top of page

JINA LA YESU LATOSHA


power of Jesus name

Bwana Yesu asifiwe…

“ Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye. ” Wakolosai 3:17

Bilia inakutaka ujue kwamba kwa kila ulifanyalo unapaswa kufanya katika Jina la Bwana Yesu,kwa sababu ndilo jina pekee lituokoalo kwalo. Biblia imeweka wazi katika hili,kwamba hutakiwi kujisumbua katika jambo au kitu chochote bali tumia tu Jina la Yesu na hilo pekee linatosha. Watu kama wengeelewa nguvu iliyopo ndani ya Jina la Yesu hakika ubunifu tulio nao leo kwenye ibada usingekuwepo kabisa. Ebu fikiria ubunifu wa kibinadamu katika ibada unavyoendelea leo,kwa maana watu wamebuni mbinu mbali mbali katika ibada,kama vile;

  1. Maombi – Yameongezwa na mambo mengine kama mafuta,chumvi,maji,vitambaa vya upako,mchanga n.k.Vimechukua nafasi kubwa kuliko jina la Yesu. Ikiwa kama Roho mtakatifu ameelekeza na yatumike kwa wakati,lakini ukweli ni kwamba hakuna maelekezo ya Roho,ni ubunifu na biashara za watu.

  2. Sarakasi ibadani – Bahati mbaya sana,zipo ibada ambazo ni za maigizo. Mbali na pale ambapo Roho anaposhuka na kufanyika ishara,Bali sasa kuna watu wanaopanga maigizo kabisa kwa faida zao,kutafuta pesa.

Hakuna sababu ya kutumia kitu ambacho hujaelekezwa na Mungu kwa Roho wake wa milele.Kwa nini imefika wakati kwa wakristo kuliacha jina la Yesu pembeni na kukimbilia vitu? Kuna haja gani ya msingi? Kama ni maombi,basi ni vyema uyafanye kwa Jina la Yesu tu. Naye mwenyewe atajibu maombi hayo. Ninakubali kwamba upo wakati ambapo Roho mwenyewe anaweza kutoa maelekezo ya kutumia chochote kile na mambo yakawa sawa sawia.Lakini kibaya ni kwamba tunatumiaga akili zetu na ubunifu wetu halafu bila kumwogopa Mungu tunasema tumeambiwa na Roho wa Mungu kufanya tuliyoyafanya.! Jamani Mungu hadhiakiwi,chochote upandacho ujue utavuna tu (Wagalatia 6:7),kama mtu atapanda udanganyifu mkubwa wa namna hii,ni lazima atavuna ghadhabu kubwa ya Mungu.

Ikiwa kama umebarikiwa, nifahamishe. Kwa msaada zaidi pamoja na huduma ya MAOMBI piga kwa namba hizi hizi; +255 683 877 900.

What’s namba .+255 746 446 446

Na Mch. G.Madumla

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page