top of page

KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~04.


  1. Karama ya maongozi na usimamizi / uongozi ( Warumi 12:8)

Kuna aina mbali mbali za uongozi. Lakini kuna aina kubwa mbili za uongozi;

  1. Uongozi wa kusomea

  2. Uongozi wa kuzaliwa nao.

Katika uongozi wa kuzaliwa nao kuna namna ambavyo Roho mtakatifu anafanya kwa mtu ambaye ndani yake kuna uongozi na hajasoma popote. Mtu wa namna hii anapokuja kwa Kristo/ anapookoka, uongozi wake unatiwa nguvu mara mbili. Pia kuna uongozi ambao mtu hakuzaliwa nao wala hakusoma, lakini baada tu ya kumpokea Yesu Kristo,gafla anajikuta akitumika katika kuongoza watu hata watu wengine wanaomjua wanaulizana ;

“je huyu si fulani? Amepata wapi haya maneno yenye nguvu ya kuwaongoza watu wazima namna hii?” Hata yeye mwenye kuongoza wanapomuuliza,hajui nini kimetokea bali anajikuta tu,watu wanamkubali na kusikia ayasemayo, hatimaye anakuwa kiongozi 

Biblia inawataja viongozi,watu wenye karama hii. Ukimwacha Yesu ambaye hakuna kiongozi mzuri kama yeye, lakini mwangalie mtu kama Gideon aliyechaguliwa na Mungu ,mtu kama Musa,mtu kama Yoshua nk. Hawa wote hawakusoma shule za uongozi lakini kazi yao inaonekana hakika.

Biblia inasema “mwenye kusimamia kwa bidii ” Hivi unajua uongozi mzuri ni dawa ? Kuna watu ambao wala hawahitaji kuombewa Bali wakikutana na mtu mwenye karama ya uongozi wanapokea kabla ya kuombewa au kushauriwa. Hujawahi kumwona kiongozi fulani ambaye akiongoza hata wewe mwenyewe unafarijika na kupata amani moyoni? Unajua kuna watu ambao wakiwa viongozi watu wa chini wanafuraha na kuwa huru. Hali ya namna hii, inaonesha nini kiongozi amebeba kwa ajili ya kundi lake.

Karama hii inaonya pale panapotakiwa kuonya,inakemea mahali pa kukemea, lakini pia karama ya maongozi imebeba maelekezo sahihi. Karama hii imetolewa kwa kusudi kundi la Mungu / kanisa liweze kuongozwa vyema ipasavyo. Kumbuka si wote wamepewa karama hii, hivyo ni vyema kuwaachia wale waliopewa karama hii waongoze kundi. Na wengine inapasa kukubali kuongozwa na wenye karama…

ITAENDELEA…

Kwa mawasiliano + 255 683 877 900.

What’s app +255 746 446 446.

Na Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page