KUMTAFUTA MWENZI WAKO
- Mch. Gasper Madumla
- May 9, 2017
- 3 min read

Mwl John C Ntogwisangu
Na mwl. John C.Ngogwisangu.
💖 *JINSI GANI YA KUMPATA MWENZI WANGU WA MAISHA..*❓
Mke /mume unayemuhitaji hayupo Kanisani, kijijini kwenu, chuoni, kwenye Makongamano au kwenye mitandao ya kijamii. Mke /mume unayemuhitaji yupo ndani yako mwenyewe.. *Yes..!* Yupo ndani yako na si Nje.
Hivyo badala ya kuhaingaika kumtafuta nje, Badili mtazamo na anza kumtafuta ndani yako. Mtu unayemuhitaji si mwingine bali ni UBAVU ambao umetoka ndani yako, hapo ulipo sasa HAUJAKAMILIKA mpaka pale utakapoipata sehemu ya Mwili wako iliyoondolewa. Ukishaupata huo UBAVU wako hapo sasa mtakuwa sehemu mbili za Mwili ambazo zitaungana na kuwa Mwili mmoja. _( Mwanzo 2 :24)._
Kama mwenzi unayemuhitaji ni sehemu yako iliyoondolewa, unapaswa KUJIFAHAMU kwanza wewe kisha utafahamu ni kipi kilichokosekana kwako ambacho kitakufanya kuwa *MTU KAMILI.* Na hii ndio maana ya kumtafuta mwenzi wako ndani yako na si nje.. Ila wengi bila ya KUJIFAHAMU wao ni wa kinanani hurukia kutafuta wenzi wao wa Maisha na kujikuta wakiwa Katika *MAJUTO* makubwa.
Katika Mwanzo 2.. Tunaona Mungu anamtoa Hawa ndani ya Adamu na kumuweka Katika bustani ya Edeni, Na si Katika bustani ya Edeni na kumuweka kwa Adamu. *_Asili ya Hawa si bustani ya Edeni bali ni ndani ya Adamu, bustanini palikuwa ni eneo lao la Kukutania na kuanza Mahusiano (maisha yao ya ndoa)._
*Katika Edeni (mazingira) yako kuna wakina Hawa wangapi? Kwa macho ya kawaida bila kuwa na Mtazamo wa Kimungu unaweza ukawaona wakina Hawa wengi.
Lakini Ukweli ni kwamba kuna Hawa *mmoja TU* ambaye ndio sehemu ya Mwili wako, hao wengine ni wakina Hawa wa watu wengine na si wako. Kilimchosaidia Adamu kumfahamu Hawa pale bustanini ni sababu alikuwa *ANAJIFAHAMU YEYE NI NANI*,
hivyo alipomuona Hawa alimtambua na kusema _”Huyu ni mfupa Katika mifupa yangu na nyama Katika nyama yangu“_ Bila kujitambua asingefahamu kama Hawa ni mtu ambaye ametoka ndani yake. Kama asingejifahamu labda angemuona Simba au Chui na kusema *_”Huyu ni mfupa Katika mifupa yangu na nyama Katika nyama yangu”._* Kama wengi Leo wanavyowaona watu ambao ni kama Simba kitabia huku wakidhani ni wakina Hawa wao, na KUISHIA _kuraruliwa MIOYO yao na kubaki na Majeraha Sugu._ *
_Si kila unayemuona anakufaa Katika bustani ya Edeni kweli anakufaa, kuna wengine ni Simba, Chui, mbwa mwitu watakaoharibu maisha yako._* Ni *HATARI* kutaka kuingia kwenye Ndoa bila kuwa na Ufahamu wa kutosha kuhusu Kile ambacho Mungu AMEKUSUDIA juu ya maisha yako. Kila mtu kuna kitu fulani ambacho Mungu ameweka ndani yake ili Akitimize ( *KUSUDI LA KUUMBWA kwako*), haupo duniani kwa BAHATI MBAYA, upo kwa KUSUDI FULANI.
Je unalifahamu ni Lipi..❓ Kama haujifahamu, utawezaje kufahamu ni sehemu gani iliyoondolewa kwako? Kumbuka bila *MAONO* (Ufahamu, kujitambua) utashindwa KUJIZUIA. _Mithali 29 :18._*Mtu unayepaswa kuwa naye anatakiwa kuwa na UWEZO wa KUKUSAIDIA kutimiza KUSUDI hilo, anatakiwa awe kweli ametoka ndani yako.* Si kila mtu Anaweza kukufikisha pale ambapo Mungu anataka Ufike. Si kila mtu unaweza kuoa/kuolewa Naye.
_Chuma na udongo vinaweza vikashikamanishwa na kuwa kitu Kimoja, Lakini Mvua itakapokuja na jua likawaka, Ufa lazima utokee na kila kimoja kitakaa sehemu yake._
Ndivyo ilivyo pale watu ambao wenye malengo, Makusudi, Wito tofauti watakapokutana, hawataweza *KUDUMU*. Namaliza kwa kukuachia swali hili..👇👇
*UNAJIFAHAMU WEWE NI NANI? UNAFAHAMU KITU GANI AMBACHO MUNGU AMEWEKA NDANI YAKO*❓
Majibu ya maswali hayo hutayapata kwa rafiki zako, wazazi wako, Mchungaji wako wala mimi siwezi Kukupa majibu Sahihi. *KAA NA MUNGU KATIKA MAOMBI NAYE ATAKUFUNULIA HAYO.**ACHA KUOMBA MUNGU AKUPE MKE /MUME, OMBA MUNGU AKUPE KUJIFAHAMU KWANZA.*
Kumbuka…. 👇👇
*Mke /mume unayemtaka yupo ndani yako na si NJE.* *
*Karibu Watsap groups. 0712463344.*
UBARIKIWE.
コメント