IKIMBIE ZINAA – 02
- Mch. Gasper Madumla
- Nov 29, 2019
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi,
Neno “ikimbie / flee from sexual immorality” lina maana ya kujitenga mbali na zinaa. Biblia inapotumia neno “kimbia” ina maana kuna uwezo ndani yako ya kukimbia,la sivyo isingesema kimbia ingawa Bwana ndiye akuwezeshaye,lakini ipo nguvu ya kukimbia ndani yako. Kukimbia na kukimbilia ni mambo mawili tofauti,lile tunalojifunza ni “kukimbia”.
Zinaa huleta majuto
Uzinzi humfanya mtu kuumia moyo na kujiuliza kwa nini alizini? Wakati mwingine majuto yanamweka mtu njia panda asijue afanye nini,je aendelee kuzini au afanye toba na kuacha. Ikiwa mtu aziniye ni mwana ndoa,majuto yanaweza kumfanya mwezi wake kuwa pia katika njia panda,kwamba na yeye atoke nje ya ndoa kwa maana mwenzake anatoka au aliye na kubakia ndani ya ndoa. Zinaa inavunja ndoa sana! kwa maana adui hujaribu kupenyeza uovu penye uovu! Ukweli ni kwamba,usiruhusu majuto yakutie dhambini au usiruhusu uzinzi wa mwenzako ukutie dhambini,kwa maana dawa ya uzinzi sio uzinzi bali ni haki. Uzinzi ni furaha ya shetani ya kitambo kidogo ambapo yenye majuto makubwa ya muda mrefu.Hata kama mzinzi akitubu kwa Bwana,lakini majuto hayatamwacha! kwa maana akikumbuka tu,kwamba alizini basi hapo ni lazima atajuta kwa nini aliruhusu kuzini? Ukichunguza kwa ukaribu suala zima la zinaa,utagundua kwamba “majuto” ni zao kubwa mno la zinaa. Na majuto ni huzuni ipelekayo kwenye mauti!!
Uzinzi ndio dhambi pekee ya kijinga!
“Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” Mithali 6:32. Kitendo cha kutokuwa na akili ni kitendo cha kukosa maarifa,kuwa mjinga!Kwa maana kama mtu aziniye angelikuwa anajua kwamba katika uzinzi atajiangamiza nafsi yake basi ni dhahiri asingezini,na angelikuwa ni mjanja. Dhambi ya uzinzi,ni dhambi inayoonesha ni jinsi gani mtu alivyokuwa mpumbavu bila kujali cheo,au kisomo chake! Kwa maana mtu hata kama ni msomo au mwenye cheo kikubwa kiasi gani lakini kwa tendo moja tu la zinaa linafunua upumbavu alionao,
kwa maana huyo aziniye na mwanamke / mwanaume hufananishwa na mtoto asiyekuwa na akili,anaitwa “baby” kisha yupo tayari kuyafanya mambo ya ajabu kinyume na utu uzima wake,hata yeye mwenyewe baadae akija kufunguka na kuyatazama hayo aliyokuwa akiyafanya itambidi acheke na kujisemea kwamba “kweli nilikuwa sina akili”. Upumbavu uliopo katika uzinzi ni ile hali ya kujua baadhi ya matokeo yake,lakini bado unafanya! Kwa maana hali ukijua kwamba kwa tendo hili la uzinzi (tena wakati mwingine na mke wa mtu au mume wa mtu),utapata mimba,mauti,magonjwa,aibu au kupigwa na mwenye mke /mume,lakini bado unaendelea kufanya,Je huo si upumbavu? Je hapo pana akili njema kweli?
Yaani kuna watu ni wapumbavu kupindukia! Kwa maana kuna watu wako tayari kufa kwa ajili ya mke /mume wa mtu,hali wakijua kwamba yupo mwenyewe wa mtu huyu,lakini wao tayari wamekubari kuyapata yoyote yale,wengine wako tayari kupata maambukizi ya ugonjwa,kwa maana utakuta mtu anayezini naye amekwisha mwambia kwamba yeye hayuko vizuri kiafya,ana maambukizo lakini hata hapo utashangaa mtu huyo akisema “hakuna shida,tutakufa pamoja tu,ajali kazini” What!!!!! Je huu si upumbavu ? Uzinzi ni dhambi ya kijinga sana,kwa maana matokeo yake mabaya unayajua kabisa lakini,hugeuki bado!
Lakini kwa nini watu wanazini?
Hali ya sasa imechafuka sana,kwa maana kitakwimu isiyo rasmi ilikuwa inaonesha wengi walio katika zinaa walikuwa ni watu wasio na ndoa. Lakini sasa sarafu imepinduka kwamba wana ndoa wapo katika kiwango sawa cha zinaa na wale wasio na ndoa. Hali hii inatisha mno!!! Baadhi ya wana ndoa wamejikuta katika uzinzi uliokithili kwa kigezo chao kimoja wanachodai kwamba hawaridhishwi na mapenzi ndani ya ndoa/hawafikishwi !!! Lakini Je hili ni kweli? Je kama mke/mume hakufikishi vizuri,ndio utoke nje? unafikiri huyo wa nje hata kama ukipewa sasa uishi naye moja kwa moja je naye atakufikisha utakapo? Utagundua hata kama utapewa huyu wa nje,bado hatakufikisha utakapo? basi hiki csio chanzo kikuu cha uzinzi. Paulo anaeleza chanzo kikubwa cha kwanza cha zina,katika andiko letu la msingi,nacho ni;
01. Kongwa la zinaa
“Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.” 1 Wakorintho 6:12. Wakorintho walikuwa ni watu wa ajabu kwa maana walikuwa na msemo huo,kwamba vitu vyote ni halali kwa mwili,hivyo hawakupa umuhimu mwili isipokuwa mambo ya roho. Uzinzi haukuwa ni shida sana kwao isipokuwa shida ilikuwa ni kukosa ibada. Watu hawa walikuwa chini ya kongwa / nira ya zinaa,kwa maana waliiendekeza! Neno hilo linasema yeye Paulo hatatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote ikiwa na maana hatatawaliwa na uharibifu wowote ule. Uzinzi ni roho / kongwa zito ambalo mtu akiwa chini ya uwezo huo,hapo hataweza kuacha mpaka avuliwe kongwa/roho hiyo. Moja ya sababu kubwa sana ya kwa nini unazini ni kwa sababu ya kutiwa chini ya uwezo wa zinaa / kukamatwa na roho ya zinaa! roho ya zinaa ni roho hatari sana inayotesa na kusumbua wengi,isiposhughulikiwa madhara yake ni makubwa mno….
ITAENDELEA…
Ikiwa umebarikiwa nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa +255 683 877 900
Na.Mch. G.Madumla
Whatsapp namba +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Comments