FUNGA KINYWA
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 22, 2015
- 3 min read
Updated: Sep 2, 2022

Mtu mmoja alinipigia,akaniambia makosa ya mchungaji wake. Bali nilimwambia “hupaswi kumnyooshea kidole masihi wa Bwana” . Ajapokosa wewe chukua hatua ya kupiga magoti kwa Mungu kusudi Mungu mwenyewe aliyemuweka ashughughulike naye. Najifunza kwa habari ya Daudi,mtu ambaye aliinukiwa na boss wake Sauli,lakini Daudi hakurudisha mashambulizi wala hatusomi kwamba Daudi alimsema kwa hila Sauli na huo ndio moyo mzuri.
Ni kweli mtumishi huyo ni mwanadamu,na kama ni mwanadamu basi ni dhahili kutawa na makosa /udhaifu tu kama mwanadamu wa kawaida kwa maana hakuna aliye na mazuri asiwe na mabaya/kasoro. Lakini shida si kasoro zake bali shida ni kwa namna gani unazifanyia kazi?
Wakati mwengine unajikuta badala ya kutafuta baraka kwa mtumishi/kiongozi wako wa kiroho na hatimaye ukatafuta laana kwa sababu ya kushindwa kutumia kinywa chako ipasavyo. Kumbuka; Kumsema mchungaji wako/ama mtumishi wa Mungu hakupendezi isipokuwa kama utasema kwa lengo la kutafuta msaada kutoka kwa Bwana. Mfano; Mtu anayesema kasoro za mtumishi katika nia njema ni lazima atasimama naye kwenye maombi kwa mzigo na atajitahidi kukitawala kinywa chake.
Hivyo ujumbe wa leo,unaangazia namna ya kufunga kinywa chako kwa kiongozi wako hasa kiongozi wa kiroho awe ni baba au mama wa kiroho. Kwa sababu moja ya shida kubwa inayotusumbua wengi ni namna ya kinywa chetu tunavyokitumia kwa wazazi wetu wa kiroho,pale tunapoona kwamba hawaendi vyema au awaendi tunavyotaka sisi,sio atakavyo Mungu bali tutakavyo sisi ambao tu watoto wao.
Shida hii tunayoiangazia sio shida kutoka kwao,bali kutoka kwa watoto wa kiroho kwenda kwa baba/mama wa kiroho.
Mara nyingi tumesikia lawama nyingi kutoka kwa washirika/watoto wakilalamika juu ya baba/mama zao wa kiroho. Watoto/waumini wanataka baba/mama yao aende kama watakavyo wao,au wafundishe kama wanavyotaka wao kufundishwa.
Kwa hiyo kama baba/mama wa kiroho akipewa ujumbe na Bwana,na watoto wanauchunguza mara mbili mbili,na kama hawauelewi basi badala ya kumwomba Mungu awasaidie,hapo ndipo huanza kunyanyua vinywa na kumsema vibaya kiongozi wakiona kwamba kiongozi huyo hayupo sawa na wengine wanafikia wakati wakisema kwamba “baba yetu hayupo rohoni kabisa!!…
” Sasa hiyo si mbaya? kama unagundua kwamba baba/mama yako wa kiroho hayupo sawa ndio uitishe mkutano wa kumsengenya? Je kwa kufanya hivyo utamsaidia ama utaendelea kumuhumiza na yeye?
Wakati mwingine tunaangamizwa kwa laana tunazozitafuta wenyewe kwa kuwa na vikao vingi vya kusengenya juu ya kazi ya Mungu inayoendelea. Unajua ni watu wangapi wamekwama kwenye huduma zao kwa sababu ya kusema vibaya huduma za wengine? ama kwa kusema vibaya juu ya watumishi wengine? sasa kwa namna hii,tutafikaje? Ikiwa wewe unainuka na kuninenea mabaya mimi na huduma yangu,kisha hapo hapo unataka Mungu akluinue katika huduma yako,Je Mungu atakuinuaje? Ikiwa wewe hukubali huduma za watu wengine?…
Wakati mwingine kiongozi wako anaweza akawa ni mtu wa duniani kabisa,tena wala hana mpango wa kuokoka,lakini ni kiongozi wako hapo kazini,au katika jamii. Sasa wewe kwa vile unajua mtu huyo hajaokoka basi unajikuta ukijikwaa mara nyingi katika kumsema vibaya hali ni kiongozi wako,ujui kwa kufanya hivyo unajipalia makaa ya moto kichwani pako? kwa maana siku akijua naye atakuchukia kisha wewe utamwona ni shetani,kumbe shetani ni wewe mwenyewe uliyeshindwa kutumia kinywa chako vizuri.
Kwa habari ya kunena mabaya,tunanena lakini je suluhisho lake li wapi? Maombi ni muhimu pia kujifunza kufunga kinywa pale inapobidi,la ukifungua basi iwe ni kwa mema. Kutengeneza viakao vya siri vya kusengenya ni hali mbaya kiroho na inashusha / inaondoa uwepo wa Mungu ndani ya mtu.
Kumbuka;
Hata kama unajua kwamba mtumishi fulani ni fake basi wewe usiwe sababu ya kushikilia bango bali wewe funga kinywa,Bwana atashughulika naye,nawe mwombee,kisha wewe kuwa Original ili fake ipotee yenyewe,chukua hiyo!
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe.
Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga sasa kwa + 255 683 877 900
What’s app number +255 746 446 446
Na Mch. G. Madumla.
UBARIKIWE.
Comments