JEHANAMU.
- Mch. Gasper Madumla
- May 22, 2019
- 1 min read

Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi.
Kwa mujibu wa agano jipya neno Jehanamu lina maana sawa na neno “Ziwa la moto au Jehanamu ya moto” ni mahali pa mateso pa adhabu ya mwisho,mateso ya umilele. Neno hili,Yesu alikuwa akilitumia mara kwa mara katika mifano yake akionesha ni wapi waovu watakapoishia ( Mathayo 13:41-43).
Hata hivyo neno hili,linaonekana kutoka kwenye neno hili la Kiebrania “ Bonde la Hinomu” lililotokana na mtoto wa Hinomu “ Mwana wa Hinomu ” ( Yeremia 19:1-13) . Bonde la Hinomu ilikuwa ni sehemu ya nje ya ukuta wa Yerusalemu mahali ambapo Waisraeli walikuwa na ibada za sanamu na waliteketeza watoto wao kama sadaka ( Yeremia 7:31). ( Mungu aliwaadhibu kwa matendo yao). Katika eneo hili,uchafu wa jiji,vigae na vyombo vya aina mbali mbali vilitupwa hapo na kuchomwa moto. Moto wake ulikuwa ukiwaka kila siku,mkali,harufu kali,moto usiozimika,uharibifu usiokoma,kuna giza baya! Picha ya nje ya bonde la Hinomu, huonesha jinsi ambavyo Jehanamu ilivyo na moto usiozimika,uharibifu wa milele,kwenye giza la milele.
Hivyo,Jehanamu ni mahali pa kutisha kuliko mahali pengine popote pale. Hakuna mtu apendaye kwenda Jehanamu, lakini ipo kwa watu ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima ( Ufunuo 20:15). Kuokoka kwa binadamu asikamatwe na moto huu, ni kumwamini Kristo na kumpokea,yaani kuokoka,( to be justified) na kumruhusu Bwana awe Bwana wa maisha yako.
Ikiwa kama umejifunza kitu,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa++255 746 446 446 What’s app ni namba hiyo hiyo
Na Mch. G.Madumla.
UBARIKIWE.
コメント