni lazima ujue ujumbe mkuu wa biblia ( the main message of the bible). Au “kusudi” la biblia. Kusudi kuu la biblia ni kuokolewa kwa watu kupitia Yesu Kristo / wokovu ( Redemption is the main message of the bible).


Kwa kuwa Mungu huona mwisho hata mwanzo wa kila kitu. Ukombozi kwa watu wote ndio mpango mzima aliouandaa Bwana MUNGU kwa watu wote pale watakaomuamini Yesu na kumpokea ndani ya mioyo yao hata kabla ya anguko la dhambi ya Adamu na Hawa maana Mungu anampango wa kumkomboa mwanadamu. Tunafahamu pale mwanadamu alipoanguka dhambini,Mungu mkakati wa Mungu wa kumkomboa ukachukua nafasi. Kumbuka tena Kipindi cha agano la kale kilikuwa ni kipindi cha kivuli kwa mambo ya agano la kale (-Waebrania 10:1a) 


Hivyo watu wa agano la kale waliishi kabla ya ujio wa mwokozi na sisi leo tunaishi baada ya ujio wa mwokozi. Hivyo ni sawa na kusema watu wa agano la kale waliishi kabla ya“Yesu” nasi watu wa agano jipya tunaishi baada ya “ Yesu ”  ukichunguza kwa makini maelezo haya utagundua kwamba “hakuna alimuona Yesu moja kwa moja physically” ingawa Yesu U hai,anaishi hata sasa.


Sasa watu hao waliokokaje,au kulikuwa hakuna wakovu?


Watu wa agano la kale waliokoka kwa kumuamini Yesu Kristo mwokozi ambaye waliamini ujio wake,na sisi watu wa agano jipya tunaokoka kwa kumuamini Yesu Kristo mwokozi ambaye tunaamini ujio wake miaka 2000 iliyopita. Watu kama akina Ibrahimu,Musa,Eliya na wengine waliomuamini Mungu wakiitazamia ahadi ya ukombozi katika Kristo Yesu,walikuwa wameokoka sawa na wewe uliyeokoka kwa kumuamini Mungu katika Kristo Yesu.

Mchungaji unayatoa wapi haya?


“ nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” Mwanzo 3:15

Kwa mara ya kwanza Bwana MUNGU anaonesha kusudi kubwa la kumkomboa mwanadamu kupitia Yesu Kristo ambaye “ ni uzao wa mwanamke” kwamba yeyote atakaye muamini na kumpokea ataokoka,na kuwa na uzima wa milele. Ahadi hii ndio ahadi ya kwanza ya ujio wa mwokozi Yesu Kristo ya ukombozi na pia ni ahadi ya kumshughulikia adui shetani na utawala wake. Na ndivyo ilivyo. Wewe je umeweka imani yako kwa Yesu Kristo na kufanya maamuzi ya kumuishia Yeye? Hujachelewa bado,fanya maamuzi sasa ya kuokoka YESU U HAI


Kwa imani tu juu ya ahadi ya ukombozi,iliwaokoa. Ebu muangalie Ibrahimu mtu aliyekwenda na ahadi za Mungu. Muangalie Musa. Na watu wengi wamekuwa na mtazamo mbaya wakidhani kwamba Musa kwa sababu hakuingia kwenye nchi ya Ahadi basi hakuingia mbinguni!!si kweli kwa mtazamo huo! Maana unaweza ukajiuliza tu,ikiwa unamtazamo huo mbaya mbona Musa huyo huyo pamoja na Eliya wakimtokea Yesu ( Mathayo 17:1-3),sasa inawezekekanaje jambo hilo.Bwana Mungu,ameandaa mpango mzuri kwako,mpango wa wokovu kwa kumuamini Yesu na kumpokea. 


Wako wengi walioangamia kwa sababu ya kushindwa kumuamini Bwana Yesu katika agano la kale,lakini ni vivyo hivyo katika agano hili jipya wasiompokea Bwana,wamepotea. Jambo la msingi ni ukombozi kwa Yesu ambaye kwa kweli hukumuona kinadharia bali kwa imani kwake kwa sababu Yeye ni Mungu yupo,na anaishi hata sasa.


Kwa huduma ya maombezi,nipigie sasa kwa namba hizi;+255 683 877 900


Namba ya What’sapp ni +255 746 446 446


Mch. Gasper Madumla


UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page