JINSI VIJANA WASIVYOJUA THAMANI YA MUDA!
- Mch. Gasper Madumla
- Sep 19, 2017
- 5 min read
*LIFE BEGINS AT 40…. HOW OLD ARE YOU?*

Mwl.Andrea G.Muhozya
Life Begins at 40.. Huo ni msemo wanao waingereza wakimaanisha maisha yako ijapokuwa yanaanza toka milele iliyopita na toka umeumbwa au toka umefika duniani na toka umeanza kukua nk nk lakini bana maisha #halisi yataanza rasmi siku ukitimiza miaka 40.
Hapo kama bado nauli ya daladala ni ishu, ada, chakula, kodi ya nyumba, nk basi ndo utaanza kuelewa maana ya muda uliokuwa unatumia Facebook kulike picha za ajabu na story zisizokupeleka popote. Nadhani unanielewa sasa hasa wewe ambaye unahisi umri wako bado ni mdogo kwa hiyo bado bado kidogo muda wa kuwa serious na maisha haujafika. Sikia kijana mwenzangu..TODAY is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.
Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.
Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international school nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!
Hapo ndo unawaza kufuga ng’ombe wa maziwa Kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bizness in Australia. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 800M! Wamejenga mjengo wa ukweli. Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda Dubai wanafikiri Atlantis, wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala mara mwendokasi mara washuke warudi nyuma kidogo kwa miguu ndo wapuyange kwa miguu kwenda shule. Na kurudi hivyo hivyo.
Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini mzazi anahitaji support kidogo una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watajua! Halafu unashangaa wenzako wanazidi kuinuliwa. Unaanza kuwaita Freemason. Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho….. (Malizia). Wakati wenzako walikuwa wanajenga maisha wewe ulikuwa unashinda Facebook kuongelea UKUTA uwepo au usiwepo, ikaisha ukaja Lissu kiboko au anaboa, ukadakia Makonda ni Bashite au Gwajima ni muongo.. Hebu fikiria kidogo. Yoote hayo yamekufikisha wapi?
Sijui kuvunja viti uwanja wa taifa mara saivi sijui fuvu la kichwa. Nape Nauye. Mara Makinikia. Haya mara Harmonize na Harmorapa je? Wema Sepetu aache siasa au la. Alikiba na Diamond nani kapatia. Mara dereva wa lissu yuko wapi? Vitu hivi vinawezaje kuwa sehemu ya muda wa mtu ambaye yuko serious na maisha yake? Gwajima uliyemjadili amekufikisha wapi. Ruge na Makonda umefika nao wapi? Mara ujadili sijui Zari ana umri gani. Can you imagine??? Yaani hicho ndo kichwa cha kijana wa kitanzania. Ukimwambia vitu vya maana anasema hana muda. Lol!! Mwingine anatukana!
Katika kipindi hiki ambacho watu wengi hasa vijana wanashinda wakitukanana mitandaoni humu nimejifunza mambo mengi kwa watu kama Mo Dewji na wengine kama Patrick Ngowi na vijana wengine waliopiga hatua sana. Ninejifunza kwao ku maintain FOCUS kwenye mambo ya msingi hasa yanayohusiana na ndoto zangu na maono. Hivi Dewji anawaza kama wewe unayewaza nani kampiga risasi nani? Hujui kuna watu mpaka leo wanabishania nani alimpiga risasi Karume au John F Kennedy? Siku zinaenda.
Halafu usipofanikiwa unalaumu serikali oh wazazi oh sina connection. Connection wakati akili yako inawaza ubishani tu day in day out? Huzuiliwi kubishana lakini jiulize are you making any progress out of it? Au wasiojadili sana hayo mambo ndo hawana roho nzuri? Hivi kwa kuwa Bakhressa hajasema chochote basi ndo hana roho nzuri kama wewe? Is that so? Wewe ndo KIPIMO cha roho nzuri? Yani kwa kuwa Mengi hajatweet basi ana roho mbaya ila wewe ndo una roho nzuri? Kweli? Unasahau haya mambo hayaishi. Na unasahau una MAISHA yako yanakungoja!
Wenzako mkifika miaka 40 watu wa rika lako wana exposure ya uhakika. Wewe at 40 bado umeajiriwa na mchana unakula kwa mama lishe chakula hata virutubisho hakina. Wenzako at 40 washaacha ajira siku nyingi washatembea dunia na kujifunza maisha kutoka kila mahali.Wewe umeajiriwa unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30yrs ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect. Kisa ulikuwa unafatilia Zitto Kabwe na Job Ndugai. Hao unaowafatilia wako ndani ya kazi zao kwa hiyo muda wao unatumikia shughuli zao wakati wewe utatumia muda wako na pesa yako kuwafatilia. Jenga nidhamu mpya ya kulinda muda wako sasa.
Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime. Kisa? Ulikuwa unatumia muda wote kuangalia vitu vya kuchekesha chekesha na kuongelea mambo ya siasa sijui wasanii sijui msanii gani ana hela nyingi sijui nani kafulia sijui nani ana mimba.. Mara umedandia uchaguzi Kenya mara umerudi Acacia mara unajadili Arsenal sijui Manchester. Eti unatoa maoni? Seriously? Maoni wakati hali yako ya kipato haijaimarika?
😡
😠
😠.
Hivi vitu vinaiba muda wako sana ndugu zangu. Mimi mwenyewe nilikuwa hivyo lakini nikastuka mapema sana! Utashangaa umri unaenda bila kupiga hatua. Umri wako ni kila sekunde na kila dakika na kila saa. Ndo umri huo. Umri siyo mwaka kwa mwaka. Ni sekunde na dakika. Ndo maana matajiri wanalinda muda wao kwa wivu mkali. Coz TIME IS MONEY. Utashangaa unapoteza muda afu unafika 40 years ndo unawaza uanzie wapi. Mungu siyo mjinga kukupa umri huu wa ujana. Hajakupa uuchezee chezee tu. Be careful my friend. Time flies.
Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You? So kama wewe unasema “Mimi bado mdogo..” endelea tu kupoteza muda wako utakumbuka tu siku moja but it might be too late. Unakuta mtu ameajiriwa au amejiajiri miaka inaenda hajui kwa nini hapigi hatua kipato hakikui lakini yupo tu hatafuti maarifa ya jinsi gani ya kutumia muda wake wa ziada kutengeneza kipato hata mara mbili ya mshahara wake. Wengine wanafanya hivyo na wanapiga hatua kubwa hadi wengine wanafikiria sasa kuachana na ajira. Ni muhimu kujifunza haya mambo. Siasa hazitaisha. Angalia your life.
Ukifika 40 years uwe very established. Bila hivyo utashangaa kweli. Wakati wenzako wachache wa rika lako mtakapofika miaka 40 wakati wenzako unasikia amenunua kiwanja Kurasini kwa sh Bilioni mbili kwa ajili ya *kupaki* tu Masemitrela zake kama 20 hivi wewe wakati huo unashangaa Kama Kurasini kumbe kuna viwanja? Wakati huo hata kigari cha mkopo tu huna. Fikiria vitu kama hivi. Utajua vizuri umuhimu wa kutumia muda wako vizuri. Sasa September hii mwaka unakatika. Wewe mwaka huu nini kipya hasa unataka kufanya kimaendeleo..
So kama unataka kuhakikisha mambo yanakuwa sawa mapema ungali mdogo ungali na nguvu nyingi bado basi njoo WhatsApp 0788366511 ujifunze jinsi ya kutumia muda vizuri na kupiga hatua kubwa! Niandikie tu message yenye maneno hayo: “Life begins at 40” then tutazungumza.
Life Begins at 40 my friend. How Old are you now?
Semper Fi,
Andrea G Muhozya Dar es Salaam, Tanzania East Africa
Comments