top of page

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~sehemu ya mwisho.

Bwana Yesu asifiwe…


Mch.Madumla

Na Mchungaji Madumla.


Karibu tuendelee.,

08.NI KWA NAMNA GANI KARAMA YANGU ITAMPENDEZA MUNGU?

Kabla ya kujibu swali hilo,ebu tujiulize kwanza nini maana halisi ya kumpendeza Mungu? Au Je mwanadamu chini ya jua anaweza kumpendeza Mungu wake aliyemuumba?

Neno hili “kumpendeza Mungu” maana yake ni kuishi katika mapenzi ya Mungu. Mfano wa kawaida kabisa,ukiwa na mtoto anayeishi nyumbani kwako akiyafanya yale yote unayomuagiza kufanya basi ni dhahili mtoto huyo atakupendeza wewe. Hivyo basi,kumpendeza MUNGU ni kufanya yale yote atakayo Mungu ufanye,mfano; kuzishika amri zake,“ Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.”1 Yoh.5:3

Basi hapo utakuwa mmoja umpendaye,na ukimpenda Mungu Naye atakupenda,imeandikwa pia;“ Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye;...”Yoh.14:21

Kwa habari ya karama ni vivyo hivyo kwamba karama yoyote ile itakayofanya kazi katika mapenzi ya Mungu Baba,basi ni dhahili kabisa karama hiyo itampendeza Mungu. Hivyo basi,mtu anaweza akampendeza Mungu wake kwa maisha matakatifu anayoyaishi.

Mfano ukiwa na karama ya uponyaji,kisha ukashuka mno,ukawa mnyenyekevu ukitambua kwamba yule aponyaye si wewe bali ni Mungu. Basi,karama yako itaongezeka na kumpendeza Mungu wako. Mfano tena;Ukiwa una karama ya unabii,kwamba Mungu anakutumia mno,papo hapo ukaendelea kushuka mbele zake na kuhitaji msaada wake Mungu kila mara huku ukionesha kwamba bila Yeye BWANA wewe huwezi chochote kile(Yoh.15:5),kwa kufanya hivyo basi ni ukweli kwamba karama yako ya unabii itakuwa na itampendeza Mungu. N.K

Shida iliyopo leo ni kwamba; watu wengi wenye karama wanajisahau na kuona kana kwamba yote wayafanyayo wanafanya wao wenyewe pasipo msaada wa Mungu. Utakuta mtumishi mwenye karama ya uponyaji anajitamba kwamba yeye ndio kila kitu,tena eti yeye ndio anayeponya na kufungua watu. Mtu huyu amesahau kwamba yeye si kitu bali Mungu pekee ndio aponyaye,kwa namna hii ya kujiinua ni makosa!!! Karama za watu wa namna hii,siku zote hazimpi Mungu utukufu tena haziwezi kumpendeza MUNGU.

Kumbuka;

Mwenye karama akijiinua,hawezi kuwa kipenzi cha Mungu. Tabia ya kujiinua ni tabia ya kiburi,na tabia hii ya kiburi ni tabia ya shetani. Kinachoua karama za watu wengi ni kujiinua.

09.CHANGAMOTO ZA UTENDAJI KAZI WA KILA KARAMA.

Kila karama ina changamoto yake namna vile inavyotumika. Changamoto hizi sio matatizo,wala shida bali ni aina ya majaribu au mapito. Zipo changamoto zinazoonekana katika kila kalama ambazo tunakumbana nazo. Nazo ni kama ifuatavyo;

(i) Kuvamiwa na wasiokuwa na karama halisi.

Leo imefika wakati mtu unashindwa hata kutofautisha kati ya nabii wa kweli na nabii wa uongo,kwa sababu manabii wamekuwa wengi mno,wengine wanatushangaza kwa unabii wao.kutofautisha kati ya mwenye karama ya kuponya na anayeigiza~yaani kuna mvulugano mkubwa sana. Lakini ukweli siku zote utabaki kuwa ukweli na hata siku moja haiwezekani ukweli ukawa ni uongo bali ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukiwa rohoni utaweza kutambua wapi kuna ukweli na wapi kuna uongo.

(ii) Ukosekanaji wa pesa za kuendeshea huduma ndani ya wale wenye karama.

Mara nyingi pesa hutumika ili kufikisha injili vijijini na hata uendeshaji wa injili huku mjini,pesa inahitajika mno. Mfano ili watu wengi zaidi waweze kumsikia mnenaji mwenye karama basi ni dhahili atahitaji chombo kitakachopeleka mawimbi ya sauti mbali zaidi,mfano mnenaji akiwa kwenye jukwaa atahitaji kipaza sauti na spika zenye nguvu ili ujumbe kwa njia ya sauti yake ufiki kwa wengi zaidi.

Pia,mnenaji  atahitaji atumie radio wakati mwingine ili aweze kusikika mbali zaidi. Vyombo hivi vyote vinahitaji pesa. Sasa si watumishi wote wanapesa ya kulipia gharama za injili,na hili kubakia changamoto.

Leo gharama za huduma zimekuwa kubwa mno,na hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya watumishi wa Mungu. Lakini hata hivyo,injili ni lazima ihubiriwe kwa gharama yoyote ile.

(iii) Kutothamini karama za wengine.

Hii bado ni changamoto kubwa ndani ya kanisa la leo kwa wale wenye karama. Watu wengi leo wenye karama wanakumbwa na changamoto hii kwamba hawapewi nafasi ya kutumika sawa sawa na karama iliyopo ndani yao. Mwishowe wanajikuta wakidumaa na karama zao,wengine karama zao hufifia,wengine zinawaponyoka na kujikuta wakiwa watupu tena kukosa kufanya lolote lile. Kumbuka; chombo kisichotumika,uchafu ni sehemu yake tena ushika kutu

~ Mfano;utakuta mwamini akawa na karama ya ualimu lakini kanisa lake halimpi nafasi ya kufundisha eti kwa sababu kanisa limekaa katika misingi ya unabii,kwa hiyo unabii unachukuliwa kuwa ndio kila kitu, hivyo basi mwenye karama ujikuta anapoteza karama yake. Sasa,hii inakuwa ni changamoto kubwa sana.

(iii) Kukosa muda wa maombi na neno la Mungu.

~ Hii pia ni changamoto kubwa kwa wenye karama kukosa muda wa maombi na muda wa kusoma neno la Mungu na kutafakari kwa sababu ya kutingwa na shughuli nyingi za kidunia.

Madhara yake makubwa ya changamoto hii ni kuduma kwa karama. Yaani karama inakuwa haina nguvu za MUNGU. Mfano utakuta mtu ana karama ya imani,mtu huyu kabla ya kuanza kazi alikuwa ni mwombaji na msomaji biblia mzuri lakini alipopata kazi (hasa ile ya kuajiliwa) akajikuta muda wake mwingi unabanwa na muajiri. Hivyo karama yake inapata changamito ya kukosa muda na Mungu.

Changamoto hizo ni chache kati ya nyingi zilizokuwepo kwa wenye karama. Sijajua wewe unapitia katika changamoto gani? Nataka niombe na wewe mpendwa kwa habari ya karama yako. Piga namba yangu ipo hapo chini;

Kwa huduma ya maombezi,tafadhali usisite kunipigia sasa +255 683 877 900.

What’s app number ni +255 746 446 446

Na Mch. Madumla Gasper

UBARIKIWE.

Comentários


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page