top of page

HAKI ITAKUINUA.

Updated: Aug 30, 2022


Tabia kuu ya “ haki” ni kutetea/kuinua / kutoa baraka (Zab.5:12). Haki ni tabia ya Mungu aliyowarithisha wateule wakeKwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki,Apenda matendo ya haki,Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.” Zab.11:7.


Yeyote anayesimama kwenye haki,hakika atainuliwa tu kwa maana “ Haki huinua taifa;…” Mithali 14:34. Anayekupigania/kukuinua ni Bwana,lakini haki iwe ni fungu lako. Kumbuka hili; mwenye haki ajipiganii yeye mwenyewe,wala hajitetei mwenyewe hata kama anaonewa bali mwenye haki katikati ya mwovu,hunyamaza na kumwacha Bwana asimame badala yake ( Zab.103:6)


Tazama mfano mzuri kwa Bwana wetu Yesu Kristo,mtu mwenye haki alisiyejipigania ( hali alikuwa na uwezo wa kujitetea) lakini alinyamaza na kuruhusu mapenzi ya Mungu yatimie. Mara nyingi ukijitetea hali ukiwa ni mwenye haki,utashindwa hiyo vita kwa sababu kuna mahali utajikwaa tu katika usemi wako. Yesu anayajua haya,ndio maana hakuona kitu cha maana cha kujitetea hata pale aliposemewa uongo mara nyingi,wakamshtaki,bali alinyamaza. Unafikiri Yesu alikuwa ni mjinga? Lah! Yeye ni Bwana mwenye uweza kuliko yule anayemshtaki,lakini ili atufundishe kitu kwa habari ya haki,ilimbidi anyamaze,naye atulie kwenye haki tu na hapo ndipo penye mapenzi ya Mungu.


  • Huna sababu ya kupambana kimwili


Adui wa kuharibu haki yako ni namna ya kupambana kimwili juu ya chchote unachoonewa ama unachopita. Ukiwauliza wengi waliofeli/walioshindwa vita,watakwambia kwamba walipambana kimwili hali wao ni watu waliomjua Mungu. Lakini kwako,ukitaka kuona ushindi juu ya hilo,basi mruhusu Bwana aingilie kati katika maombi yako kisha usije ukanyanyua mdomo wako wala kupambana kwa namna yoyote kwa jinsi ya dunia hii.


Kwa maana ukumbuke katika upambanaji wa moto “dawa ya moto si moto,bali ni maji” hii ikiwa na maana, kama mmoja amepanda juu yako,wewe shuka na hapo utamshinda vizuri bila kuumizana,lakini ukijaribu kupanda kama alivyopanda hapo ujue uharibifu mkubwa utatokea na baadae utajuta kwa nini usingelishuka na mambo yangeliisha mapema kabisa.


  • Haki inazuia uharibifu / Magonjwa ya kuambukiza (Kwa wana ndoa)


Pale unapogundua kwamba mwenzi wako hajatulia,basi hapo kinachohitajika kwako ni kusimama kwenye haki/ kuchunga njia zako. Tambua kwamba; Ugonjwa hauna nguvu kwa mwenye haki. Hata kama huyo asiyetulia akiwa na ugonjwa wa kuambukizwa,lakini wewe njia zako zikawa na Bwana basi ujue huwezi kuambukizwa magonjwa hayo hata kama mtakuwa mnakutana kimwili/mnashiriki tendo la ndoa. Dawa ya kumfanya atulie mwenzako ni “ haki” tu,na si kulipiza,kwa maana wapo watu ambao na wao sasa wanatoka nje ya ndoa kwa sababu wenzi wao na wanatoka,kumbuka matokeo ya malipizi ni “mauti ” . Isiwe hivyo kwako.


  • Jifunze kutawala hasira na uchungu


Neno linasema; Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka Waefeso 4:26. Hii ina maana kwamba, hasira ipo tu,lakini lazima ujue namna ya kuitawala,isije ikakusababishia kutenda dhambi. Hata Uchungu usije ukachukua nafasi ndani yako kiasi cha kusababisha kumkosea Bwana. Ikiwa umefanyika kuwa mwenye haki kwa kuokoka,basi ni vyema ukaishinde hasira,tena usiruhusu uchungu kukaa ndani yako hata siku ya pili.


Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kwa hasira na hatimaye kubeba uchungu, lakini sivyo ambavyo mwenye haki anapaswa awe. Kumbuka “ hasira ” ni roho ya shetani yenye kubeba mauti. Ikiwa ni hasira ni roho,basi unahitaji msaada zaidi wa maombezi ili kusudi roho ya uchungu,na hasira zikuachie (Maana Haki itakuinua ikiwa utaishinda hasira,na kutokubeba shina la uchungu)


Kumbuka;


Ili Bwana akupiganie katika changamoto hiyo,utulivu unahitajika sana,ukisimama kwenye haki,hakika utauona mkono wa Bwana kikamilifu,hata wengine watashangaa!!!. Ujapoachwa,wewe simama kwenye haki tu,Bwana atahusika na hali hiyo na utauona ushindi. Ama ujapoonewa kwa namna yoyote ile,hata hapo usipande bali simama kwenye haki tu.


Unajua wengi hatuwezi kutulia tukiwa kwenye mazingira magumu,na ndio maana vita inakuwa ni yetu na si ya Bwana kwa kuwa tunataka kupambana tuwezavyo na kuzuia nafasi ya Bwana kutupigania.

Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe.


Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900


What’s app + 255 746 446 446


Na Mch. G. Madumla.


UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page