DHAMBI.
- Mch. Gasper Madumla
- Apr 3, 2019
- 2 min read
Updated: Sep 2, 2022

Dhambi ni nini?
Unaposikia neno “dhambi” unapata picha gani? Unapomwona mtu aliyetenda dhambi,unapata picha gani?Kila mmoja anamtazamo wake tofauti na mwingine katika neno hili “dhambi”,wengine husema hivi na wengine vile,lakini mtazamo ulio sahihi juu ya dhambi ni ule mtazamo wa kibiblia “biblical truth”. Biblia inatazama dhambi kama uasi,kutokutii sheria za Mungu. Hivyo dhambi ni “ kuasi maagizo ya Mungu – 1Yoh.3:4” “ni kutotii/disobidient sheria za Mungu/neno katika mawazo,maneno au matendo- 1Samweli 15:23”.
Dhambi imetokea wapi?
Nini asili ya dhambi? – Kabla ya shetani kuwa shetani,alikuwa ni malaika wa sifa. Lakini alimwasi Mungu. Kwa kuasi kwake,dhambi ikaanzia hapo. Hivyo dhambi haikuanzia kwenye bustani tu bali ilianzia kwa aliyekuwa malaika kwa kuasi kwake,naye ndiye shetani /Ibilisi. Hata hivyo,ibilisi akapenyeza uasi kwa Adamu na Hawa,nao wakaanguka kwa kutotii maagizo ya Bwana (Mwanzo 3:1-7). Ibilisi alijaribu kuwaaminisha akina Adamu na mkewe hasa kupitia mwanamke Hawa maana yeye ndiye aliyedanganwa (1 Timotheo 2:14),kwamba endapo wataenda kinyume na maagizo ya Mungu hawatakufa,nao wakaanguka katika kutotii. Na dhambi ikaingia ulimwenguni mwote na kwa dhambi hiyo mauti ikawafikilia wote (Warumi 5:12)
Dhambi usababishwa na nini?
01. Hila za ibilisi.- Shetani ndio msababishi wa kwanza kukufanya uingie dhambini,yeye alikuwa mtenda dhambi tangu hapo zamani. Ukweli ni kwamba ibilisi yupo kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu,hivyo yoyote uyafanyayo ni lazima ukutane na ukinzani wa ibilisi. Kazi aifanyao ibiilisi ni kuiba,kuchinja,kuharibu (Yoh.10:10) – yeye ni mwuaji tangu zamani.
02.Tamaa ya mtu – Ingawa nyuma ya tamaa mbaya yupo ibilisi,lakini mwanadamu anatamaa nyingi ambazo zinazompeleka kwenye dhambi, “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. ” Yakobo 1:14-15
Aina za dhambi
Dhambi ya Adamu na Hawa (Kutokutii)- Dhambi hii ilishughulikiwa pale msalabani,hata hivyo kwa yeyote aliye nje ya msalaba wa Bwana (Asiyemwani Kristo/asiyeokoka) anahusika moja kwa moja na dhambi hii,lakini pia dhambi inakuwa na nguvu ndani yake
Kutokumwamini Yesu ni dhambi – Yoh.3:16-18
Dhambi ya mauti- 1 Yoh.5:16
Dhambi zingine/Matendo ya mwili – Wagalatia 5:19-21
Matokeo ya dhambi.
Mauti/kifo -Ezekieli 18:20,Mwanzo3;19
Mateso na maangaiko ( Kama vile magonjwa mengi huja kwa sababu ya dhambi,Yoh.5:1-14,Zab.103:3)
Kujitenga na uso wa Mungu -Isaya 59;2. Kumbuka hili,hakuna dhambi ya namna yoyote itakayokutenga na upendo wa Mungu,bali Mungu bado anatupenda sote. Ila ukifanya dhambi ni wewe unayekimbia mbali kwenye uwepo wa Mungu,lakini hata hapo bado pendo la Mungu kwako bado lipo na ndio maana anakutarajia urejee.
Kuikosa mbingu ikiwa kama utaendelea kudumu hapo kwenye dhambi. (1 Wakorintho 6:9-11
Nini kifanyike?
Kazi ya msalaba ilikuwa ni kushughulikia dhambi hasa nguvu ya dhambi isiendelee tena kutawala kwa watu wa Mungu. Kupitia msalaba,Yesu alitufia dhambi ili mimi na wewe tuwe huru. Kumbuka pia,Asameaye dhambi ni Mungu,lakini pia Yesu anayo amri ya kusamehe dhambi (Luka 5:20),Hata;hivyo yafuatayo ni mambo muhimu unayoweza kuyafanya;
Kumwamini Kristo na kurejea kwake kwa njia ya toba (Yoh.3:16 ,Matendo 2:38)
Kumwomba Roho mtakatifu akusaidie-
Kumbuka;-Ikiwa kama ulikwisha mwamini Kristo na ukahesabiwa haki(ukaokoka),na dhambi imekuwa kwako ni mzigo mzito ambapo mara nyingi umekuwa ukitubia tubia mara kwa mara na kujikuta bado dhambi kwako ina nguvu.Basi hapo ujue hapo unahitaji msaada zaidi wa Mungu,kwa kuonana na mchungaji mkae na kuangalia ni nini kinachoendelea kwako.
Ikiwa kama umebarikiwa, nifahamishe. Kwa msaada zaidi pamoja na huduma ya MAOMBI piga kwa namba hizi hizi; +255 683 877 900
What’s namba .+255 746 446 446
Na Mch. G.Madumla
UBARIKIWE.
Comments