KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~05
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 25, 2016
- 1 min read

Karama ya uponyaji.
Kawaida uponyaji ni kazi ya Mungu mwenyewe. Mungu amewainua watu wake na kuweka uwezo huo wa kuwafungua waliofungwa na nguvu za giza,kuwaponya magonjwa yote na maradhi mbali mbali n.k Uwezo huu huitwa “karama ya uponyaji ” Yesu ndiye mwenye karama hii ni wa kwanza ,pia aliipitisha kwa mitume wake(Luka 9:1)
Moja ya eneo ambalo Roho mtakatifu anajidhihilisha ni katika uponyaji unayopitia katika watumishi wake pale wawekapo mikono yao kwa wagonjwa na wadhaifu,gafla uponyaji ujitokeza (Marko16:18). Kwa mgonjwa kuwa na Imani ni kitu muhimu sana lakini “karama ya uponyaji “ haizuiliwi na imani ya mgonjwa,kwa maana mgonjwa anaweza akawa aamini lakini hapo hapo akaponywa na Mungu kupitia mtumishi wake ( Matendo 3:1-9). Kazi ya uponyaji inaeleza uwepo wa Mungu asiyeshindwa
Kwenye kanisa,kuna watu ambao Mungu amewainua kwa kazi hiyo tu. Lakini bahati mbaya watu walioinuliwa wengi wamejisahau kwa kushindwa kumpa Mungu utukufu kwa maana wakidhani ni wao ndio wanaoponya kumbe ni Mungu isipokuwa wao wanatumiwa tu kama vyombo vya Bwana. Na wengine badala ya kuendeleza kitu hiki kizuri walichopewa, utakuta wanaacha na kwenda kugombea madhabahu ya kuimba au kufundisha hali wao sio walimu wala sio waimbaji kwa maana wao wamepewa uponyaji tu ( ingawa wanaweza kuponya kwa neno tu, lakini inafaa kufikiri mara mbili juu ya karama gani aliyokupa Bwana)
Kumbuka ;
Karama ya uponyaji inafanya kazi na wanyenyekevu,watu ambao wenye kusikia zaidi maelekezo ya Mungu kuliko ya mwanadamu. Lakini pia kwa wale ambao wana mahusiano mazuri na Mungu,watu wa namna hii kama watakirimiwa karama na Roho mtakatifu basi hakika karama itafanya kazi yake ipasavyo…
ITAENDELEA…
Kwa msaada zaidi +255 683 877 900. What’s app +255 746 446 446.
Na Mch. G. Madumla
UBARIKIWE
Comments