top of page

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~07


  1. Karama ya miujiza / Matendo ya miujiza (1Wakorintho 12:10)

Karama ya miujiza ni kazi ya Roho mtakatifu yenye kueleza uwepo wa nguvu za Mungu kwa watoto wake. Hii ni karama muhimu sana inayowaleta wengi kwa Yesu hata wale wasioamini wakiona ishara,ajabu na miujiza gafla wanaamini. Roho mtakatifu akiwa kazini miujiza mingi isiyoelezeka ni lazima itokee.

Lakini pamoja na hayo, Matendo ya miujiza ni karama itolewayo na Roho mwenyewe kwa watu wake,si wote bali watu fulani kama apendavyo Yeye. Kuna miujiza inayofanyika na watu wasiokuwa na karama hii isipokuwa mahusiano yao na Bwana yamekaa vizuri,hivyo miujiza hutokea moja kwa moja. Lakini kuna wale ambao hakika wamekirimiwa karama hii ya matendo ya miujiza 

Biblia imefulika ishara, ajabu na miujiza kuanzia vitabu vya agano la kale mpaka agano jipya. Lakini miujiza yote ilikuwa ikifanywa na Roho mtakatifu mwenyewe. Karama hii hutegemea sana kiwango cha Neno la Mungu ndani ya mwenye karama. Kwa maana Bwana hulithibitisha “Neno lake” Kwa ishara ( Marko16:20)

Kwa kuwa hii ni karama kwa ajili ya kuujenga  mwili wa Kristo basi aliyepewa karama ya namna hii anapaswa afahamu kwamba karama inamwinua Yesu / inamtangaza Yesu Kristo mpaji wa karama. Ikiwa aliyepewa akishindwa kufanya hivyo,basi ni lazima Roho mtakatifu atamwacha na hatimaye atajikuta akiongozwa na roho chafu katika miujiza yake huku aweza kuwadanganya watu kwamba bado yupo na Roho mtakatifu, kumbe alishamwacha peke yake. Hapo ndio kile tunachokisikia kwamba nabii fulani ni nabii fake…

ITAENDELEA…

Kwa msaada zaidi +255 683 877 900. What’s app number +255 746 446 446

Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

Commentaires


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page