top of page

JE BADO HUJAFANIKIWA KUPATA MTOTO KWENYE NDOA YAKO?

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Kusudi mojawapo la kila ndoa ni kwamba mume na mke wazae watoto. Ni jambo la kawaida kuwaona baba na mama wakifurahia wanapowaona watoto wao ambao Bwana amewapa. Lakini pia ni jambo la kuugua moyo pale ambapo wanandoa waliokuwa wakitarajia kupata watoto alafu hawakupata; Biblia inasema  “ Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.” Mithali 13:12 . Moyo mwanadamu unaumia sana pale mtu anapotarajia kitu alafu kitu hicho kikachelewa kuja au kisije!!!. ( Kwa sababu ni ukweli usiopingika kwa wanandoa kwamba; wanapofunga ndoa basi hapo hutarajia kupata watoto).Matarajio ya kupata mtoto katika kipindi hiki yametofautiana sana na yale matarajio ya kipindi cha miaka ya zamani kwa sababu hapo mwanzo waamini walijua fika mtoto ni zawadi itokayo kwa Mungu,Lakini leo tumeshuhudia mara nyingi watu wakienda kwa waganga kutafuta watoto au mara nyingi wanandoa wamekua wakitumia njia za kipepo katika kutafuta mtoto.

  1. Mtoto anatoka wapi?

Wanaume wengi kwenye ndoa wamechanganyikiwa siku za leo kwa maana wanadhani mtoto anatoka kwa wake zao. Na ndio maana umeona wakidai wake zao wawape watoto au wakati mwingine huwanyanyasa wanawake na kuwaita majina ya ajabu ajabu kama vile “…wewe mke wangu ni tasa tu..”. Tabia hii ya wanaume katika ndoa inaonesha ukweli kabisa kwamba hawajui mtoto anatoka wapi,wao hujua ni mwanamke ndiye anawajibu wa kuleta watoto? Sasa nikuulize wewe,Hivi ni kweli mwanamke / mke ndiye ana wajibu wa kukuletea watoto? Imetoka wapi wazo hkama hili?. Na bahati mbaya pia,wapo wanawawake / wake wamechanganyikiwa wakidhani mwanaume ndiye atoae watoto,hivyo wanawake wa namna hii,siku zote utakuta wakidai waume zao wapatiwe watoto. Biblia inasema “ Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi. ” Mwanzo 30:1. Huo ndio mtazamo wa mwanamke Raheli,kama ulivyo mtazamo wa wanandoa wa leo wakidhani ya kwamba mtoto anatoka kwa mpenzi wake.

Mtoto ni zawadi itokayo kwa Mungu. Kumbuka ; ikiwa kitu kikiwa ni “zawadi’‘ basi ujue huwezi ukadai kwa kulazimishwa kupewa bali unaweza kumwomba mwenye zawadi akupe. Na akikupa wewe unapaswa kupokea bila manunguniko kile alichokupa. Lakini wengi leo wanaomba mtoto na Mungu huwapa,lakini wanapopata mtoto ambaye hawakumtarajia basi hurudi kwa Mungu na kumnungunikia kwamba “ kwa nini nimepewa mtoto huyu…” Kha! jamani kwani hata huyo si ushukuru Mungu,hujui kwamba ni zawadi tu hiyo? Mfano wanandoa wanaweza wakawa wanaomba Mungu awape mtoto wa kiume,na Mungu akawape mtoto wa kike kwa kusudi kubwa tu. Lakini cha ajabu wanandoa hao wakaanza kumlalamikia Mungu,na utawaona kwa namna ya malalamiko yao katika matendo,kwa maana wataanza kwa jitihada zao za kumtafuta mtoto wa kiume,sasa watu wa namna hii utakuta mwisho wa siku wamezaa watoto wengi wanaofutana fuatana hatahuwezi kujua yupi ni mkubwa alafu wote wamekuwa wa jinsia moja labda ya kike kwa sababu wao hawaridhiki na wanatafuta mtoto wa kiume! Laiti mtu akijua kwamba mtoto ni zawadi itokayo kwa Bwana,basi angelidhika na yule ambaye Bwana amempa.

  1. Je ni kweli mtoto anatoka kwa Mungu?

Biblia inajibu swali hili kwa wepesi kabisa ;“ Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.” Mwanzo 25:21. Biblia inatupa mambo muhimu ya kujifunza kupitia andiko hili; Kwanza tunaelezwa “Rebeka alipata mimba kwa sababu Mungu alifungua tumbo lake” hii ni kuonesha kwamba Mungu aliruhusu Rebeka naye apakate mwana,kwamba mtoto hutoka kwa Mungu. Lakini pia tunaona utaratibu uliotumika kwa Rebeka kupata mimba,ullikuwa “utaratibu wa maombi”. Kwa nini mpaka maombi yafanyike ndipo Rebeka apate mtoto ?

JIBU;

Rebeka amesimama kuwakilisha wanawake wote ambao matumbo yao “yamefungwa” lakini kufungwa kwa tumbo la Rebeka hakukutokana na shetani bali Mungu mwenyewe. Kumbe hata Mungu anaweza akalifunga tumbo la mwanamke kwa muda fulani ili “kusudi lake lipate kutimia”. Tumbo la Rebeka lilikuwa limebeba kusudi kubwa la Bwana kiasi kwamba haikuwa rahisi kushika mimba;Katika hili jifunze hata kwako,inawezekana bado hujapata mtoto lakini ujue lipo kusudi la Mungu katika huyo atakayekuja. Jambo hili si wengi wanalitazama hivi ninavyokufundisha leo. Lakini shetani pia anaweze kulifunga tumbo la mwanamke pale ajuapo kusudi kwa kile kitakachozaliwa,hivyo haitakuwa rahisi kuzaa kwa muda uatakao wewe. Kumbuka wewe unapanga na Mungu anapanga vile vile,na muda utakao wewe ni tofauti na muda atakao Mungu. Lakini jambo la pili “ Isaka alihitajika aombe” hii ni sawa na kusema kama Isaka asingeliomba,labda Rebeka asingelishika mimba kwa wakati uliokusudiwa.

Je Isaka wako yupo? yupo wapi? Ebu cheki leo,mumeo ndiye anayetakiwa kuwa kama Isaka wako,lakini mwangalie hata kama anaomba!!! Au angalia kuomba kwake ni ajabu! Isaka wako akilala ujue utachelewa sana. Lakini cheki tena leo,utakuta Isaka wako sio wako kwa kweli wewe umemwiba tu,ni mume wa mtu mwingine ila wewe unalazimisha uzae naye. Kha! sasa inakuaje hapo kwa mfano!. Hapa nina maana ya kwamba Kwanza hamjafunga ndoa,ninyi ni wachumba sugu sasa ni mwaka wa tano mnaishi pamoja Au la mmewekeana viapo tu kwamba wewe ni mke wangu na wewe ni mume wangu. Sasa ; Isaka /mume wa namna hii hawezi kuwa na ujasiri kumwendea Mungu,maana njia zenu bado hazifai.

  1. Nini cha kufanya unapokuwa hujapata mtoto kwa muda mrefu?

01. Usimlaumu mwenzi wako wa ndoa. ( Ona ya kwamba hana makosa,kwa kuwa si yeye anayepaswa kukuletea mtoto kwenye ndoa yako). Isipokuwa penzi lizidi kunoga kwake na kumwona ni mtu mzuri kwako atokaye kwa Bwana.

02.Usipokee shauri kwa kila mtu. ( Kwa sababu hata wao hawana uwezo wa kukupa mtoto).

03.Endelea kuomba si kwa manunguniko kwa maana mtoto ni zawadi tu.( Ni lazima ujue kwamba hutakiwi kunungunika bali mshukuru Mungu huku ukimsihi Bwana kwa mapenzi yake awape na ninyi furaha ya watoto. Katika hili,mnapaswa kuombewa pia maana kama kuna kifungo kutoka kwa shetani basi kiachie kwa njia ya kuombewa na mtumishi wa Mungu. Kama unamwamini Mungu,basi acha kutumia miti shamba ya namna yoyote hata madawa ya hospitali stopisha kwanza,ili Bwana kwa mkono wake atende. Mkumbuke Sara mwanamke asiyetumia miti shamba wala hospitali tena mwanamke aliyekoma katika siku zake,lakini katika hayo bado Bwana alimtendea Sara kwa kuzaa mwana (Mwanzo 18:14)

Ikiwa umebarikiwa na fundisho hili nifahamishe pia. Kwa maombezi pia nipigie kwa namba hizi hizi + 255 655 111 149 / 683 877 900 / 762 414 446.

WhatsApp ni +255 655 111 149.

Mch.G.Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page