top of page

GEUZA MITANDAO YA KIJAMII KUWA MADHABAHU YA BWANA.


Bwana Yesu asifiwe

Kwa ufupi,

Mtazamo tulionao kuhusu mitandao ya kijamii ni mtazamo usio sawa,kwa maana wengi tunaitazama mitandao ya kijamii kama sehemu ya uhuni na uchafu wa kila namna. Ni kweli kabisa kwamba mitandaoni kuna uhuni mkubwa unaofanywa kiasi kwamba kama umeokoka ukisikia ishu ya mtandao,inakuchefua!!!. Lakini ufahamu kwamba katika mitandao ya kijamii kuna nafasi ya kuitumia vyema na ikakulipa vyema. Kwa maana si wote wenye kuitumia kihuni,kuna wachache wanaoitumia vyema,na wanafanikiwa.

Neno mitandao ya kijamii humaanisha mitandao kama “ Fecebook,twiter,Instagram,Whatassp,Tango,Imo,N.K ” Hata hivyo mitandao ya kijamii ipo mingi sana kwa maana kila siku watu hufikiri ni kwa namna gani wataweza kufungua mitandao mipya ya kijamii.

  1. Lengo mama la mitandao ya kijamii ni “mawasiliano”. Katika mawasiliano,kuna mengi tunaweza kuyaona yanayofanyika katika mitandao hii;

  2. Matangazo / Biashara,

  3. Mapenzi,

  4. Uhalifu,

  5. Habari ,

  6. Michezo /games,

  7. Kwa ajili ya Neno la Mungu. N.K

Ukiangalia takwimu ya matumizi ya mitandao ya kijamii,utagundua asilimia kubwa ya matumizi ni katika mawasiliano nje ya wokovu/nje ya Neno la Mungu. Takwimu hii inapatikana kwa kuangalia tu ni kwa jinsi gani watu wanatumia mitandao ya kijamii,mfano ni kwa kiwango kipi FB,inatumika,au Whatsaapp anatumika,au Instagram n.k. Lakini uzuri ni kwamba wewe unaweza kugeuza matumizi yako ya kawaida na kwa kumuhubiri Kristo. Leo Dunuia imepindukia kwenye mitandao ya kijamii kwa kiwango kikubwa,kwa maana ukitaka kuwapata watu,basi watafute kwenye mitandao ya kijamii na huko utawapata wengi tu. Tena ukitaka kuwapelekea injili watu wengi,tumia mitandao ya kijamii kwa injili na uwe na uhakika wataipata injili hiyo. Leo imefikia wakati watu wamekimbia kutoka makanisani na kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii,sasa nawe endenda huko huko walikokimbilia uwapelekee injili ya Bwana.

  1. Kwa nini wengi wanashindwa kuitumia mitandao kwa ajili ya Bwana?

01. Mitazamo isiyosawa.

Ukweli ni kwamba shetani amefunga ufahamu wa walio wengi na kuhakikisha wanakuwa na mitazamo isiyo sawa kuhusu mitandao ya kijamii. Kwa maana wapo watumishi wa Mungu ambao mpaka sasa wanaitazama mitandao ya kijamii kama chaka la wahuni! Hivyo kwa mtazamo huo,wanajizuilia kuingia huko,kumbe wangeliingia huko huko wangelifanyika msaada zaidi kwa kuwatoa wale waliopotea. Lakini wengine watumishi,wamefungwa ufahamu kiasi kwamba wanaitumia mitandao ya kijamii kama watu wasiookoka! Kwa hivyo lengo mama la matumizi sahihi halifanyiki. Kwa hiyo,changamoto kubwa ni mtazamo isiyosawa ndio usumbua wengi hata kushindwa kuzama mitandaooni.

02.Elimu waliyoipata.

Elimu ndio utengeneza mitazamo. Kwa kile unachotazama sasa ujue kwamba kimetokana na uelewa wako wa elimu uliyoipata. Hivyo elimu,kama elimu,inawakwamisha sana watu kutumia mitandao ya kijamii ipasavyo. Cheki elimu yako uliyonayo,alafu angalia ni nini unachoona,na kuamini. Wengine wamezuiliwa kimafundisho na walimu wao wa kidini,au wazazi au walimu wengine. Kwa hiyo elimu isiyofaa imewazuia!

03. Kwa historia ya walioshindwa!

Wapo wengine wamekwamishwa na wengine waliowatangulia ambao walishindwa kuitumia vyema mitandao ya kijamii na watu hao wakajikuta wameharibikiwa maisha yao. Sasa wale wanaotaka kuanza,wanapoangalia ushuhuda wa waliowatangulia,basi na wao hawawezi kutumbukia humo kwenye mitandao kwa sababu wanaofia wasije wakaanguka kama watangulizi. Elimu bora inahitajika kugeuza imani zao.

  1. Je ni kweli mitandao inaweza kuwa madhabahu ya injili ya Bwana?

Jibu ni ndio,inawezekana kuitumia mitandao kama madhabahu ya kuhubiri na kufundisha neno la Bwana. Mfano wa wazi ni kama mahali hapa kwenye mtandao unaousoma sasa,mimi nimegeuza matumizi yasiyofaa na kisha nikatumia mahali hapa kama madhabahu ya Neno la Bwana. Na hakika ninaona matunda yake mazuri kwa maana kupitia mahali hapa,Yesu amewapa wokovu wengi,wengi wameombewa,wengi wamelejezwa kwa Bwana. Kumbe inawezekana kabisa!!!! Lakini Je ni watumishi wangapi wanafanya jitihada hizi? Laiti kama kila mtumishi akajifunza namna ya kutumia ukurasa wake wa mtandao kwa ajili ya injili ya Bwana,hakika wengi wangehubiriwa kwa wepesi kule waliko,na kungelikuwa na kanisa moja lenye nguvu,kanisa litembealo /mobile church.Anza sasa,fungua Face book,instagramu,whatsapp,n.k kisha kusanya watu,na peleka Neno la Bwana,ili pamoja tuungane kama kanisa la Bwana. Hii ni neema iliyofunguliwa bure,itumie vyema sasa.

Ikiwa kama umebarikiwa,nifahamishe tumtukuze Mungu pamoja. Kwa msaada zaidi na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900

What’s app namba +255 746 446 446

Na. Mch.G. Madumla.

UBARIKIWE.

Recent Posts

See All
JIANDAE NA MAFUNDISHO YAJAYO.

“ Shalom mpendwa… Ninajua ya kwamba umekuwa ukifuatilia masomo mengi katika uwanja huu. Mungu azidi kukubariki na kukuinua. Tulikuwa...

 
 
 

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page