top of page

JE WEWE U MTUMWA? MTUMWA WA HAKI AU DHAMBI?

@ Madumla G.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi ;

Je wewe u mtumwa? Mtumwa wa haki au dhambi? Ni swali hilo la kujiuliza. Na ukijiuliza swali hilo utagundua kuwa wewe pia ni mtumwa kama nilivyo mimi ni mtumwa, lakini je ni mtumwa namna gani hapo ndipo watu tunatofautiana. Jambo la kushangaza ni kwamba watumwa wa haki ni wachache ukilinganisha na watumwa wa dhambi. Kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya, nimegundua kuna maumivu kwenye utumwa wa aina zote mbili, kwa maana wote wawili wapo chini ya sheria ya bwana wao.

  1. Mtumwa wa haki.

Mtumwa wa haki ni yule ambaye amefungwa na sheria ya neno la Bwana, hana uhuru wa kutenda ya kwake bali yale tu atakayo Bwana Mungu. Mtumwa wa haki ni lazima awe na kazi ya Bwana wake, na ni lazima aifanye “ Paulo mtumwa wa Kristo ” Warumi 1:1. Yeyote ambaye ni mtumwa wa Kristo, basi ujue hana lake mwenyewe isipokuwa hufanya Bwana atakayo. Jifunze kwa Paulo, si kila sehemu Roho mtakatifu alimpa ruhusa ( Matendo 16:6) kwa sababu yeye ni mtumwa wa Kristo.

Jiulize Je wewe unakwenda kila sehemu utakapo? Ikiwa ndio, lazima ujihoji na kujikagua kwa maana kutakuwa na shida kwenye wokovu wako! Roho mtakatifu hawezi kukupa ruhusa katika kila uendako, ufahamu hilo. Mtumwa wa haki ni lazima awe limited / azuiliwe juu ya mambo fulani asiyafanye na mengine afanye. Hivi mtumwa anaweza kufanya yote atakayo isipokuwa ameruhusiwa na Bwana wake?

Kumbuka; mtu Yeyote atakaye kuwa mtumwa wa haki ni lazima ataudhiwa tu! ( 2 Timotheo 3:12). Hivi ujawahi kumuona mtu ambaye kwa kweli amejitoa kikamilifu kwa Bwana kiasi kwamba mambo yake yote ni ya Bwana lakini papo hapo haachi kukwazwa! Wapo wa namna hii.

Ukitumika kwa Bwana ni lazima utakwazwa, utaumizwa ; wakati mwingine wanaokufanyia hivyo ni watu wale wale wa nyumbani kwako. Lakini uyaonapo hayo, usishtuke Kwa sababu wewe u utumwa wa Bwana, na maudhi / mateso hayana budi kuja. Yajapo hayo, wewe endelea kutumikia kifungo chako cha haki, ukitazama nyuma na kuwaangalia watu wengine unaweza ukakata tamaa!/ ukaanguka. Heri kuwa mtumwa wa haki, ukae nyumbani mwa Bwana na ufanye sawa sawa na Bwana atakavyo.

Lengo la Mungu ni kwamba kila anayeokoka kwa kumpokea Bwana Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yake awe mtumwa wake kwa sababu Yesu ndiye Bwana wake. Yesu akiwa Bwana wako maana yake wewe u mtumwa wake na unatakiwa kumsikiliza Yeye Bwana anataka nini. Hapo zamani kulikuwa na mfumo wa watumwa na bwana zao, bwana alikuwa ndie boss mwenye kauli ya mwisho na anayesikilizwa sana.

Maamuzi yote yalitoka kwake! Hivyo, nafasi ya bwana sasa imechukuliwa na Yesu ambaye sasa naye ni Bwana juu ya maisha yako. Ebu jihoji, unanafanya nini sasa, je Bwana wako amekupa ruhusa? Je kule uendako, umepata ruhusa kwa Bwana wako? Unataka kuingia kwenye ndoa na huyo mtu, Je Bwana wako amekupa ruhusa? Unataka kufanya biashara, Je umeruhusiwa na Bwana wako? Jihoji sasa, alafu jijibu mwenyewe!

  1. Mtumwa wa dhambi.

Huyu ni mtu ambaye yupo kwenye gereza la dhambi. Dhambi kama roho inamuendesha itakapo naye ujikuta akiitumikia kwa maumivu mengi. Kumbuka ;kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi ( Yoh. 8:34). Ibilisi ndio bwana wa dhambi, baba wa uongo tangia zamani. Naye ana milki gereza la watumwa wa dhambi ingawa Yesu alikwisha shughulikia dhambi pale msalabani. Hivi; jihoji leo, je yale uyatakayo mema kuyafanya unayafanya hayo au unafanya usiyoyata kufanya? Je upo tayari kulipa gharama ya aina yoyote ili ufanye dhambi?

Wewe hujawahi kuona mtu asiyetulia mpaka afanye dhambi fulani hivi, ndipo unamuona katulia. Yaani dhambi inamkereketa na kumuwasha washa ndani yake, hivyo akisha fanya sasa utulia. Wewe je unapelekeshwa na tamaa hata kufanya dhambi mara kwa mara? Ikiwa ndivyo, basi ujue unahitaji msaada zaidi wa kukombolewa hapo ulipo maana u mtumwa wa dhambi. Kuitumikia dhambi sio mpango wa Mungu bali ni mpango wa shetani.

Mimi sielewi, eti kuna faida gani kuitumikia dhambi? Au unajisikia furaha gani unapopanga kumkosa Mungu? Ebu fikiria anapata faida gani mtu ambaye anafunga safari kutoka Kibamba-Mbezi mpaka Temeke kiembe mbuzi au mpaka Keko magurumbasi ( Yaani umbali fulani hivi mrefu) kwa ajili ya kupeleka umbeya tu! Au kwa ajili ya usinzi!!! Ni mbaya sana, huu unaitwa utumwa wa dhambi ambao mtu anapelekeshwa kutoka sehemu fulani mbali mpaka sehemu nyingine mbali kwa ajili ya kufanya dhambi fulani hivi, alafu akimaliza hurejea nyumbani kwake mbali tena usiku!!!

Sijaelewa wewe u mtumwa wa namna gani, mtumwa wa haki au dhambi? Lakini ni maombi yangu leo uwe mtumwa wa haki yaani mtumwa wa Kristo. Lakini ukiona kuna mambo yasiyokuwa ya Mungu yanakupelekesha hata kuanguka dhambini mara kwa mara, ujue unahitaji masaada zaidi. Ikiwa ndivyo, ebu chukua hatua ya imani unipigie sasa kwa;

+255 683 877 900

Namba ya What’sapp ni .+255 746 446 446

Mch. Gasper Madumla.

UBARIKIWE. 

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page