KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~06.
- Mch. Gasper Madumla
- Feb 1, 2016
- 2 min read

Karama ya neno la hekima ( 1 Wakorintho 12:8,Matendo 6:10)
Moyo wa adili wa kupambanua mema na mabaya huitwa “hekima” Au ufunuo wa neno la Mungu kwa watu sahihi,kwa muda na wakati sahihi huitwa “hekima” . Tunapozungumzia kuhusu “neno la hekima” tuna maana ya ufunuo maalumu wa Neno la Mungu kwa ajili ya kutatua shida fulani kwa haraka. Mfano mzuri ni pale shida ya mitazamo ilipotokea katika mafundisho huko Yerusalemu kwa maana kuna watu walifundisha kuhusu kuokoka ni lazima kutairiwa kwanza,
Lakini Paulo na Barnaba wakashindana na watu hawa,mwishoe wakaamua Paulo na Barnaba wapande kwenye balaza la Yerusalemu kuuliza kuhusu jambo hilo. Utatuzi wa mgogoro huu ulihitaji “neno la hekima “ yaani ufunuo wa neno la Mungu kwa wakati huo. Ndipo Yakobo akaachilia neno la hekima na kesi ikaishia hapo (Matendo 15:13-22). Hivyo Neno la hekima linafanya kazi hasa pale ambapo njia ya kawaida imekosekana,hapo unahitaji ufunuo wa neno ili utoke hapo.
Karama ya neno la maarifa ( 1 Wakorintho 12:8)
Neno la Mungu ni kweli yote tunayohitaji. Hivyo karama ya neno la maarifa ni aina ya maarifa unayoyahitaji katika Neno. Mfano Neno linasema Bwana atakulinda uingiapo na utokapo,Sasa ni maarifa gani uliyonayo katika Neno hilo hata liwe halisi kwako?Angalia mfano wa pili huu; Yesu alipodaiwa kodi ya hekalu ya nusu shekeli kule Kapernaumu.
Pesa haukuwepo kwa wanafunzi wake muda ule lakini Yeye mwenyewe Yesu alikuwa na “maarifa” ya kuipata hiyo pesa,bali wanafunzi wake hawakuwa na maarifa. Kwa Neno la maarifa akamwambia Petro aende akavue samaki,yule azukaye kwanza anapesa ndani yake, Petro akafanya hivyo na hatimaye maarifa ya Yesu yakawasaidia kulipa kodi ya nusu shekeli.
ITAENDELEA…
Kwa msaada zaidi mawasiliano ;+255 683 877 900What’s app number ni +255 746 446 446
Mch.G.Madumla
UBARIKIWE.
Comments