KODI YA HEKALU.
- Mch. Gasper Madumla
- Jun 10, 2019
- 3 min read
Updated: Sep 2, 2022

“ Kodi ya hekalu / The temple tax. “
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi ,
Katika kipindi cha Musa, kulikuwa na kitu kiitwacho “Hema ya kukutania”. (au mahali patakatifu) ilikuwa ni maskani ya BWANA / mahali pa ibada ambapo watu wazima matajiri kwa maskini waliagizwa kulipa nusu shekeli, ni fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli nazo zitatunzwa kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania, kazi kubwa ya nusu shekeli ilikuwa kulitunza hema ya kukutania( Kutoka 30:11-16).
Hivyo kodi ya hekalu ilikuwa ni nusu shekeli iliyolipwa kila Mwaka kwa ajili ya kutunza hema ya Bwana. Hata hivyo katika kipindi cha agano jipya, baada ya kubomolewa kwa hekalu katika mwaka 70 BK, Warumi walitumia kodi hii ya nusu shekeli kutunza hekalu la Jupita. Ingawa kulikuwa na upinzani Mkubwa kutoka kwa Masadukayo ambao walikuwa mstari wa mbele kuipinga kodi ya hekalu.
( Kwa sababu haikuwa katika makubaliano mazuri)
Kipindi fulani, Yesu naye alipoingia Kapernaumu alikutana na kodi ya hekalu. Wale watozao kodi, hawakujua kwamba Yesu Mwenyewe ndiye haswa hekalu tena hawakuhitaji kuthamini jengo lililojengwa na mwanadamu. Biblia inasema; “24 Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa.
27 Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.“ Mathayo 17:24,27
Ufunuo juu ya kodi ya hekalu.
01. Yesu hulipa kodi. ( Mathayo 17:24)
“ Hata walipofika Kapernaumu, wale watozao nusu-shekeli walimwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nusu-shekeli? Akasema, Hutoa.“
Neno linatuambia, Yesu mwenyewe alikuwa akitoa au kulipa kodi. Maana take nini? Bila shaka Yesu anatufundisha kuwa, Yeye pia alikuwa mmoja wa watu mwenye kuheshimu mamlaka iliyopo, naye ni mlipa kodi ili kusudi kuwafundisha watu wote wasikwepe kulipa kodi. Ingawa Yesu,
alifahamu zaidi kuliko wale watozao nusu shekeli ya Hekalu, kwa maana Yeye mwenyewe ndiye hakalu lenye maana. Lakini alilipa kueshimu tawala iliyopo. Sasa Leo, hii ebu jiulize ni wakristo wangapi wanaokwepa kulipa kodi kwenye serikali zao? Au ni wangapi waliokamatwa kwa sababu tu hawakulipa kodi? Utagundua ni wengi wameshindwa kulipa kodi. Ni vyema kujua ili, kushindwa kulipa kodi yoyote ya serikali yako ni kupingana na hiyo mamlaka, na kwa kufanya hivyo ni dhambi!!!
02. Samaki aliyebeba kodi yako.
Kulikuwa na samaki wengi katika ziwa lile, lakini maelekezo yaliyotolewa yalimlenga samaki mmoja tu, yule“azukaye kwanza” huyo ndiye aliyebeba kodi ya Petro ( pamoja na Yesu). Yesu alimpa maelekezo muhimu sana Petro, yatakayomsaidia Petro kupata kodi, maana hakuwa na kodi, na wakati huo wanahitajika kulipa kodi.
Hivyo ilikuwa ni kazi ya Petro kutembea kwenye neno la Kristo( maelekezo) ili afanikiwe kupata kodi. Kodi ilikuwepo lakini imefichwa kwenye kinywa cha samaki, hivyo ili kuipiata ilihitaji utii Wa juu Wa kutembea sawa sawa na Neno la Kristo kwa maana Kama Petro asingelifanya kile alichoambiwa na Bwana basi ukweli upo wazi, asingelipata hiyo kodi😂😂😂.
Leo hii, tunahitaji kulipa kodi au malipo mbali mbali, na tunagundua kwamba hatuna pesa ya kulipa ingawa tunakubaliana kulipa lakini ukweli hatuna pesa!! Unadaiwa lakini, hujui unalipaje maana huna kitu. Mazingira haya haya ndiyo mazingira aliyokutana nayo Petro. Kumbe unaweza ukawa na Yesu, lakini ukakosa pesa ya kulipa kodi!!! Utaipata hiyo pesa ya kulipa kodi mpaka utakaposimama na neno la Kristo. Unajua Petro alikuwa ni mwanafunzi mwenye kujua Siri ya kufanikiwa, naye akafanya kama alivyoagizwa,
kweli samaki huyo alimvua Yule “ Wa kwanza azukaye” na hatimaye akafanikiwa kupata kodi ya hekalu akalipa kwa ajili take na kwa ajili ya mlipa kodi Yesu.
Jambo la kwanza la kujifunza, ni “namna ya kufuata maelekezo” ukweli ni kwamba Petro alijaribu kutembea kwenye Neno/ maelekezo sahihi, kwa maana kama angeliamua kutafuta samaki yeyote asingelipata kodi ya kulipa! Hata leo, lipo Neno la BWANA lenye kutuongoza katika kufanikiwa sehemu mbali mbali, lakini wengi hatuliishi neno.
03. Uinjilisti.
Tukio la kuvua halina tofauti na kazi ya injili kwa wote, kuokoa waliopotea. Bila shaka ,injili ya BWANA inapohubiriwa, ni lazima roho za watu waliopotea zivuliwe/zipatikane. Petro mvuvi anafananishwa na mwinjilisti, samaki ni roho ya mtu iliyopotea. Sasa; makanisa mengi ya Leo yapo katiba majumba ya kupanga mahali ambapo kodi inahitajika kulipa kila mwisho wa mwezi. Wakati mwingine kanisa linaweza likawa linajitegemea kwenye jengo lake binafsi, lakini bado utagundua linahitaji pesa ya kulipa mambo mengi.
Sasa; ni kana kwamba Mungu analiagiza kanisa litoke likavue samaki, ambaye samaki huyo atakuwa na kodi ya kulipia mambo mengi. Lakini kanisa ni lazima litembee kwenye kanuni halisi za uvuaji ( litembee kwenye neno la Kristo, ili kusudi lifanikiwe kumleta samaki sahihi aliyebeba kodi ). Ukichunguza hiki ninachokufundisha leo,
utagundua kwamba samaki wapo wenye kodi lakini, wavuvi hawapo tayari! Kanisa likikaza kwenye injili ya Kristo, kuwaleta watu kwa Kristo basi ni dhahili kuna mambo madogo madogo yatakaa sawa. Lakini kanisa la leo limesahau kazi hii ya uinjilisti, kiasi kwamba imefika wakati badala ya injili ihubiriwe yanahubiriwa mambo mengine. Toka sasa👣, nenda kavue, samaki yupo tayari BWANA amemwandaa kwa ajili yako .
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900
Whatsapp+255 746 446 446 .
Na Mch.G.Madumla.
UBARIKIWE.
Comments