top of page

CHUKI.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi;

Neno hili“chuki”ni neno dogo sana lakini lina matokeo makubwa sana. Sikudhani kama “chuki” limebeba mambo mengi kiasi hiki. Hivyo ni vyema tutafakari kuhusu “chuki ” ,ili tupone! Awali ya yote chuki ni kinyume cha upendo. Na ndio maana ukisikia mtu akisema “fulani anakuchukia…” basi maana yake “fulani hjakupendi..”. Hata hivyo,tunaweza kuitasfiri tena chuki kama hisia mbaya ndani ya moyo dhidi ya mtu mwingine.

Kwa mujibu wa Neno la Mungu,tunapaswa kuchukia uovu,na sio kumchukia mtu “ Enyi mmpendao Bwana, uchukieni uovu; Huwalinda nafsi zao watauwa wake, Na kuwaokoa na mkono wa wasio haki. ” Zab.97:10,Soma pia Zab.119:104,Waebrania 1:9 n.k . Uovu kama shina la ubaya,ndilo jambo pekee ambalo unaelekezwa uchukie. Ukiwa unampenda Bwana,huna budi kuchukia uovu wa aina yoyote ile. Wakati mwingine mtu anaweza akawa ni mtenda maovu,lakini bado hujaambiwa umchukie huyo mtenda maovu,bali chukia maovu ayatendayo na huyo mtu umpende.

Ikiwa ndio hivyo,kwa nini basi wewe ambaye ni mtumishi wa Bwana unamchukia mtumishi mwenzako kwa mema yake? Kwa nini hata unamchukia ndugu yako si kwa mabaya,bali kwa mema ayatendayo? Ebu fikiria; mtumishi mmoja anadiriki kumchukia mtumishi mwenzake anayehudumu naye kwenye madhabahu moja ya Kristo,anamchukia kwa mema wala si mabaya! Hii ni ajabu sana!!!!! Umeshawahi kuona mkristo akimchukia mkristo mwenzake tena kwa mema,Sasa unajiuliza,inakuwaje hapo? Yaani ikiwa wewe unahudumu pamoja nami kisha mimi ninakuchukia hali wewe hujakosea lolote lile,tena unatenda haki na unafanya kazi ya Bwana ipasavyo lakini bado nakuchukia!!! Kwa nini hali inakuwa hivi? (kinyume na kile tulichoagizwa kwenye neno la Mungu)

  1. Sababu kubwa ya mtumishi wa Mungu kuchukia mtumishi mwenzake pasipo ubaya ni “wivu ”

Hakuna kitu kibaya kama wivu,hasa ndani ya kanisa la Bwana. Kwa maana wivu ndio unamfanya mtu mmoja ambaye ni mtumishi kabisa,kumchukia mwenzake ambaye kainuliwa hapo kanisani. Kwa hiyo anajiuliza,kwa nini kainuliwa yule,kwani ana nini ambacho yeye hana? Kwa hiyo mtu mwenye wivu hawezi kumpenda mtumishi mwenzake kwa sababu tayari wivu umekomaa na kujenga chuki.Angalia kwa kakazake Yusufu watu ambao walikuwa wanamchukia Yusufu kwa sababu wivu uliwakaa sana hata wakapanga mabaya ya kuua (Matendo 7:9). Mimi  nakuuliza,kwa nini umwonee wivu mwenzako aliyeinuliwa? Kwani na wewe si upo wakati wako? Kwa nini umchukie mtumishi mwenzako? Ikiwa unamchukia mkristo mwenzako,Je utaweza kumpenda adui yako?

  1. Biblia inasema nini kuhusu chuki? (Biblia inasemaje kuhusu mwenye chuki?)

01.Mwenye chuki,hajaokoka kwa maana bado yupo gizani –“ Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.” 1 Yoh.2:9,soma 1 Yoh.2:11. Kumbe! Ukisema umeokoka,na huku unamchukia mlokole mwenzako,basi wewe utakuwa bado upo gizani,hujaifahamu kweli !

02.Mwenye chuki ni mwuaji – “ Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. ” 1 Y oh.3:15. Ebu tafakari wewe mwenyewe kuhusu mstari huu unaotisha sana. Kumbe yeyote anayemchukia mtu,ni mwuaji. Sasa fikiria tuna wauaji wangapi kanisani? Watu ambao huingia na kutoka katika nyumba ya Bwana lakini kumbe ni wauaji wakubwa! Mungu atusaidie kwa kweli! Unajua unawezaukawa unaongozwa na mwuaji hapo kanisani kwa sababu ya chuki tu! sasa fikiria jinsi ya maongozi yatokayo kwa mwuaji yatakuwa vipi?

katika ujio wa Kristo alisema “ lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ” Mathayo 5:44.  Mimi nauliza tena ; kama mtu wa Mungu hawezi kumpenda mtu wa Mungu mwenzake,anawezaje kumpenda adui yake? Ukweli ni kwamba,haiwezekani! Hivyo,kile alichokisema Yesu,ni kigumu kwa mtu anayemchukia ndugu yake,kwa maana hawezi kumpenda adui yake wala kumwombea mema. Kumbe,ili ufanikiwe kumpenda adui yako,itakulazimu kwanza umpende ndugu yako/mkristo mwenzako. Jiulize wewe mwenyewe ni mara ngapi umemtakia mabaya adui yako? Je ni kweli ndivyo Yesu asemavyo? Jiulize,ni mara ngapi hata umemwomba Mungu amtendee mabaya huyo adui yako!!!! Je ni kweli ndivyo ulivyoambiwa na Bwana? Umepata wapi sasa,maombi ya ajabu ajabu ya namna hiyo?

  1. Dawa ya chuki.

Dawa ya chuki ni moja tu nayo ni “kumpenda Mungu”. Kwa sababu ukimpenda Mungu,hata ukawa na hofu naye,basi ujue utampenda na jirani yako pia. Na ukimpenda jirani yako,huwezi kumchukia. Kwea kulitambua hili,Yesu alitupa amri kuu na ya kwanza nayo ni “Kumpenda Mungu” Marko 12:30)

Ikiwa kama umejifunza kitu, nifahamishe na Kwa msaada zaidi piga;Kwa msaada zaidi pamoja na MAOMBI piga kwa+255 683 877 900

What’sapp namba .+255 746 446 446

Mch. G. Madumla.

UBARIKIWE.

Comments


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page