HEKIMA YA MUNGU
- Mch. Gasper Madumla
- Sep 19, 2017
- 2 min read
Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.” Yoh.7:37-38
Maandiko hayo yanaeleza kuhusu “Roho mtakatifu” lakini pale biblia inasema “mito ya maji itatoka ndani yake” yaani kwa kumwamini Kristo,basi Roho mtakatifu ajidhihilishe ndani yako katika hekima,nguvu na Kila namna ya kupendeza. Vyote hivi vinakusudiwa kutoka ndani yako. Watu wanapotafuta hekima ya Mungu,wakutafute wewe. Watu wanapotafuta Neno la maarifa,wakimbilie kwako. Biblia inaongeza kusema;
“Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.” Yoh.7:38
Hii ikiwa na maana kwamba watu waitafute hekima ya Mungu kwako. Watu wenye kiu mbali mbali za kidunia kama vile kiu ya uesharati,uzinzi,wizi,sigara,uongo n.k wanapokuja kwako wakutane na mito ya maji yaliyo hai yenye kutoka ndani yako,kisha wakapokee maji hayo.
Mkristo ni wa mtoaji wa Neno la uzima. Watu wanapokujia waione njia,kweli na uzima ndani yako. Katika lugha ya kibiashara ningelisema kwamba kuwa mkristo ni sawa na mtaji ambao watu wanatakiwa wautafute kwako. Wakikupata wewe wawe wamepata mtaji wa katika maisha yako na singinevyo.
Unapokuwa ni mkristo uliyejazwa Roho mtakatifu,basi ujue mito ya maji itatililika kutoka kwako. Yaani ndani yako itatoka hekima ya kutia faraja mahali panapohitajika faraja,au ndani yako itatoka neema ya uponyaji kwenye maeneo yote.
Sasa ikiwa upo ndani ya Yesu na mito ya maji yaliyo hai,haitoki basi ni lazima kujiuliza kwamba ni kweli upo ndani ya Yesu? Au kuna shida gani ndani yako? Kwa maana Yeye Yesu ndani yake imo mito ya maji yaliyo hai yaani yupo Roho mtakatifu aliyefulika. Vipi kwako,watu wanapokutafuta wanamuona Mungu? Watu wanaiona ile neema ya kuzaa matunda ( moyo waushuhudiaji) ? Watu wanajisikia vizuri wanapokutana wewe?
Kumbuka;Kila mkristo anatakiwa kutoa kwa watu wa nje. Mkristo unapaswa utoe tunda la Roho ( Furaha,upendo,amani,utu wema,upole,kiasi,uvumilivu,fadhili na uaminifu).
Fanyia kazi hili,uweze kuwa mtu wa “kutoa” zaidi kuliko kupokea. Watu wanahitaji kupokea kutoka kwako wewe ambaye umepata neema ya wokovu.
Kwa mawasiliano zaidi piga +255 683 877 900
What’s app ni +255 746 446 446
Na Mch.G. Madumla
UBARIKIWE.
Comments