IJUE BIBLIA YAKO.
- Mch. Gasper Madumla
- Feb 20, 2015
- 2 min read

Bwana Yesu asifiwe sana…
Kwa ufupi;
“ Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele. ” Isaya 40:8Vitu tuvionavyo vinaharibika,vitu vyote chini ya jua huja na kuondoka,bali neno la Mungu litasimama milele.Neno “ milele “ ni muda usiokuwa na kikomo/Muda usiohesabika. Hivyo neno la Mungu litasimama katika muda usio na kikomo.“ Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. ” Mathayo 24:35Tukumbuke ya kwamba; neno“ Biblia” limetokana na neno la Kiyunani “ biblion” lenye maana ya makusanyo ya vitabu vya neno la Mungu ( Vilivyovuviwa kwa pumzi ya Mungu aliye hai,ni maneno ya Mungu yenye uhai,yenye kufundisha,kuelimisha na kuadabisha)“ Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ” 2 Timotheo 3:16
Biblia ina vitabu 66, Agano la kale lina vitabu 39 na, Agano jipya lina vitabu 27.
Nyaraka za mtume Paulo ziliandikwa kama mnamo mwaka 48. BK. Ufunuo ndicho kitabu cha mwisho cha agano jipya,mnamo mwaka wa 100 BK kiliandikwa. Mpangilio huu haukulenga muda wa kitabu kilipoandikwa na Roho wa Bwana. Maana kama mpangilio huu ulilenga muda basi ni dhahili kabisa kitabu cha Ayubu kingekuwa katika mtililiko wa juu,yaani kingepangwa juu ya vitabu vingine au kingepangwa baada ya vitabu vya torati kwa sababu kitabu cha Ayubu kimeandikwa zamani kuliko vitabu vyote.
Katika biblia ya Kiyahudi,vitabu vyake ni hivi hivi,lakini mpangilio wake hutofautiana kidogo maana wao wamevigawa vitabu hivi katika makundi matatu tu; ~ Sheria (torati) ~ Manabii ~ Maandishi.
Lugha zilizotumiwa katika biblia.
Biblia katika agano la kale limeandikwa sehemu kubwa katika lugha ya Kiebrania,ingawa yapo mafungu ya maneno yaliyoandikwa katika lugha ya Kiaramu.Mfano katika vitabu kama ;Ezra,Yeremia na,Danieli Vimekutwa na mafungu ya lugha ya kiaramu. Hii ni kwa sababu kiaramu ilikuwa ni lugha iliyotawala katika uhamisho wa Baleli.Lugha iliyotumika katika agano jipya ni lugha ya Kiyunani ambayo ilikuwa ni lugha ya ulimwengu wote wa dola ya Kirumi.
Hata hivyo biblia ilikuja kutafsiriwa kwa mara ya kwanza ili kuwezesha uelewa kwa watu wengi wa kila taifa. Tafsiri ya kwanza inayojulikana ni Septuaginta. Hii ilikuwa ni tafsiri ya kutohoa maneno kutoka katika lugha ya Kiebrania kwenda katika lugha ya Kiyunani kama jinsi vile agano la kale lilivyoandikwa katika lugha ya Kiebrania.(Tafsiri hii ilifanyika mnamo kama katika mwaka 280 KK,huko Iskanderia nchini Misri)
Hata hivyo;kwa maelezo mengi zaidi na ya kina,tafadhali soma hapa katika,ingia sasa UCHAMBUZI WA VITABU 66 VYA BIBLIA TAKATIFU.
What’s app number pamoja na mawasiliano mengine ni +255 746 446 446
Mch.G.Madumla
UBARIKIWE.
Comments