EBERI KIZAZI CHA SHEMU, CHANZO CHA NENO WAEBRANIA.
- Mch. Gasper Madumla
- Jul 11, 2018
- 1 min read
Bwana Yesu asifiwe…
Kwa ufupi sana.
“ Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.” Mwanzo 11:16
Nuhu mtu aliyepata neema machoni pa Mungu, na aliyemwamini Mungu. Mtu huyu alikuwa na hofu na Mungu kiasi kwamba utii wake ulikuwa mkubwa. Lakini haya yote ni kwa neema tu ya Mungu. Nuhu alikuwa na watoto watatu ambao biblia inawataja kwa mujibu wa malango ya kiroho, kuanzia Shemu, Hamu na Yafethi. Hawa watatu walikuwa chimbuko la makabila / mataifa. Hata hivyo mpango wa Mungu ulipitia kwa Shemu.
Shemu alikuwa na kizazi yaani watoto mbali mbali. Mtoto wa kwanza anaitwa Arfaksadi. Naye Arfaksadi akazaa na kizazi kikaendelea( Mwanzo 11:10). Kizazi cha tatu (kama lango) kinaitwa Eberi. Eberi naye akazaa na kizazi kikaendelea mpaka kwa Abramu ambaye baadae aliitwa Ibrahimu. Eberi ni babu ya Ibrahimu mwenye jina ambalo kwa mara ya kwanza tunaliona kwa Ibrahimu, jina “ Mwebrania” likitumika kwa Abramu. Abramu hapo kwanza aliitwa “ Abramu Mwebrania ” ( Mwanzo 13:14). Hii ikiwa na maana Abramu ni mmoja wa mzao wa Eberi mtoto wa Shemu. Na katika uzao wa Ibrahimu ni watu wa Eberi au Wa-Ebrania, kizazi kikubwa kabisa. Hivyo jina hili lilipanuka kimaana hapo baadae kwa kubadilika mazingira, muongezeko wa watu n. K kwa mfano, Neno kama Myahudi ( Yaani watu kuto ,au Isaeli, likachukua nafasi.
Kwa mawasiliano piga + 255 683 877 900
What’s app ni +255 746 446 446
UBARIKIWE.
Commentaires