top of page

KIBURI.

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

  1. Kiburi cha uzima.

Fikiria mtu ambaye aombi kabisa kwa sababu si mgonjwa. Haendi kanisani kwa kuwa haoni haja ya kwenda kwa sababu ataboreka hivyo ni afadhali atume watoto waende badala yake. Au anaona ni afadhali atume sadaka zake kwenye simu kwa mchungaji lakini yeye hubakia nyumbani maana anaona shida kuchangamana na watu wengine. Fikiria tena mtu fulani ambaye ana utele maisha au ni mdada mazuri hivi,kwa sababu hizo zinamfanya kujiona ni wa viwango vya juu kuliko wengine.

Mtu yeyote wa tabia hizi huitwa ni mtu mwenye “ kiburi cha uzima” Hivyo kiburi cha uzima ni pale mtu anamwacha Mungu kwa sababu ya uzima alionao kwenye mwili wake.

Hivi unajua hata kule kushindwa kuomba ni kiburi? Ndio ni kiburi kabisaa!!!,kwa sababu ukiwa ni mwanadamu,basi ujue unamwitaji Mungu akusaidie na ili akusaidie ni lazima uombe,vipi ukikataa,? Je hutakuwa na kiburi? Jiulize.

  1. Kiburi ni nini hasa ?

Ni hali ya kujisikia au kujiona bora zaidi ya wengine na kukataa kusaidiwa. Kiburi ni tabia ya shetani na ndio sifa yake ya kwanza ya pili ni udanganyifu.Kumbuka; shetani kabla ya kuwa shetani alikuwa malaika,kiongozi wa sifa “ rusifa“. Naye kwa kuwa alikuwa kiongozi mkubwa wa sifa,alitamani asifiwe yeye badala ya Mungu. Na hapo ndipo akaanguka hata kuwa shetani. Kwa kuwa ibilisi ana kiburi tangu hapo zamani,kiburi hicho hicho ndicho kilachomwangusha Adamu na mkewe Hawa ;

kwa maana walikula matunda ya mti waliokatazwa. Walikula wakitamani kujua mema na mabaya,wawe kama Mungu,na hii ndio tabia ambayo shetani alipanda kwa mwanadamu. Kwa lugha nyepesi Adamu na Hawa walitaka kuinuka zaidi ya mipaka yao waliopewa na Mungu na hicho ni kiburi

Hivyo ikasababisha kiburi kuwa ndani ya mwanadamu anayezaliwa. Na huu ndio ukweli,kwamba kila mtu anachembe chembe ya kiburi, ila dawa yake ni kuokoka na Roho mtakatifu kushughulikia hiyo tabia.

  1. Kiburi ni chukizo kwa Mungu.

Biblia imejitahidi kueleza sehemu nyingi kwamba kiburi au moyo wa kiburi ni machukizo kwa Mungu. Hivyo yapo maandiko mengi yanayoeleza kiburi ni chukizo. Lakini tuliangalie hili;

“Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA;Hakika, hatakosa adhabu.“ Mithali 16:5

Ukiwa na moyo wa kiburi basi ujue umekuwa ni chukizo kwa BWANA. Na ni lazima upate adhabu kama sehemu ya malipo ya kiburi ulichonacho. Moja wapo ya adhabu au tokeo la kiburi ni “kukataliwa“. Ebu cheki,mtu yule ambaye hupenda kujisifu na kujiona ni bora sana kuliko wengine,alafu angalia matokeo yake,utagundua ni lazima watu watakuwa hawana furaha naye,yaani amekataliwa kutoka kwenye mioyo ya watu.

Hujawai kuona mtu wa namna hii mwenye “mbwembwe” za kujiinua inua,anavyokataliwa? Au watu wanamchukia kwa sababu ya kiburi chake cha kujielezea mambo yake ili aonekane.

Jamani kuna watu wanapenda sifa !!! Watu wa namna hii,ujiinua na kujiweka juu katika mazungumzo yao au kimienendo yao kiasi kwamba wanaboa kwa kweli!!! Mbaya zaidi kwa watumishi wanapokuwa wamekamatwa na tabia hii ya shetani,utakuta akijisifu sana na yupo madhabahuni hapo,kwa hiyo lisaa lizima hakuna alichokieleza chenye maana hata kimoja!!! Sasa unamweleza nani hayo mambo yako??? Ni nani kakuuliza? Yanatusaidia nini sisi tuliokuja kukutana na Mungu? Hii ndio tabia inayotesa kanisa la leo,kiburi ni kibaya!!!

  1. Mungu hawezi kumwinua mtu mwenye kiburi.

Ukimwona mtu mwenye kiburi kainuka labda kiroho,kapanda,ujue kajipandisha yeye mwenyewe wala sio Mungu. Kwa maana Neno linasema Yeye Bwana huwapinga wenye kiburi ( Yakobo 4:6). Sasa Mungu hawezi kukinzana na neno lake. Kiburi ni siri ya kushuka wala sio kuinuliwa.

  1. Nalijifunza kujishusha kupitia mrembo mmoja kule Sinza ( Home land), Mtazame mwanadada huyu;

Pale mtaani petu nilipokulia Sinza,Kulikuwa na hosteli ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar. Hapo pana mwanadada mmoja ambaye sijui jina lake lakini kile ninachokijua kwake ni kujishusha kama tabia nzuri aliyokuwa nayo kipindi hichooo. Tulipokuwa maskini,akipita huyo dada basi lazima atasalimia wote,na kila mtu alimchukulia wa thamani kwake kiasi kwamba kama ndio wewe ni mwanaume unaweza sema anakutaka kimapenzi labda,na kumbe wala! Mdada wa watu ndio ilikuwa tabia yake yaani alikuwa hajisikii. (Kwa uzuri alikuwa mzuri wewe unafahamu ninaposema “mdada mzuri“) aliwapita wenzake kwa urembo,lakini yupo peace na watu wa kila namna. Sasa,kwa kijitabia hako tu,kilisababisha kupendwa na kila mtu hapo maskani. Mrembo wa watu hakuona kitu kijiinua,bali alikuwa si wa kiburi na akapendwa na watu wa rika mbali mbali na hatimaye jinsi mbali mbali. Jifunze hapo!!!

Sio unapata smart phone ya teckno tu,basi mabega juu,!!! nzuri

io umepewa kuhubiri kidogo tu,basi mabega juu kujiona wewe ndio pekee!!!! Weeeh acha,Mungu ana watu wake wewe,. Jifunze katika kushuka,acha watu wakuelezee sifa lakini sio wewe,kumbuka wakusifiwa na kuinuliwa ni Mungu pekee – ZAB.48:1.

  1. Jihoji maswali haya,wewe mwenyewe sasa hivi;

Je kuna sababu gani ujiinue? Je kuna umuhimu gani wa kuyaeleza mambo ya kwako pasipo kuulizwa? Je utapata faida gani hasa ukijisifu nakujiona u bora? Kwa nini usiseme ukweli tu ?kwa nini umekosa mipaka katika semi zako? N.K

Kila anayejikweza atashushwa,na anayejishusha atakwezwa.( Luka 18:9-14)

Ukijishusha ukanyenyekea na kutii ujue utainuliwa na Mungu. Lakini ukijitahidi kujiinua,ujue utashushwa tu. Sasa nalisema hili kwako wewe unayesoma hapa,ili ujue kama unataka kupandishwa na Mungu, anza leo kushuka kwa unyenyekevu,kubali kujifunza kwa wengine, acha mambo ya sifa kujielezea wewe tu n.k,na hapo utaona namna ambavyo Mungu atakavyokuinua. Fanyia kazi hilo.

Ikiwa fundisho hili limekubariki na umejifunza kitu,basi nifahamishe kupitia namba zangu + 255 655 111 149 / 683 877 900 / 762 414 446.

WhatsApp ni +255 655 111 149.

Mch. G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page