KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU~01.
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 6, 2016
- 2 min read

Karama ni uwezo wa kiroho wa utendaji kazi wa Roho mtakatifu ndani ya mwamini katika Kristo / aliyeokoka. Neno “karama” ni tofauti na Neno “ kipaji” Kwa maana kipaji ni uwezo wa kimwili ambao mtu huzaliwa nao bali karama ni uwezo wa kiroho apatao mtu hasa baada ya kuokoka.
Tena kusudi la kipaji ni kumpatia mtu mkate/mahitaji ya kiuchumi bali karama ni kwa ajili ya kudhihilisha uwepo wa Roho mtakatifu katika uzima na uponyaji. Hivyo kila aliyeokoka “ana karama “ ndani yake kwa kufaidiana na mtu mwingine. Kwa mujibu wa biblia,kuna aina mbali mbali za karama za Roho pia kuna huduma za Roho mtakatifu,yaani;
Huduma 5 za Roho mtakatifu ( Waefeso 4:11)
Karama za Roho mtakatifu
Roho mtakatifu ndiye mwenye kumiliki karama zote naye ndiye mpaji wa karama. Kumbuka,kuna tofauti za karama Bali Roho ni yeye yule,tena kuna tofauti za kiutendaji wa kazi kwa kila karama lakini Roho ni yule yule mmoja ( 1 Wakorintho 12:4-6). Kama Roho ni mmoja mwenye kutoa karama mbali mbali basi ni dhahiri kwamba“hakuna karama kubwa na karama ndogo” kwa karama zote zinaendeshwa na mmoja, Roho mtakatifu.
Karama za Roho mtakatifu;
Karama ya masaidiano / msaidizi ( 1 Wakorintho 12:28)
Hii ndio karama ya kwanza ya Roho mtakatifu. Roho mtakatifu huwainua baadhi ya watu maalumu na “ kuwapa roho ya usaidizi “ ili kusudi kazi ya Bwana ikamilishwe. Kwa maana kazi yoyote ya Bwana haiwezekani kukamilika kama hakuna wenye karama ya masaidiano. Angalia mfano huu, Mungu alimwinulia Musa watu ambao ndani yao akawapa karama ya masaidiano.
Ambao walimsaidia kazi kwa moyo mmoja hatimaye wakabeba pamoja mzigo wa Musa ( Kutoka 18:24-27). Haikuwa tu hali ya kuwateua watu bali ilikuwa kuhusu “karama ya usaidizi “ ambayo iliwafanya waliopewa karama wakapenda kujitoa. Katika huduma ni lazima watu wapewe karama hii ili kumsaidia kazi mchungaji kiongozi bila kulalamika. Ni kazi ya kiongozi/mchungaji kumwomba Mungu kuhusu karama hii ya kwanza ili Bwana awainue watu watakaobeba mzigo wake pamoja kwa moyo wote.
ITAENDELEA…
Kwa huduma ya maombezi tafadhali usisite kunipigia simu yangu hii;+255 683 877 900
What’s app number ni+255 746 446 446
Na.Mch.Gasper Madumla.
UBARIKIWE.
Comentários