top of page

IMARISHA NDOA YAKO ( Building a great marriage) ~ 01

Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi…

Hakuna kitu cha muhimu kama kuwa na ndoa yenye amani na furaha. Maana ustawi wa ndoa yako ndio mafanikio yako. Hivyo unapoona ndoa yako ina shida,basi ujue si jambo la kupuuzia kabisa kwa maana kama utapuuzia ujue unaifanya ndoa yako kuvunjika. Ndoa ni taasisi ya namna yake ni kama chuo fulani kinachohitaji akili na utulivu ili ufahulu. Cha ajabu katika ndoa ni pale ambapo mwanandoa anapopewa cheti cha ndoa siku ile tu anapofunga ndoa kablla hata ya kuingia katika ndoa.

  1. Ikite ndoa yako katika msingi wa Kristo

Unajuajambo lolote zuri linahitaji msingi mzuri. Na kwa kuwa ndoa ni safari ndefu,inahitaji msingi mzuri. tunaposema ikite/isimamishe ndoa yako katika msingi wa Kristo tuna maana kwamba hofu ya Mungu itawale katika ndoa yako. Wewe na mwenzi wako mwe watu mliokubali kuongozwa na Mungu,suala la ibada kati yenu lisikosekane kila siku. Ndoa iliyosimama katika Kristo haiwezi kutikiswa ikatikisika. Upepo na dhoruba ijapo na kuipiga ndoa hiyo,bado ndoa itasimama tu wakati wote.

Lakini ni vyema sasa tukajiuliza swali hili,“kuna haja gani ya kuimarisha ndoa? au kwa nini ndoa iimarishwe kwani ni mbovu?” Hili ni swali muhimu sana kwa maana kama ndoa yako ni imara,hakuna haja ya kuiimarisha kwa sababu tunaimarisha kitu kilichokuwa dhaifu au kibovu. Tuangalie mifano michache katika Neno kuhusu ndoa ambazo zilihitaji matengenezo,ndoa hizi zimeandikwa kwa ajili ya kuponya ndoa zetu.

INAENDELEA HAPA KUANDIKWA SASA…..

Ebu sikia hii;

Kulikuwa na mdada mmoja ambaye alikuwa ameolewa na ameokoka japo wokovu wake ulikuwa wa kimashaka mashaka. Mdada huyu ni mrembo, na akiwa ofisini kwake mahali ambapo anajua mumewe hayupo karibu, huwa huru zaidi kuendelea na mambo yake. Ana simu mbili . Moja ni ya nyumbani na ya kutembelea na ya pili ni ya ofisini tu ambayo mumewe haijui hiyo;

akitoka ofisini huizima na kutumbukiza kwenye droo yake kisha funguo huondoka nayo. Simu ya ofisini ni ya kuchati na watu wake, ambao kwa kweli ni wapenzi wake na amewaambia atakuwa hapatikaniki kila aondokapo ofisini sababu hiyo simu ataizima;alafu simu zote zina strong password / zina paswedi kali kwenye kila kitu. Wewe umeshawahi kuona password hata katika kupokea simu tu. Duh!! .

Sasa;Kwa picha hii tu, inaonesha binti huyu hajamfanya mumewe kuwa rafiki kwa sababu kuna mambo mengi anayoyafanya na mumewe hayajui yaani mume amefichwa. Sasa sijui kama na mumewe naye ni hivyo hivyo au la! Ilo watajua wenyewe bhana sisi sio kazi yetu. Lakini nilikuwa nakuonesha jinsi wanandoa wanavyo danganya. Sijui wewe katika eneo hili kama umepona!

leo kuna shida hii ya wanandoa kudanganyana kwa sababu tu kwanza wokovu wao ni wakugushi, pili hawajafunzwa kiroho sawa sawa kuhusu mambo ya ndoa. Mwenzi wako lazima awe rafiki yako wa karibu sana. Najaribu kukuwekea msingi wa fundisho la leo kwa namna ambayo ukimtanzama mpenzi wako wa ndoa umuone yeye kuwa ni rafiki. Hivi unajua rafiki yako akikuhitaji umfuate mahali fulani hata kama umechoka utaenda tu.

Ndio, utaenda tu, hutaangalia umbali, wala hutaangalia atakulipa kiasi gani, bali utajikuta ukifunga safari na kumwendea. Sasa chukua picha hiyo hiyo kisha mweke mumeo hapo au mkeo hapo, alafu fikiria ni mara ngapi mumeo au mkeo anakuomba umfanyie jambo fulani labda anakuhitaji katika tendo, nawe kila wakati unasema “ nimechoka ” au “ leo tena sipo vizuri, ninaumwa, naomba uniache… “. Nikuulize huo ndio urafiki kweli? Unafikiri aende wapi sasa? Nimekupa mfano tu.

Nilimwona mwanandoa mmoja, alikuwa ni mwanaume mmoja aliyekuwa na wivu wa kupitiliza. Najua kila mwanandoa si mke wa la mume wote wana wivu. Lakini huyu mwanaume ninayekusimulia alikuwa na wivu kwenye centigrade 99.9 / viwango vya juu vya wivu. Yeye akisikia mke wake kasimama na mtu lazima apeleleze huyo ni nani aliyesimama na mke wake, utakuta akiuuliza “ kasimama na nani, eeh niambie” alafu wakimwambia “ kasimama na shoga yake, mama Frank… ” husema “ ahaa, bahati yake “. Sasa siku moja akamuona mkewe kampakia jibaba / jeba ( mwanaume) mmoja hivi kwenye gari maana mkewe ana gari yake binafsi hutumia kwa shughuli zake.

Jamaa alipoona hivyo, ilimbidi aanze kuifukuzia ile gari ya mkewe. Sasa sijui alimpata au la! Lakini yule mwanaume aliyempakia kumbe alikuwa ni mdogo wake mkewe yaani ni shemeji tu. Khaa! Wivu gani wa namna hii,? Unafikiri una uwezo wa kumchunga mkeo? Akiamua kufanya ujinga si anafanya tu, kwani wewe upo naye kila saa? Hata mke, huwezi kumchunga mumeo. Mumeo atachungwa na nguvu za Mungu ambazo zitasababishwa na ufahamu huj wa namna ya kuimarisha ndoa yako.

Yapo mambo mengi yanayotendeka kwenye ndoa na bahati mbaya wanandoa hawajui kuyafanyia kazi katika kuboresha. Katika fundisho hili tunapoendelea utajua moja hadi jingine na ni kibiblia tu. Lakini kabla sijaanza kukueleza mambo Hayo, nianze na hili la karibu kabisa;

  1. Badiliko la ndoa linaanzia kwako.

Usimtegemee mwenzako akuletee badiliko kwenye ndoa yako, kwa maana ni wewe ndio wa kubadilika kwanza. Upya wa ndoa unaanzia kwako sio kwa mumeo / mkeo ni wewe. Usiseme kwamba wewe upo sawa bali mwenzako ndio tatizo bali sema ni mimi ndio natakiwa nizidi kubadilika ili kubadilika kwangu kukawe chachu ya kufanya mwenzangu abadilike pia.

Ni kweli mwenzako anaweza akawa ndio chanzo cha migogoro yote ya ndoa yako, lakini katika hayo yote wewe umeonesha jitihada gani ya kubadilika kwanza wewe, maana mbona na wewe una- react / unarudisha mashambulizi? Umegundua kwamba hata kwako kunahitajika badiliko la ndani. Ikifika wakati ukamuona mwenzako hafai, ujue na wewe hufai maana ninyi ni mwili mmoja basi mwili wote haufai.

Hivi ikiwa mwenzako ni mkosaji, kazi yako wewe ni ipi? Na wewe ukosee kama sehemu ya kulipiza kisasi? Kama mwenzako hajali, je na wewe unatakiwa kutomjali? Tafakari hayo, ikiwa ndivyo ufanyavyo hivyo, ujue na wewe una shida kwa kweli. Ila wewe ukibadilika katika eneo lolote lile, ujue utasababisha badiliko kubwa kwenye ndoa yako.

Ebu fikiria mume kakosea ni mkorofi hivi, alafu wewe mke unachukua ukorofi wake kwa kumnyima unyumba / tendo la ndoa kama adhabu ya ukorofi wake. Je unafikiri hiyo ndio dawa? Au unafikiri atajirekebisha kwa adhabu hiyo? Mimi nakuambia mume hawezi kujirekebisha kwa adhabu hata mke hawezi kujirekebisha kwa adhabu. Kwa sababu adhubu sio nidhamu. Adhabu ( punishment) lengo lake ni kuleta chuki, ghadhabu, hasira bali nidhamu ( despline) hufanyika kwa kuongozwa na pendo mara nyingi ni kwa mazungumzo yenye hekima…

Kwa msaada zaidi wa ushauri, maombezi na mengineyo. +255 683 877 900

What’s app +255 746 446 446

@ Mch. G. Madumla.

ITAENDELEA…

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page