top of page

JICHO LAKO LIKIKUKOSESHA LING’OE ULITUPE MBALI NAWE.


eye

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi,

 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum” Mathayo 5:29

Andiko hili halina maana ya kuuchukia mwili wako kwa kuuharibu.Tafsiri ya andiko hili,halipo kwa jinsi ya kimwili isipokuwa Yesu anajua fika viungo vyetu katika mwili vinatukosesha sana kwa tamaa. Lakini hoja ya msingi anayoizungumzia hapo ni kwamba;ikiwa kama kuna kitu/jambo ambalo linaonekana ni la muhimu sana katika maisha yako,mfano wa jicho lilivyo na maana kwenye mwili wako,lakini ukagundua kwamba kitu/jambo hilo linakusababisha umkose Bwana,basi ni afadhali uachane nalo kuliko kuendelea nalo na kisha ukaingia hukumuni.

Mfano unaweza ukawa na rafiki tu ambaye mmeshibana sana,na kwa nje anaonekana ni mtu mzuri,lakini unapomchunguza kiroho unagundua kwamba rafiki huyo ndiye chanzo kikubwa cha kurudi nyuma katika wokovu/kiimani,sasa Neno linakutaka umwache huyo ajapokuwa ni mzuri kwako na anapendeza,lakini ni afadhali umkose kuliko kukufanya kuingia dhambini.

Wakati mwingine jicho likoseshalo linaweza likawa ni eneo lako la kazi ama kazi fulani uifanyayo. Kazi hiyo inaweza kuonekana ni njema katika jamii uliyopo hata kiasi cha watu wengine wanaisifia lakini ukweli wenyewe unaujua wewe uifanyayo kazi hiyo,unapogundua kazi hiyo ni lango la jehanamu,lango la kukuangusha dhambini,ni afadhali kuiacha/kuingoa na kuendelea na wokovu wako bila kazi. Mfano hu,Yesu ameutoa hali akijua vizuizi vyetu vinavyotuzuia,

Yeye ni Munhgu anajua jinsi ambavyo watu wakipenda inakuwa ni vigumu kuacha kwa sababu basi tu wamependa hata kama kitu walichopenda kina madhala,lakini Bwana akwambia leo,ni afadhali kungoa kinachokukosesha ufalme wa mbinguni kuliko kuendelea kukishikilia. Chunguza ni nini ulichonacho kinachokukwamisha,hata kama ni kizuri namna gani,kubali kulipa gharama ya kukiacha,usonge mbele na Bwana.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900

What’s app namba yetu; +255 746 446 446

Na Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

Commentaires


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page