KANISA ( THE CHURCH) ~ 01
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 14, 2019
- 4 min read

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Je kanisa ni muhimu?
Ebu fikiria swali hili; Je wakristo wanaweza kuwepo bila kanisa.? Au Je watu wanaweza kumwomba Mungu binafsi bila kanisa? Ukiyatafakari maswali haya, utagundua ni maswali muhimu sana kwa maana hapo zamani kabla ya kanisa la mitume hakukuwa na kanisa lakini watu waliendelea na taratibu zao za kuomba kama kawaida. Lakini hali ya maisha ya leo, nini hasa umuhimu wa uwepo wa kanisa? Sijui kama umeshawahi kujiuliza swali hili. Yafuatayo ni maswali yanayoweza kuulizwa mara nyingi kuhusu kanisa;
“ Kwa nini kuna makanisa mengi? Kwa nini makanisa hayapo kitu kimoja hali yote ni makanisa ya Kikristo? Je nani amekosea kanisa lako ulilopo au kanisa lingine hata mkatofautiana,? Lipi kanisa la kweli? N. K”
Maswali hayo mtu anaweza kujiuliza. Lakini ni vyema tukaanza na kujua kanisa ni nini haswa?
Kanisa ni nini hasa?
Kuna njia nyingi za kujibu swali hili, kwa sababu biblia imetupa maana mbali mbali ya kanisa. Lakini nataka nikupe maana ambayo labda hukuwahi kuisikia kabisa kuhusu kanisa. Kwanza kabisa ufahamu tunapozungumzia kanisa tunalenga mambo haya mawili “Kanisa linaloonekana / the visible church ” na “kanisa lisiloonekana / The invisible church “
01.Kanisa linaloonekana / visible church.
Hili ndilo kanisa ambalo watu wote wa duniani /wamataifa wanaloweza kuliona. Ambapo kanisa la namna hii, linahusisha vitu kama “wachungaji, watu/washirika, majengo, madhehebu, mali22-23. . Kanisa la namna hii, halina hasa mausiano ya karibu na Kristo kama jiwe kuu la pembeni.
02.Kanisa lisiloonekana / the invisible church.
Hili ndilo kanisa ambalo halitegemei majengo hili liwe kanisa bali ni wale wote waliookoka na ni waamini wa kweli Katika Kristo. Kitu cha muhimu kutofautisha ni hilo kanisa la kwanza ni kwamba, waamini hawa wa kanisa lisiloonekana , Mungu hukaa ndani yao ( Yoh. 14:23). Watu ambao wanaushirika wa moja kwa moja na Kristo na Mungu Baba. Watu hawa huiwatwa kanisa lisiloonekana kwa maana kitu mali, majengo hakiwasumbui.
Kwa tafsiri nyingi tulizonazo kuhusu neno “kanisa” kama tulivyoandika hapo awali. Sina haja ya kuzirudia ila tafsiri hii, nikupayo leo ni tasfiri mama na fupi. “Kanisa ni mwili wa Kristo “- Waefeso 1:22-23. Kumbuka, ikiwa kanisa ni mwili wa Kristo itakuwa na maana Kristo Yeye mwenyewe ndiye kichwa na waamini tunatengeneza mwili. Kristo akiwa ni kichwa ina maana Yeye ndiye mtawala na mwenye mamlaka juu ya kanisa lake. Ujue kwamba, kila kitu ambacho mwili hufanya hutegemea kichwa na ndivyo lilivyo na kanisa ambalo hutegemea Kristo kwa kila kitu. Hii inatupa picha kwamba kama mwili utatengwa na kichwa basi ni dhahili utaangamia.
cha kanisa, (hivyo kanisa sio la mtu yeyote bali ni mali ya Kristo) hii ina maana pia hata kama waamini au mwamini ni mtenda dhambi bado kanisa li takatifu kwa sababu ni mwili wa Kristo ambao ni mtakatifu siku zote. Dhambi ya mtu huyo itashughulikiwa kama mtu aliyetenda dhambi, lakini kanisa litabakia takatifu siku zote.
Mambo manne muhimu wa kufahamu kanisa ;
Umoja / one.
Utakatifu / Holy.
Pamoja / Universal.
Utume / apostolic.
01.Umoja /One.
Tunaposema kanisa la Kristo ni moja tunamaana ya Umoja wa kiungu / God’s unity. Wakristo wanapaswa wawe kitu kimoja / Christians are supposed to be united together as one. Hii haina maana ya kwamba tusiwe na madhehebu mbali mbali tuliyonayo leo, lakini humaanisha katika madhehebu yetu lazima tuwe kitu kimoja kwa maana tu mwili wa kichwa kimoja yaani Kristo ( Matendo 4:32)
02. Utakatifu / Holy.
Kwa kifupi, kuwa mtakatifu kuna maana kubwa mbili “Kutakasika / being pure na kutengwa kwa kazi ya Mungu/ being set apart for God”. Tonapoliona kanisa takatifu, tunaiona picha ya Kristo ambaye ni mtakatifu. Ni vyema ufahamu kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya kanisa, ili kanisa liwe safi / takatifu ( Waefeso 5:25-27)
03. Pamoja / Universal.
Kuwa pamoja ni tofauti na kuwa wamoja. Kwa maana unaweza ukawa na mtu pamoja lakini usiwe naye na umoja. Hii ina maana yeye uliyekuwa naye pamoja ni yule uliyopo naye sasa, ukiulizwa upo na nani hapo. Bila shaka utajibu ;nipo pamoja na fulani. Lakini suala la umoja ni pale nia zenu zi na umoja? Mnania mamoja? . sasa “pamoja /universal” ina maana wakristo wote wanapaswa kuwa na hali ya upamoja ulimwenguni mwote. Kwa mfano;ukienda china leo na kukutana na jamii ya kiKristo ya china, unapaswa uwe pamoja nao pasipo kutengwa kidhehebu, wewe uwapokee jinsi walivyo na wao wakupokee jinsi ulivyo, kisha mketi pamoja.
04.Utume / Apostolic.
Tunaposema “utume” tuna maana ya kanisa lijengwe kwenye msingi ya kazi na mafundisho ya mitume. Ambao hao mitume wamesimama kwenye neno la Mungu ( mitume ni wale waliokuwa wanafunzi wa Yesu, pamoja na Paulo, misingi iliyowekwa na Yesu)
Kumbuka;
Kanisa lolote likitafsiri kinyume na maana halisi ya maneno hayo, basi kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa kinyume na kanisa la Bwana. Kanisa la Bwana ni kundi la waaminio / waliookoka katika Kristo na si vinginevyo. Dhana ya kanisa kama jengo la kuabudiwa siyo tafsiri sahihi ya kanisa kiroho, ingawa wengi tunajua kanisa kama jengo fulani.
Je nini kusudi la kanisa / the purpose of the church.
Kwa ujumla wake, kanisa la Kristo linakusudi moja kubwa ambayo ni “kuwafanya waamini kumpenda Mungu na kupendana wao wenyewe” Hata hivyo tunaweza kulivunja vunja kusudi hili katika makusudi madogo madogo kama vile.
01.Uhusiano wetu kwa Mungu ( Wakolosai 3:16,Marko 12:30)
Kumwabudu Mungu katika Roho na kweli.
Kujiunganisha na Mungu kwa njia ya maombi.
02.Uhusiano wetu kwa waamini wengine ( Wakolosai 1:28,Marko 12:31)
Kufundisha na kuhubiri Neno.
Kutii Neno na kuliishi.
Kutia moyo ukuaji katika jamii.
03.Uhusiano wetu kwa wamataifa/ kwa watu wote.
Kuonesha/kumulikia Nuru ya Bwana kwa mataifa.
Kuinjilisha / uinjilisti.
Kuwahurumia mataifa/ kuwasaidia katika hali ya huruma na neema.
Mambo hayo nane, kila moja ni mtaji wa somo linalojitegemea. Ikiwa u mwalimu waweza kuanza kupanua wigo katika mambo hayo pamoja na vipengele vyote vya fundisho hili zuri, na hatimaye kupata masomo mengi ya kuwafundisha watu wako kwenye kanisa. Jambo moja la kukumbuka, ni hili “uwaambie watu wako kwamba, hilo sio kanisa la mchungaji bali ni kanisa la Kristo” kwa maana wengi hukosea na kuona makanisa waliyonayo ni yao kumbe kanisa ni mali ya Kristo.
ITAENDELEA…
Ikiwa kama umefaidi/umepata kitu hapa, naomba unifahamishe. Kwa huduma ya maombi pia piga namba hizi hizi ; +255 683 877 900.
What’s app namba ni .+255 746 446 446
Na Mch. G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comments