KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~02
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 9, 2016
- 2 min read

Karama ya kukirimu / Mfariji ( Warumi 12:8)
Roho mtakatifu yeye mwenyewe ndio mfariji na mtia moyo wa kwanza. Hivyo,kuna watu ambao wamekirimiwa moyo wa kukirimu,moyo wa kufariji ingawa wao si wachungaji wala si wazee wa kanisa,basi tu – Kwa uaminifu wao mbele za Bwana wamejikuta wana moyo mkubwa wa huruma,moyo wa upendo,moyo wa kujali . Kazi hii ni kubwa na sio kazi ya kiongozi wa kanisa ikiwa kama hakupewa na Bwana uwezo huu,kamwe hataweza kuachilia faraja inayohitajika.
Neno “Kukirimu ” ni hali ya kumkaribisha mtu,Tena kumpokea mtu vile alivyo kwa upendo. Ni tendo la kujali hali mtu mara nyingi karama hii huambatana na hali ya “kufariji” ndio maana huitwa karama ya kukirimu au karama ya kufariji. Uwezo wa kiroho wa namna hii tumeanza kuona kwenye kanisa la kwanza huko Jerusalem na kule Antiokia ( Matendo 6:3).
Kwa sababu ya kuwepo Kwa karama hii,basi kanisa likaongezeka. Unajua watu hukimbilia kanisani kama sehemu ya kutua mizigo yao kwa maana wameumiza na kuumizwa huko nje. Sasa wanapokimbilia kanisani wanategemea kuonana sio na mchungaji au nabii,bali kuonana na watu wenye moyo wa kufariji.
Hivyo,wakikutana na watia moyo,watu wenye kukirimu basi hapo uwe na uhakika watu hao waliokimbilia kanisani watabakia kanisani na hatimaye watakuwa washirika. Siri ya ukuaji wa kanisa au fellowship yoyote ile hutegemea karama hii ya “ukarimu”. Ebu fikiria hivi; ikiwa mtu mmoja ameingia kanisani kwa mara ya kwanza halafu akakosa mtu wa kumjali,hivi huyo ataendelea kuja hapo kweli?
Au fikiria kwamba Binti aliyetoka bar,kaja na nguo fupi akiwa hajitambui halafu anakutana na mtu anayemkemea kuhusu uvaaji wake,hivi huyo binti si ataondoka zake,arudi kwenye bar? Kumbe ilihitajika watu wenye karama ya ukarimu na kutia moyo,wamfunike aibu yake,na kumleta taratibu kwa Kristo kwa kumwonesha upendo kwamba Kristo amekuja kwa watu kama hao,kisha yakifanyika hayo binti aliyetoka dhambini hakika atabaki.
ITAENDELEA…
Kwa msaada zaidi+255 683 877 900
What’s app number ni +255 746 446 446
Na Mch.G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários