KUCHEMSHA CHURA KWENYE SUFURIA.
- Mch. Gasper Madumla
- Apr 30, 2017
- 1 min read
Na Mtumishi wa Mungu Humprey Fungo.
Bwana Yesu asifiwe…
Ukimchukua CHURA na kumuweka kwenye sufuria yenye maji ya moto sana , chura huyo ataruka haraka sana na kutoka nje ya sufuria hiyo.
Lakini ukimchukua CHURA na kumuweka kwenye sufuria yenye maji ya baridi atabaki kwenye maji hayo bila kuruka nje ya sufuria, ukiichukua sufuria hiyo yenye maji ya baridi yenye CHURA ndani , ukaiweka kwenye jiko na kuanza kuyachemsha maji taratibu, CHURA atabaki anazubaa ndani ya maji hayo , joto la maji litaongezeka lakini CHURA atabaki humo humo kwenye sufuria , utayachemsha maji mpaka yatatokota CHURA atabaki humo humo bila kuruka nje ya sufuria, itafika hatua
atashtuka atatamani kuruka nje lakini atakuwa amechelewa sana mwishowe atakufa katika maji hayo ya moto.
Je ni nini kimemuua CHURA , wakati maji yalipokuwa na joto dogo CHURA alitumia nguvu nyingi sana kurekebisha joto lake ili lilingane na joto la maji akajifanya mjanja . Lakini mwisho wa siku alichoka akaamua kuruka akashindwa ,wakati wa kuruka nje ukipofika alishindwa kujiokoa kwa kuwa alikuwa Hana nguvu tena . Laiti Kama CHURA angejua hatari iliyo mbele yake angeruka nje ya sufuria wakati maji bado ni ya baridi.
Mpendwa usiwe Kama CHURA wakati wa kuruka nje ya sufuria ni Sasa usisubiri mpaka maji yachemke Utakuwa umechelewa sana , watu tuliookoka tumeruka nje ya sufuria mapema ,
Itafika wakati utatamani Kuokoka lakini hutaweza kupata nafasi hiyo Utakuwa umechelewa sana, nafasi ya kuokoka haitakuwepo tena.
Wakati uliokobalika ni Sasa.
Na mtumishi Humprey Fungo
Comments