DHAMBI YA UCHAWI.
- Mch. Gasper Madumla
- Jan 24, 2020
- 3 min read
Updated: Aug 30, 2022

Tafsiri ya kiroho ya uchawi ni utumiaji wa nguvu za giza katika kudhuru kitu ama mtu chini ya utawala wa ibilisi shetani. Uchawi hutegemea imani kwa miungu/ibilisi na majini yake ili kusababisha uharibifu wa kuchinjaji,kuua, kubomoa n.k. Ushirikina ni chanzo kimoja wapo cha uchawi kwa maana ushirikina ni hali ya kutoa imani kwa Mungu na kuamini miungu.
Katika biblia,uchawi ni moja wapo ya dhambi mbaya ya mauti kwa maana uchawi ni machukizo makubwa kwa BWANA Mungu. Agano la kale limetaja dhambi tatu za mauti ambazo afanyaye moja ya dhambi hizo,itampasa auwawe,dhambi hizo za mauti kwa mujibu wa agano ni kama ifuatavyo;
Kuabudu sanamu
Kujamiiana na mnyama
Uchawi.
Hayo matatu yalikuwa hayana msamaha kabisa,Bwana Mungu alipotoa sheria zake,hakutaka kabisa mambo hayo yafanyike. Lakini hata hivyo watu wengine walifanya kwa kuwa walikuwa na shingo ngumu,na hatimaye walikufa wote. Uchawi haukuanzia sasa,ulikuwepo tangu enzi za zamani za watu. Watu wengine walimwacha Mungu na kugeukia uchawi wakidhani watafaidika nao,na hatimaye walilipwa mauti.
Usimwache mwanamke mchawi kuishi (Kutoka 22:18)
Kwa mujibu wa sheria,mtu mchawi alistahili kifo. Huyo mchawi,Awe ni mwanaume ama mwanamke hakuwa na utetezi wa namna yote ile isipokuwa mauti ilimuhsu. Mauti hiyo,ilikuwa ni mauti kabisa kabisa ya kufa kimwili na kuzikwa. Hii yote ni kuonesha “uchawi”ni machukizo makubwa ya Mungu.Uchawi umebeba picha ya “chuki,kumwacha Mungu” tafsiri ya agano la kale ni mchawi asiishi kabisa,tafsiri hii ni kivuli cha tafsiri mama ya agano jipya.
Katika agano jipya,hatajapewa mamlaka ya kuua mtu hata kama ni mchawi,isipokuwa tumepewa mamlaka ya kuua uchawi ambayo ni roho iliyo ndani ya mtu aitwaye mchawi ( Luka 10:19). Ndani ya mtu mchawi kuna roho ya uchawi hiyo,lazima tuiue kwa kuipiga kimaombi.
Hatuwezi kuiacha roho ya namna hiyo ikaendelea kuishi. Lakini tunapaswa kumweleza wazi wazi mchawi pasipo kumwogopa kwamba, aache uchawi wake lakini akikataa maonyo na mafundisho ya Neno la Mungu basi ataenda pamoja na uchawi wake ( kufa na atakufa,kwa maana uchawi utakapokufa hautamwacha na yeye).
Kwa maana uchawi ni dhambi ya mauti!Kumbuka; Mtu mchawi ni mtu wa giza,na mtu wa Mungu ni mtu wa nuru,kwa hiyo haiwezekani kuishi pamoja watu wa namna hii! Lazima giza lijitenge na nuru. Ikiwa kama unaishi na uchawi na unaona upo salama,tambua kwamba haupo salama.
Mauti hamwachi mchawi.
Ikiwa uchawi utakuwepo mahali fulani,basi ujue mauti ipo hapo pia. Katika kipindi hiki cha neema Bwana ametoa nafasi ya kiupendeleo kwa wachawi kusalimisha mambo yao,watubu na kuiamini injili,waokoke nao wataishi. Dhambi ya uchawi ni kama dhambi ya kuabudu sanamu,kwa maana zote mbili zinatoa kipaumbele kwa miungu.
Kwa kuwa neema ya kurejea ipo,watu wameizoelea hiyo neema na kuona kwamba wanaweza wakaishi hali ni wachawi,lakini ni lazima watu wajue kwamba neema haizoeleki hata mara moja kwa maana Mungu ni yule yule,aliyesema mwanamke mchawi asiishi ndiye yule yule anayeagiza watu watubu na kuiamini injili ya Bwana. Tanasema uchawi ni dhambi ya mauti kwa sababu ni machukizo makubwa,lakini inasameheka ikiwa itatubiwa.
Kwa nini ibilisi akutumie kuua?
Hakuna haja ya kuua,wala hakuna haja ya kutumia uchawi ikiwa Bwana yupo mtoshelevu wa kila kitu. Lakini tunafahamu kwamba wapo wengine “wanatumika katika uchawi pasipo kupenda,wengine hawajijui “. Tumeshuhudia wengi wakitumika katika uchawi bila wao kujua kama wanatumika. Wengine wao wamejikuta wakiota ndoto za ajabu ajabu,wakiwa makaburini au wakiwa kwenye miti mirefu na wanakula nyama za watu,au wanaua kabisa,kisha wakiamka wanajikuta ni kana kwamba walikuwa kweli kwenye tukio halisi,na waliyoyaona yanakwenda kutendeka.
Kutumika kiuchawi,ni lango baya linapaswa kutubiwa lakini kuuliwa uchawi huo katika maombi yenye nguvu! Inawezekana kuepukana na dhambi ya uchawi,tena inawezekana ukaombewa na roho ya uchawi ikatoka,hujachelewa bado!. Ikiwa kama unaishi na mtu mchawi, basi usikubali uchawi ukaishi,bali lazima uchawi ufe naye aelezwe anachokifanya aache mara moja.
Ikiwa umebarikiwa,nifahamishe na kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI nipigie sasa+255 683 877 900
What’s namba +255 746 446 446
Na Mch.G. Madumla.
UBARIKIWE.
ความคิดเห็น