top of page

CHANZO CHA DINA BINTI YAKOBO KUBAKWA.


Bwana Yesu asifiwe…

Kwa ufupi.

Moja kati ya jambo baya katika jamii yoyote ni tendo la kumdhalilisha mwanamke. Hakuna jamii inayoweza kuvumilia udhalilishaji/unyanyasaji wa kijinsia.Hata zamani unyanyasaji wa kijinsia ulipigwa vita vikali pamoja na kwamba kulikuwa na watu ambao waliendesha mfumo dume. Maadili ya zamani yalikuwa ni rafiki kwa mabinti,na kwa sababu hiyo unyanyasaji wa kijinsia ulikuwepo kwa kiwango kidogo sana ukilinganisha na siku hizi. Kwa sababu siku hizi maadili yamepolomoka sana kuanzia ngazi ya familia.

Dina mtoto wa Yakobo abakwa! Tukio baya la udhalilishaji  kutendeka kwa binti wa Kiyahudi. Lakini ukiona binti kabakwa basi kuna sababu zilikuwepo. Sababu hizi zinaweza kupatikana katika upande wa binti au mbakaji au wazazi,bila kusahau ibilisi kama chanzo kikuu. Katika kila pande utakuta kuna sababu zinazochakia kubakwa kwa Dina binti Yakobo,na kwa sababu hizi tunaweza kujifunza kitu ili kusudi tuchukue hatua ubakaji ukome. Ebu tusome habari hii;

Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kuwaona binti za nchi.  Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri. Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa maneno mazuri.” Mwanzo 34:1-3

Biblia inasema “akatoka kuwaona binti za nchi” maana yake alijichanganya na kwenda kujiunganisha/kuwasabai mabinti wa kimataifa. Mchanganyo huu ndio sababu kubwa ya kwanza ya kubakwa kwake,(nami nataka nibakie kuelezea sababu hii moja tu). Hii inaonekana hawa binti za nchi,hawakufanana hata kitabia na Dina. Kwa hiyo kuna roho/mambo aliyapata ambayo hakuwa nayo hapo mwanzo.

Kutoka na kwenda nje ya hema” kulifungua lango kwa adui Shekemu hata kumwona na kupanga mipango mibaya ya kubaka. Hili ni fundisho kwako! Ukitoka na kujichanganya na “mabinti wa nchi” ujue utanaswa na adui,kwa sababu umeingia kwenye 18 yake. Shekemu alikuwa hajamwona Dina (labda hajamwona kwa ukaribu na kuona uzuri wa binti wa Kiyahudi,mtoto teketeke,mrebo-hatariiii),

lakini Dina alipojichanganya tu kwa “ kutoka” Lah!! Jamaa akaona chombo hiyoooo,naye akatimiliza lengo lake baya. Ebu fikiria kama Dina angeendelea kubaki hemani,hivi Shekemu angembaka? Biblia inasema mpingine shetani naye atawakimbia tena tusimpe nafasi ibilisi !! Lakini ukimpa nafasi adui basi ujue “atakukimbilia akudake kabla hujafika ” na atakumaliza hapo hapo kabla hujapoa!!!!. Leo tuna visa vingi vya mabinti kubakwa kule walipoenda,yaani walipojichanganya tu,basi akina Shekemu awafanyi uzembe,wanabaka fasta!.Wakina Shekemu wapo wengi wakutosha.

Hivi unajua ya kwamba binti habakwi hemani? Ndio bali atabakwa akiwa nje ya hema,tena akijichanganya kwenda kwa binti za nchi,basi ujue hawezi kurudi salama!!! Kisa hiki kinatuonesha kwamba mwenye makosa ni Dina binti Yakobo,kwa maana bila shaka alikuwa akijua imani ya baba yake na taifa zima kwamba ni watu wa Mungu waliotengwa na waovu. Tulia hemani /Stay in camp

Tena bila shaka alifundishwa maadili ya kutunza usichana wake na ndio maana aliweza kuwa bikira kwa muda wote huo. Kwa hiyo mwenye jukumu hasa la kuzuia kubakwa ni mwanamke mwenyewe. Kwa upande wa Dina alichemka! Yakobo baba’ke alimfundisha yote mambo muhimu.

Shekemu adui wa Dina/Israeli baada ya kutimiza lengo lake,biblia inasema “moyo wake ukaambatana na Dina,akampenda” Kwa nini asingempenda tangu mwanzo na ampende baada ya kumwingilia? Nini kilichomfanya Shekemu ampende Dina? Je ni penzi moto moto alilopata hata kumbikiri binti wa watu? Bila shaka ni penzi la mtoto wa Kiyahudi aliyekosea likamchanganya mmataifa huyu asiyetailiwa. Kumbuka kumbe hata adui anayekutafuta akikupata,naye ana data / anachanganyikiwa Duh!!

Tunajifunza kitu kikubwa hapo,kwamba ikitokea binti kabakwa au katembea na kijana,basi ni rahisi moyo wa kijana kuambatana na binti. Katika kuambatana huku,kuna roho,binti lazima apokee kutoka kwa kijana. Ndio maana unaweza kuona hata leo kwa mabinti ambao walianza vizuri na Bwana,lakini walipompa nafasi adui na kujikuta wameangukia kubakwa,au kulala na kijana,basi wanakuwa na mapepo hatariii. Tena ukimwombea binti wa namna hii ndio utajua ninachokisema hapa.

Lakini biblia inasema huyu mbakaji “akawa anasema naye Dina kwa maneno mazuri” Hii ni kuonesha kwamba mbakaji tendo alilolifanya ni la kawaida kabisa,ni sawa na kusema alikuwa akimpooza Dina achukulie kawaida tendo la kubakwa! Adui ibilisi naye hufanya hivyo,kwa maneno kana kwamba ni mazuri lakini mwisho wa maneno hayo mazuri ni mauti!!! Jifunze kwa Dina,wewe usije ukabakwa au ukabaka!

Kwa msaada zaidi pamoja na maombezi +255 683 877 900

What’s up .+255 746 446 446

Na mch. Gasper Madumla.

UBARIKIWE.

댓글


Post: MAFUNDISHO

Follow

  • Facebook
  • Twitter

©2022 by MAFUNDISHO YA NENO LA MUNGU. Proudly created with Wix.com

bottom of page