IMANI IOKOAYO.
- Mch. Gasper Madumla
- Feb 8, 2019
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi; Awali ya yote,kumbuka ya kwamba imani ni daraja la majibu yako yote kwa maana pasipo imani huwezi ukampendeza Mungu (Waebrania 11:6).Hata hivyo kitendo cha kuamini uwepo wa Mungu ni mwanzo tu wa imani. Unaposoma somo la imani utagundua kwamba mataifa huamini tofauti na wapendwa, kwa maana watu wa dunia kwanza nilazima waone hata kugusa ndipo waamini,Lakini waliookoka huamini pasipo kuona kwa macho ya damu na nyama.Swali la kujiuliza katika fundisho hili; Je imani iokoayo ni ipi? Inatoka wapi hasa?
“ Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa? ” Yakobo 2:14 .Ni swali makini sana hili;kwa maana ikiwa umeokoka na unaamini kabisa,Je kuamini kwako pasipo kutenda kile unachokiamini,Imani yako inaweza kukuokoa. Hivyo kupitia andiko hili utagundua mambo yafuatayo yanayoonekana kwa haraka; “ Mwamini ameitwa ndugu,ndugu mwenye imani bila matendo,Je imani yake itamwokoa?”. Hivyo imani iokoayo ni ile imani kwa Kristo Yesu yenye utii. Yeyote aliyeweka imani yake kwa Bwana na kutii katika kile Bwana atakacho,mtu huyo huitwa kwamba ana imani iokoayo.
Ebu fikiria hili;
Fikiria wewe ni mkristo unayeamini kabisa katika Bwana kalini unapitia kwenye tatizo fulani,labda tuseme ni mgonjwa.Na unaamini ya kwamba Bwana ndiye Mungu aponyaye. Alafu pata picha kwamba upo kanisan,kisha mchungaji akasikia kuomba na wale wote wagonjwa,mchangaji akatangaza madhabahuni kwamba “yeyote ambaye ni mgonjwa sigea mbele madhabahuni na Bwana atakuponya wakati wa maombi jioni ya leo. Lakini ingawa umesikia tangazo hilo,na usiende kule madhabahuni;ukaamua kubakia pale pale ulipoketi. Je kwa imani uliyokuwa nayo,itakuokoa ikiwa hujachukua tendo la kunyanyuka na kwenda mbele? Mtu mwenye kuamini bila kukitendea kazi kile unachoamini hana imani iokoayo.
Ni muhimu kujua kwamba hatuhesabiwi haki kwa njia ya matendo bali kwa imani tu lakini imani pasipo matendo imekufa. Hivi unafahamu hata mashetani wanaamini na kutetemeka? ( Yakobo 2:19). Lakini hawawezi kutenda mapenzi ya Mungu isipokuwa wewe na mimi tunaweza kutenda vile Mungu atakavyo. Ukifahamu ya kwamba unahitaji imani iokoayo basi huna budi kujifunza kiundani kuhusu imani. Kama kuna imani iokoayo basi ni dhahiri kuna imani isiyookoa. Bila shaka imani isiyoweza kuokoa ni ile imani yenye shaka. Mtu anaweza akawa anamwamini Mungu kabisa lakini akawa anaona shaka mara kwa mara hata aombapo bado akiona shaka basi hiyo imani haiwezi kukuokoa. Ebu cheki wanafunzi wa Yesu kwenye Mathayo 17:14-22,.
Hapo utaona wanafunzi wa Yesu ambao walishindwa kutoa pepo,na si kwa sababu walikuwa hawana imani! Bali walikuwa na imani yenye shaka kwa maana imani yao ilikuwa ni pungufu. Imani pungufu,ni imani isiyookoa bali imani timilifu ndiyo iokoayo.
Nifanye nini niipate imani iokoayo?
Hauitaji mambo mengi ili uwe na kiwango kizuri cha kuamini kwa maana Mungu ndiye afanyaye yote. Hata hivyo kwa upande wako,mambo yafuatayo ni muhimu ;
01. Kukubali kuwa mwanafunzi.
Watu wengi wamekosa misuli ya imani hata wao wenyewe hawawezi kuomba wala kujiombea na mambo yakaonekana kwa sababu ya kukataa kujifunza / kuwa mwanafunzi. Ninaposema uwe mwanafunzi nina maana ukubali kuketi chini ya kuhani afundishaye na ujifunze kama mwanafunzi ajifunzavyo. Kuna mambo mengi ya imani unahitaji kujifunza,kuna masomo mengi ya neno la Mungu unahitaji kujifunza,hivyo utapata uelewa na kujengwa imani yako pale tu utakapokubali kuwa mwanafunzi. Shida ya walio wengi leo,ni kwamba watu wanatafuta njia za mkato. Watu hukimbia kimbia kutoka kanisa hadi kanisa ,sehemu hadi sehemu kutafuta miujiza,na wala sio neno. Kitu gani biblia inasema kuhusu chanzo cha imani“ chanzo cha imani ni kusikia Neno la Kristo ” Warumi 10:17.
02. Kulitii neno.
Kila unachoambiwa na Bwana unajaribu kukifanyia kazi kwa kukiweka kwenye matendo,na hapo ndipo utakapomwona Bwana kwa maana kwa kufanya hivyo unakuwa ukitembea kwenye mstari wa imani iokoayo. Yale yale mambo unayoyaona wewe ni madogo madogo,lakini yafanyie kazi.+ Nitajuaje kwamba nina imani iokoayo? Ukiwa na imani kwa Kristo,imani ya namna hii. Utaanza kuona matokeo mazuri katika yale uyafanyayo ,mfano uona kiu ya kushuhudia,utapata wepesi wa kujibiwa maombi yako. Lakini pia shetani hatakuacha,shetani atakutupia makombora kwa lengo la kukuangusha.
Ukiona upo rohoni sana na makombola / majaribu yakiongezeka,wewe ujue ni hila za shetani anajaribu kukuzima,lakini wewe komaa na Bwana na ushindi utauona.+ Imani iokoayo ni lazima ijaribiwe. Hata kanuni za kawaida za maisha huwa tunajaribu kitu kuona ubora wake upoje. Na ndivyo ilivyo imani uliyokuwa nayo,lazima ipitishwe kwenye moto ili uchongwe imara. Tazama wote watu wa imani,utagundua wote walipitishwa kama kwenye moto,lakini uzuri ni kwamba Bwana alikuwa nayo; hivyo hata kama unapitishwa leo kwenye jaribu lolote lile ujue Bwana yupo nawe na chukulia jaribu hilo ni chekecho ya kupima imani gani uliyonayo.Songa mbele tu.
Kwa msaada zaidi na mengineyo +255 683 877 900 Mch.G.Madumla.
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Kommentare