HAWA NDIO WAZAZI WALETAO MATENGANO!
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 6, 2018
- 3 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi…
Mojawapo ya tatizo kubwa linalosumbua kwenye familia nyingi ni tatizo mgawanyiko baina ya ndugu kwa ndugu tena ndugu wa karibu sana. Wakati mwingine ni ndugu wa baba na mama mmoja! Zipo sababu kadha wa kadha zinazowagawa ndugu na ndugu, lakini mojawapo ya sababu hizo wazazi na wenyewe wanahusika kuleta mgawanyiko. Tumeshuhudia mara nyingi wana ndugu hawaongei, hawapatani kwa sababu wazazi wao wenyewe wamekosa maelewano. Leo mimi ninajua inawezekana tatizo hili lipo pia kwenye familia yako, na hujui hata sasa mtamaliza lini mizozo hiyo kwa maana ni kana kwamba haiishi!!! Hivi ushawahi ona ogomvi wa ndugu kwa ndugu! Nakwambia usiombee ugomvi wa namna hii, kama kwa familia yako hakuna basi mshukuru Mungu sana, lakini ukiwauliza wale ambao kila kukicha ni matusi, na vitimvi kwa sababu kuna hali ya kupishana kwa kila mmoja, watakuambia ni shida gani wanayopisana
Wazazi au walezi wanatizamiwa kuleta amani kwenye familia na kuhakikisha familia inamjua Mungu lakini bahati mbaya, kinachotizamiwa kimegeuka na kuwa ni tofauti kabisa maana wazazi baadhi yao wamekuwa na taswira mbaya kwa watoto kiasi kwamba watoto wamekosa jema la kujifunza kutoka kwao. Ebu fikiria ndio unaishi na baba na mama ambao matusi yale ya nguoni kwao ni kila siku, mara baba kumpiga mama sababu ya ulevi wake, jamani ni kero!!! Unajua hata inafika wakati watoto wanashindwa kuwaleta marafiki zao nyumbani maana ni aibu tupu! Wewe hujui tu, ila mimi najua haya, yanaumiza sana 😭😭😭!!! . Ni shida ukiwa na wazazi wasiomcha Mungu, maana suala la kutoelewana kwao ni la kawaida tu.
Mbali na hayo, ebu jifunze jinsi mgawanyiko unavyoweza kuchipua kwa kuichukua familia ya Mr. & Mrs Isaka ( Isaka na Rebeka). Familia hii iwe kama case study / kitovu cha kujifunzia leo hii; Isaka na Rebeka walikuwa na hali ya sintofahamu hata kusababisha makubwa yaliyo mabaya kwa watoto wao Esau na Yakobo, Wazazi hawa walileta mgawanyiko mkubwa kwa watoto. Kwa maana Isaka alimpenda Esau na Rebeka alimpenda Yakobo, imeandikwa;
“ Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na Rebeka akampenda Yakobo ” Mwanzo 25:28
Hii ni sawa na kusema Esau alikuwa kipenzi cha baba na mdogo wake alikuwa kipenzi cha mama. Sasa hapo ndipo mgawanyiko unapoanza kuonekana, kwa sababu watoto wawili wa baba mmoja na mama mmoja lakini kila mmoja ana mtu wake ampendaye! Haikutakiwa kuwa hivyo!!! Kama Esau akifanikiwa kuleta zawadi kwa wazazi wake basi ni dhahiri atamletea kwanza baba yake kitakachobakia ndicho apewe mama au mama akose kabisa!!! Angalia Yakobo naye kama akifanikiwa kuleta zawadi atamletea mama na kitakachobakia apewe baba au akose kupewa kabisa! Je si wazazi wameleta mgawanyiko? Ebu fikiri zaidi kama Esau atakuwa na familia yake na Yakobo vivyo hivyo, Je wataelewana hawa? Maana tangu utoto waligawanywa. Au fikiri tena kama baba angelikufa mapema huku mtoto ampendaye akiwa hai Je hatanyanyapaliwa / hatatengwa na ndugu yake au mamaye?
Epu chukua picha hiyo hiyo ya Isaka na Rebeka kama wazazi alafu ilete leo kwenye mazingira ya kwako nyumbani kwenu. Ndio tuseme baba yako anampenda ndugu yako mmoja sana kuliko wengine alafu mama akampenda mwingine. Je si shida hiyo? Na ndivyo ilivyo hata sasa! Utakuta baba anampenda mtoto mmoja sana kuliko watoto wengine yaani hata huyo mtoto akikosea yeye baba haoni makosa, tena mbaya zaidi anamtetea. Kwa hiyo mtoto anayependwa na baba kwa kiwango hicho, utakuta “ anavimba kichwa ” ( anajiona yeye ndio kila kitu) ujawahi kuona mambo haya?
Mbaya zaidi mtoto katika ukuaji wake hawezi kuwaona wenzake ni bora au ni watoto kama yeye alivyo. Mara nyingi sana atawadharau na kuhakikisha ya kwamba yeye ndiye awe mtoa ripoti yote ya mambo ya familia kwa siku nzima. Wakati baba ajapo kutoka kazini, mtoto apendwaye ndiye atakayeeleza ni nani kavunja kioo, ni nani katukana, ni nani kaongea na mama, yaani ni nani kakosea. Sio kapatia, bali nani hasa kakosea ili kusudi baba atoe adhabu. Tena wakati mwingine mtoto anasababisha hata baba kumkemea mama au kumpiga. Lakini haya yote ni kwa sababu ya wazazi wamependa watoto wao kimafungu mafungu, hawajui kufanya hivyo kunawaharibu watoto pamoja na kuleta mpasuko wa kifamilia.
Kwani unafikiri mpasuko wa kifamilia unaanzaje? Ni hivi hivi, yaani kidogo kidogo hatimaye huyu aongei na huyu na yule haongei na yule. Ukiwa ni mzazi ; jifunze kuwapenda watoto wako wate sawa, hata kama unaona mtoto wako mmoja si mtiifu, lakini wewe mzazi usioneshe unamchukia kisha na kuwapenda wengine. Tena usiseme “huyu ndio kidume, bhana lazima nimpende kuliko dada zake, wao si wataolewa tu… ” Ishiii,!!!! Maneno ya kipuuzi hayo, kwani unajua atakaye kusaidia baadae, unafikiri ni huyo mtoto wa kiume? Ahaa wapi, huwezi kujua ni yupi atasimama na wewe, kwa maana watoto wote ni sawa. Ukifanya hivyo, ujue utaigawa familia yako hapo baadae!!! Shida hii inatatuliwa na pendo la usawa kwa watoto wote.
Ikiwa kwenye familia yako kuna sampuli fulani za mipasuko ya namna hii, ebu nijulishe sasa, ili tuombe wepesi na kufuta hiyo hali maana kwa Mungu hakuna linaloshindikana. Namba zangu zipo hapo juu kabisa ( mahali palipoandikwa mafundisho ya neno la Mungu)
Kwa mawasiliano zaidi piga Kwa +255 683 877 900
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Comments