top of page

JE UNAIKUMBUKA SIMULIZI YA KIMBALA MBALA ? šŸ˜Ž


Shalom…

Kwa ufupi sana.

Watoto wa siku hizi hatujui simulizi za wazee wetu wa kale. Hiki kizazi cha ā€œ dot komā€hakina maana kabisa! Hivi wewe unakumbuka simulizi gani za kale? Zamani hizo wazee walitumia muda wao kwa ajili ya kukifundisha kizazi kwa njia ya simulizi, hivyo utaona akina babu na bibi huketi chini ya mwembe na kusimulia hadithi kwa lengo la kufundisha jamii. Sasa kuna story ya kimbala mbala. Huyu alikuwa ni kijana mwenye choyo, mnafki, mwenye roho mbaya.

Siku moja mzee kimbala mbala na wenzake walikutanika nyumbani. Na kimbala mbala alikuwepo siku hiyo. Muda ulipowadia wa kupika chakula, basi kama ilivyokawaida, wakina mama wakaingia jikoni ā€œ kukorofisha mamboā€ kimbala mbala alipogundua kwamba wakina mama wanaanza kupika chakula alafu ni chakula kile kitamu akipendacho, basi unaambiwa kimbala mbala akaenda kitandani kulala.

Kimbala mbala alipokuwa kitandani wala hakulala usingizi bali alijifanya kana kwamba amelala huku akitega sikio na kuwaona wakina mama wakishughulika huko jikoni kwa maana unajua tena nyumba za udongo wakati mwingine ukiwa ndani unaweza ukachungulia chungulia nje kwenye kamlango kamakuti. Walipomaliza kupika wakaenda kumwamsha kimbala mbala aje ale, na kimbala mbala kwa unafiki wake akajifanyisha eti anakoroma ā€œ griiiii, groooohā€

basi mzee wake akakazana kumwita ā€œ wee kimbala mbala, amka tule.. ā€ kimbala mbala anamsikia mzee wake lakini kajikausha kimyaaa! Kama kalala kweli. Wale wamama wakapakua chakula na kuanza kunawa huku wakimsubili kimbala mbala aamke. Baada ya dk chache, mzee wake alipoona kimbala mbala aamki, akaamua kumpiga piga mguuni huki akimwambia ā€œ wee mtoto, amka… Shauli yako, sisi tunakula chakula chote, wewe si umelala bhana, utajua mwenyewe ā€ Lakini hata hivyo kimbala kaukausha, kimya, yeye anajifanya kama vile anakoroma tu. Sasa mzee kaona isiwe kesi, kaondoka naye kaenda kuketi chini, akanawa.

Wale wamama wakamwuliza ā€œ vipi,? Huyo kimbala mbala haji,? ā€ mzee akawaambia wamwache nao waendelee kula. Ile wanaanza tu kula, kimbala mbala huyo kaamka, lakini huku kajifanya anapepesuka pepesuka, macho kafumba. Basi unaambiwa kimbala mbala kaenda moja kwa moja mbaka kwenye sinia la maankuli / chakula, kalikanyaga ā€œpaaa! ā€œ na guu lake la mashoto. ā€œ Aaaaah, aiseee, ā€ ndivyo walivyoshangaa wakina mama na mzee wake. Wakaacha kula kisha mara kimbala mbala akafungua macho yake na kuanza kupiga matonge huku akiwaambia`` karibuni kula waungwana, haaa mmesusa!! ā€œ basi kimbala akafakamia chakula chote yeye mwenyewe huku akicheka cheka na maneno yake ya kuwasanifu kiunafiki.

Kimbala mbala jamani, hata kwa kulumangia hafai!!! šŸƒšŸƒšŸƒ. Tabia ya kimbala mbala ni mbaya na inakufundisha usiwe mnafiki, maana kuna wakati mtu anaweza akatamani kupanga mambo yake mwenyewe bila kuangalia wengine. Ebu fikiria yaani mtu yupo tayari hata kumwaribia mwenzake ili apate yeye. Ni mbaya, usipende kumtendea mtu kitu usichokipenda utendewe wewe. Usiwe kama kimbala mbala !!

Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi, au kama unahitaji kuongea nami moja kwa moja +255 683 877 900

Na Mch Gasper Madumla.

What’s app ni +255 746 446 446

UBARIKIWE.

ComentƔrios


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page