KITABU CHA UFUNUO.
- Mch. Gasper Madumla
- Aug 30, 2018
- 3 min read
UCHAMBUZI MFUPI :
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi sana ( a quick look).
Kama jina lake lenyewe lilivyo “ kitabu cha ufunuo” kimejawa na ufunuo, hata ukiniuliza maana ya mafunuo hayo, mimi sijui kwa kweli lakini nataka nikupe japo muktasari wa kitabu hiki cha ufunuo kutokana na kiu ya wasomaji wengi wanaotembelea hapa kila siku. Ni jambo la kutia moyo kuona idadi kubwa ya watumishi mbali mbali duniani wakijifunza neno la Mungu hapa, ebu cheki kwa sasa rate / takwimu ya watu wanaoona ( viewers) ni 800 hadi 1000 kwa siku, yaani kila siku na takwimu ya wanaotembelea ( Visitors) wakijifunza neno ni watu 300 – 400. Wengi wametafuta kujua habari za kitabu cha ufunuo. Nami ni vyema leo niandike japo kwa ufupi sana.
Mwandishi wa kitabu cha ufunuo anajitambulisha mwenyewe kama mara nne kwamba yeye ni Yohana mtume ( Ufunuo 1:1,4,9.22:8). Huyu mtume ndiyo yule alikuwa mmoja wa watoto wa Zebedayo ( Mathayo 10:2). Bila shaka Yohana alikuwa ni Myahudi. Ufunuo kiliandikwa kwenye kipindi ambacho kwa kweli wakristo walikuwa wamegubikwa mateso, hivyo inakadiriwa kama AD 95 kitabu kiliandikwa. Makanisa saba ya Magharibi kwenye Asia ndogo ndio hadhira husika iliyoandikiwa ( leo ni mimi na wewe ndio tumeandikiwa). Lengo kuu la kitabu cha ufunuo ni kuwatia moyo waamini wasimame imara kwenye mateso wakingoja ujio wa Kristo utakaowanyakua wenye haki na kuwahukumu wakosaji!/ waovu.
Lakini pia “ Kusudi la kitabu cha ufunuo ni kuwatia moyo waamini katika Kristo kwamba shetani ataongeza mateso kwa waamini lakini waamini wanapaswa kuwa waaminifu, kuvumilia hata kufa. “Kitabu cha ufunuo kinaonesha mambo ya aina mbili;
Mambo ya zamani ( yaliyopita)
Mambo ya baadae sana ( yajayo)
Na hapo ndipo penye utata kwa msomaji kwa maana sasa mtu hujiuliza “ jambo hili nilisomalo ni lililopita au ndio linakuja“. Lakini lazima utambue ya kwamba neno la Mungu lolote limevuviwa, hivyo ikiwa unahitaji kuelewa kwa neno hilo, huna budi kumwomba Roho mtakatifu akusaidie kukupa ufunuo juu ya kilichoandikwa. Hivyo “ Ufunuo ” kinaeleza lugha yake katika picha na taswira. Lakini pia kuna tarakimu zilizoandikwa, nazo zina maana kubwa sana kimaana, kwa mfano tarakimu ya namba saba utaona kumeandikwa “ makanisa saba, mihuri saba, roho saba, vinara saba, tarumbeta saba” hivyo namba saba huwakilisha “ukamilifu” pamoja na tarakimu nyingine. Hivyo msomaji anapaswa kujua maana ya tarakimu kuanzia namba moja ili kusudi anapokutana na tarakimu iliyoandikwa kwa lengo la kujua maana imlahisishie kuelewa.
Unajua mwanzo na mwisho wa kitabu hiki ni kama unaangalia tamthilia fulani hivi kwa sababu matukio yake yamebeba uhalisia wa vitu kwa lugha ya picha. Kitabu kinaonesha matukio ambayo mwisho wake yanafikia kwenye kuangamizwa kwa uovu na kuanza kwa Yerusalem mpya ya milele ambayo kila mwamini huangalia akitaraji kufika huko. Ufunuo kimebeba matukio makubwa saba ambayo yote ni maono. Ambayo maono hayo yanaanzia kwenye maono ya kanisa halisia pamoja na Yesu akiwa kichwa cha kanisa na kumalizikia kwenye maono ya uzima wa milele.
Jambo moja muhimu kujua kwenye kitabu hiki ni kwamba ufunuo huu ni wa Yesu hivyo ni jambo la kiroho sana ambapo msomaji anapaswa awe rohoni ili kusudi aweze kuelewa kilichoandikwa. Sio rahisi lakini inawezekana kuelewa kwa msaada wa Roho mtakatifu. Uwe mwangalifu sana unaposoma ufunuo kwa maana usije ukabeba jambo au ufunuo sivyo ndivyo kisha ukafundisha sivyo ndivyo,maana ni afadhali ukae kimya ukiomba kuelewa kwanza ndipo ufundishe.
Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi, basi Wasiliana nami Kwa + 255 683 877 900
Na Mch. Gasper Madumla.
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Comments